Wadada wanapendelea zaidi marashi ya kiume kwa sababu huwa yananukia vizuri

Mkuu mbona mi nilinunua lakini inanuka vibaya? ni original kabisa kwani niliingiza batch namba yake kwe mtandao ikaniletea jina. Pia nilii-scan kwa barcode.
Nzuri ni ipi? yenye alcohol au free alcohol.?!
Aisee achana na hiyo ya kwenye mitandao kama upo Dar pita mlimani city itafute hata hawa jamaa wa S H Amons wanakuaga nayo ama Jd pharmacy ,harufu yake sio mbaya Mkuu ,labda hiyo haikua yenyewe
 
Katika kukutana na kuongea kwangu na baadhi ya wadada, iwe hapa bongo na hata ughaibuni, nimeshasikia wakisema kuwa wao wanapendelea zaidi marashi [pafyumu, deodorant, na body sprays] ya kiume kwa sababu huwa yananukia vizuri.

Niliwahi kuwa na mfanyakazi mwenzangu mmoja hivi aliyewahi kunambia kuwa yeye hutumia viondoa harufu [deodorant] vya kiume.

Nilimshangaa kidogo pindi aliponambia hivyo. Niliona ni kitu cha ajabu kwa sababu sipati picha njemba kutumia marashi ya kike.

Baadaye tena nikakutana na mdada mwingine naye akanambia kwamba yeye anapenda kutumia 'pafyumu' za kiume. Nikaguna kidogo...halafu nikamkumbuka yule mfanyakazi mwenzangu.

Basi, nikadhani labda ni hao wawili tu. Siku moja niko nyumbani chumbani nasikia mlango unagongwa....kuuliza nani huyo? Nikasikia sauti ya dada binamu...eti anaomba kujipulizia unyunyu wangu wa Bottega Veneta!

Kumwuliza kwa nini unataka unyunyu wangu ambao ni wa kiume? Nikapata jibu lilelile...eti unanukia vizuri! Khaaa!

Sasa nikabaki najiuliza....hivi ni kweli marashi ya kiume wadada wanayependa kihivyo?

Ningependa kusikia toka kwa wadada wa JF pia kama haya niliyoyasikia ni ya kweli.

Karibuni.....
Nawewe paka ya kike
 
Ni kweli kabisaaaa.. Marashi ya kiume yana harusfu nzuri na pleasant kuliko ya kike. Marashi mengi ya kike yana harufi kali sana inayokera. Sikumbuki kuwahi kununua marashi ya kike, siku zote natumia ya kiume. Nikiketewa zawadi na mtu marashi ya kike huwa nagawa. I can't stand the smell from marshi ya kike
 
Back
Top Bottom