Wafugaji 50 waliopotea kwenye Pori la Akiba la Selous wapatikana wakiwa hai

Mko 50 mifugo 1780 mnakufa njaa? Waafrika tuna tatizo la kuthamini na kuonea ubahili vitu ambavyo vinatakiwa kutuokoa wakati wa shida.

Ulitaka wamuuzie nani kule porini? Wamekuambia walikuwa wakila nyama za ng'ombe wao lakini wakakosa maji, unawalaumu kwa lilpi? Tumia akili basi.
 
Hilo kundi la ng'ombe likiingia kwenye shamba la mahindi kwa kweli hakibaki kitu!,Hawa watu nawapa pole lakini maeneo mengi wamewasababishia wakulima kadhia kubwa na wengine kupata vilema na kuppteza maisha...
 
Unaonaje wangetumia hayo mamilioni waliompa mzee mzigua na hata ikibidi kuongeza pesa kidogo wakodi maroli kuliko hiyo adha waliyoipata? Ndio maana huyo jamaa anawalaumu
wasukuma bahili sana kutumia hela kwa mambo wanayodhani sio ya msingi..
Ina maana hawakuwa hata na simu yenye GPS ikawapa uelekeo
walikuwa wanazunguka porini in circle
 
Hao jamaa nao buana...
Kama walikuwa na ng'ombe hiyo njaa wameipata wapi yani wanachinja ngombe kisha wanakunywa damu tu hata kama waliwaacha ina maana walishindwa hata kuchoma na kubeba nyam huko walikoelekea...
 
Aisee wafe njaa wakati wana ngombe.Walishindwa kuchinja ngombe wale .
 
Huyo aliyewaingiza chaka lazima ni mkulima,hiyo inaitwa passive resistance.

Halafu hoja ya kutoka kununua ng'ombe ni changa la moto tu hao wanaswampa tu baada ya kuharibu mazingira ya watu huko Rufiji.
 
Inasikitisha sana the. Way walivyohaso ila tatizo wafugaji nao hawajielewi wanang'ang'ania kuwa na nifugo ming'ombe mingi mwisho WA cku ndio wanahangaika kuhamahama wauze tu waangalie maisha mebgine
 
Labda walishindwa kupata moto!
..yani walishindwa hata kufanya kama hawa jamaa wakaupata huo moto..
1483694983158.png
 
Tatizo una mawazo ya kizungu....mali kwako ni gari nyumba....wamasai ni tofauti na usitulazimishe tuamini unachoamini
Kiukweli haujanielewa.
Uhai ndiyo unatakiwa utangulie katika vyote ulivyotaja hapo. Ikitokea siku kwa mfani jambazi ananitolea bunduki kisa gari nitaliachia.
Ikitokea siku tupo 50 na tuna mifugo 1780 hautakufa njaa ukiwa na mimi.
 
poleni sana kwa kupotea sijajua ilikuwaje kwa sababu wawindaji hutumia jua linapochomoza wanajua huu ni upande Fulani linapozama hujua tuko mahali Fulani .
 
Ulitaka wamuuzie nani kule porini? Wamekuambia walikuwa wakila nyama za ng'ombe wao lakini wakakosa maji, unawalaumu kwa lilpi? Tumia akili basi.
Soma mpaka mwisho. Hivyo vinyesi walivyokua wanakula hujaona hizo aya?
 
Unaonaje wangetumia hayo mamilioni waliompa mzee mzigua na hata ikibidi kuongeza pesa kidogo wakodi maroli kuliko hiyo adha waliyoipata? Ndio maana huyo jamaa anawalaumu

Nililiangalia kuanzia walilpokuwa stranded porini, sasa wameishiwa maji na chakula wanaanza kuchinja ng'ombe kunywa damu na mikojo, nikalinganisha na hoja ya jamaa akisema kwa kuwa walikuwa 50 na mifugo 1,700+ hawakupashw akupata njaa porini. Kule wangefanya biashara na nani? Hata wangelikuwa nafedha zisingeweza kuwasaidia.

Walikuwa katika wakati mgumu sana.
 
Back
Top Bottom