Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,584
- 1,189
WAFANYABIASHARA DODOMA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA UJENZI WA MACHINGA COMPLEX
▪️Jiji kujenga sakafu kupunguza nguvu
▪️Mbunge Mavunde awachangia 10m kutunisha mfuko wa Soko
▪️Awataka Mgambo wa Jiji kuacha kutumia mabavu
▪️Aahidi kuwaunganisha na Taasisi za fedha kwa ajili ya mitaji
▪️DC Shekimweri aahidi kusimamia utatuzi wa kero sokoni
𝐃𝐨𝐝𝐨𝐦𝐚
Wafanyabiashara wadogo wa Soko la Machinga Complex Jijini Dodoma wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa namna ilivyowahamisha kutoka barabarani na kuwajengea soko maalum maarufu kama Machinga Complex.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa soko Kaimu Mwenyekiti wa Machinga Complex Ndg. Lucas Kingamkono ameishukuru serikali kwa uwepo wa soko la Machinga ambalo limerahisisha ufanyaji wa biashara kwa wafanyabiashara hao wadogo ambao awali walikuwa maeneo ambayo hayakuwa rasmi na hivyo kufanya biashara kwa mashaka.
Akizungumza katika mkutano huo,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde ameupongeza uongozi wa soko Kwa kuandaa mkutano wa kusikiliza kero za wafanyabiashara ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi kutunisha mfuko wa soko kwa kuchangia Tsh 10m.
Mbunge Mavunde ameahidi kusaidia upatikanaji wa mikopo kwa wafanyabiashara hao kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji na Taasisi za Fedha na kutumia fursa hiyo kuwataka askari mgambo wa Jiji kuacha kutumia mabavu makubwa kushugulika na wafanyabiashara wadogo.
Naye Mkuu wa wilaya ya Dodoma Alhaj Jabir Shekimweri ameahidi kusimamia na kushugulikia utatuzi wa kero na changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa soko la Machinga Complex ili kuweka mazingira bora ya biashara.