Theodor herzl
Member
- Nov 10, 2021
- 95
- 225
Sasa gari la 2017 toyota Fortuner bei rand 250,000/: ambayo ni 38,750,000/: kule be forward utakuja mil.50 fortuner la japan, bado Ushuru , kumbe africa kusini ukiwa na taarifa sahihi unapata gari bei nzuri sana na hakuna garama kubwa ya kusafirisha kama ilivyo japan, kwa sasa Africa kusini ndo pa kwenda kununua gari za kazi kama hilux kwa sisi wafugaji , Japan wanauzia umaarafu ILA south africa ndo Habr ya mjini kwa wale risk taker.Hizo zinauzwa kuanzia rand 250 000 kuendelea mpaka rand 350,000 muda mwingi wauzaji wanakua na documents za SA kwa hiyo kuingia Tanzania wanatumia kama kuja kutembea unapewa miezi mitatu au sita unalipia unalipia hicho kibali na Bima mteja akifika bei yeye ndio anaenda kulipa kodi gari ikishakua ndani ya Nchi..ukitaka kununua gari yenye Reg ya SA ndani ya Tanzania nenda nae Police kitengo cha magari ya kutoka Nje wanalikagua hiyo karatasi utakayopewa utaitumia kuwapa TRA kwa ajili ya kulipia kodi wengine huko hawaendi hata kama gari sio la kona atapata usumbufu ila ukiwa mpakani utaonyesha documents za kutoka SA ili ulipie ukiwa ndani unaonyesha zile za SA na wao walikague gari ukiruka kimoja ndio mnasema Interpol wamekuja kumbe ni hao hao Polisi wa Tanzania wapo kwenye kazi hiyo...
Sent from my TECNO B1g using JamiiForums mobile app