Wadada wengi wanajiuza kijanja janja

Nov 6, 2016
73
182
TUNA CHANGAMOTO KUBWA SANA YA MABINT WANAJIUZA KIJANJA JANJA

Na Comrade Ally Maftah
JITU LA MIRABA

Baada ya kupitia changamoto za kutengana na aliyekuwa mke wangu, nilianza heka heka za kutafuta replacement yake, hapo ndipo nilipokutana na masarakasi ya kunifanya kujifunza kwamba dunia inazunguka.

Uzoefu wa kwanza ni kwa wale wanawake waliokuwa machoni mwangu nikasema sasa hapa nashika nilipopashika kwanza, nikawa naanzisha uhusiano wa hao kwanza,

Mwanamke akiniona kwa mbali anasema yes nimelipata bwana la nguvu, hapa laki laki hazikosekani, anajichomeka kumbe sisi wengine uchawi wetu ni sabuni na tabasamu tu muda wote tunacheka na mitumba yetu tunajitahidi kuifikicha fikicha.

Mdada anaingia kwenye uhusiano unamwambia mipango ya kutafuta pesa anakwambia live mwanamke anataka matunzo babu, mimi natongozwa na wengi sijaja kutafuta pesa, ulivyonitongoza hukujua kama kuna kuhudumia, basi unakatazama kadada kameshalamba kama hamsini elfu, unatamani ukadunde jabu moja la mgongo unagundua Paulo na Hasila waliomba maombi usiyoyaweza ndipo milango ikafunguka.

Nikasema sikubali ngoja nikawatafute waliopo kwenye Dating Site, nikajua hawa wana utayari goma itakuwa ni kuziandaa kadi za harusi tu, uzuri designer na printer ni mimi mwenyewe, huko nako vituko havikuisha, mwanamke anataja bwana anayemtaka ukijitazama kwenye kioo unasema huyu anamtaka Comrade Ally Maftah, mrefu, mweusi, msomi, mchapakazi, nasema humo nimefiti.

Haya mama tukae tupange suala letu wewe si unatafuta mchumba, twenzao beach comber bili nitalipia, pale hesabu zangu 5000, hata awe anabeba na mishkaki haiwezi kuzidi.

Mwanamke kwanza anasema hana nauli, sio mbaya naweka 5000 lingine au nikufuate ulipo, ukipiga simu tena ohh nilishindwa kukupigia niungie na vocha, isiwe tabu 2000 hiyo, unga na bando ukija beach uperuzi peruzi.

12000 inakuwa imekatika, akifika sasa anavyokuhoji kuhusu uwezo wako wa kipesa utafikiri dalali anataka kukuuzia nyumba ya watu ya urithi, unajiuliza huyu ndio alokuwa akitafuta mchumba huyu.

Kifupi ni kwamba dada zetu wengi sasa hivi wanadanga, wanatumia mitandao kudanga, na wengine wanatumia ujanja wa kuwazungusha zungusha wanaume hata watano, ukizidisha mapenzi anakukata speed anakuwa kama dereva wa ndege, mtindo huu upo kwa mabinti wa 2000, hawa wanaweza wakawa na mlolongo wa wanaume wanaotongoza kama 10, ukimtongoza hanyooshi maelezo anakuweka kati, hakubali na wala hakatai wewe unaona ngoja niendelee kunogesha penzi, hawa hawakupigi mizinga mizito, wanakupiga miba miba tu, ili akikwambia hakutaki usimsumbue, na jichanganye baba umbuguzi hapo hakuna sheria itakulinda, jamii yote itakukataa.

HUO NI UTAFITI WANGU, HASIRA ZAKO USINILETEE MIMI, MWENZIO BADO NASAKA SAKA

Ndimi Comrade Ally Maftah
JITU LA MIRABA
CHALINENEE
 
Attachments

  • IMG-20240504-WA0129.jpg
    IMG-20240504-WA0129.jpg
    57 KB · Views: 3
Nyie vijana wa miaka hii mna kampeni yenu ya "KATAA NDOA" mtaendelea Sana kupata shida kwenye maisha yenu....hiki kizazi chenu cha 90's na 2000's nawaonea huruma sanaa
 
Utafiti wa kisomi kabisa very interesting umejaribu kuutafuta kweli Kabisa Dada zetu ndio walivyo sasa mbayazaidi wanawatetezi kibao
 
Wanawake wengi wana michezo hio endapo atakua hajakudadisi vizuri ila akijua doo ipo, mbona hamna kesi.
 
Chimbuko la haya yote ni ugumu wa maisha.

Tanzania idadi ya watu inazidi kuongezeka, huku wanawake wakiwa wengi kuliko wanaume.

Kazi zimekuwa za shida, huku elimu ikididimiza uwezo wa kufikiri na kukoleza uoga haswa kwa wanaume.

Hivyo, watu wanazaa watoto na kushindwa kuwahudumia ipasavyo.

Binti hana ujuzi mwingine zaidi ya kuvaa na kupendeza, na ili apendeze anatafuta madanga (wanaume) ili awezeshwe.

Wanaume waoji nao tumepungua kwa hiyo mabinti wengi wanazalishwa na kuachwa, na hivyo wengine wanaona bora kuchuna na kusepa tu.

Maadili nayo ni zero, mabinti hawaelimishwi umuhimu wa ndoa kwa sababu wengine wamelelewa na mzazi mmoja (haswa mama na au bibi).

Jamii imeporomoka sana katika Karne hii ya 21.

Sisi tuliyozaliwa 70,80 na 90 mwanzoni ndiyo tunayashangaa haya ila hawa wa 90 mwishoni na 2000s ndiyo watoto wetu na hayo ndiyo waliyojifunza kwetu.

Lawama kwa watoto wa 2000 zinapaswa ziende kwa wazazi wao ambao ni wazaliwa wa miaka ya 70s hadi 90 mwanzoni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom