Wabunge waliobebwa kwa mbeleko mwaka 2020 hali ni tete, Arusha mjini na Mbeya mjini kimeumana

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,873
11,123
Dollar za kimarekani ziliadimika hivyo ilifanya biashara kwetu wakinga kuwa ngumu kidogo na Mimi pia nilikaa kimya kutafuta dollar ili kuweza kuagiza mizigo ya biashara, Kwa bahati nzuri hata Nairobi nao dollar ilikuwa shida kwao.

Turudi kwenye mada kwa sisi wana CCM na mambo yanayoendelea.

Mrisho Gambo wa Arusha mjini na Dkt Tulia Ackson wa Mbeya mjini kuwashambulia wana CCMwenzenu hakuwezi kuwasaidia kushinda Ubunge 2025,Mngeyafanya hayo wakati ule Rais ni Rais na Mwenyekiti ni Mwenyekiti kweli kweli.

Ndani ya CCM hali ni shwari na bahari imetulia, Hali ni mbaya na tete kwa Wabunge waliobebwa kwa mbeleko ya Mwenyekiti wa wakati huo mwaka 2020 na Bashiru Ally, Hili ni kundi lililoingia Bungeni kwa kulazimisha matokeo.

Hawa watu hawakuwa na Sera wala ushawishi wowote ule mbele ya Wajumbe wa CCM asilia na mbele ya wapiga kura bali nguvu na hofu ya Mwenyekiti kwenye Uchaguzi wa mwaka 2020 ndio walipata nafasi za Ubunge.

Sasa wameanza kupinga kila kitu na kuhoji ili kuonyesha utofauti kuwa wao si wa kundi la mbeleko.

Mimi ni muhanga niliyeponea chupu chupu kukatwa kwenye kura za awali za wajumbe ingawa wajumbe walinikubali hivyo sikubebwa kwa mbeleko bali uwezo wangu binafsi na wala siogopi uchaguzi wa 2025.

Jambo kubwa alilolifanya Samia ni kuhitimisha mpango wa pale Lindi, Rais Samia aliamua kulizika rasmi kundi la Sukuma Gang kwa kumuondoa mtendaji mkuu na mratibishaji muhimu wa pale Lindi.

Kuondolewa kwa Katibu Tawala pale Lindi Bwana Ngusa Samike ndio ilihitimisha rasmi kambi ya kubebwa kwa mbeleko yaani Sukuma Gang.

Katika hali ya kawaida kwenye kura za maoni hakuna mtu wa kuweza kumkata Andrew Chenge Ubunge ni Mwenyekiti tu.

Arusha mjini na Mbeya mjini ni ngumu sana kwa CCM kushinda, Arusha mjini na Mbeya mjini sio maeneo ya kuleta porojo kama Singida au Newala huko.

Arusha mjini na Mbeya mjini watu wametengeneza loyalty kwa upinzani iwe shida au raha

Katika maeneo ambayo upinzani hautumii nguvu ni Kawe Dar es Salaam na maeneo yote yenye watu wanaojitambua.

Ahaaa Nakumbuka Mwita Waitara alivyoamua kukimbia Ukonga Dar na kwenda porini huko alifahamu fika Ukonga Dar sio sehemu za poroja za CCM.

Soma Pia:
Arusha mjini CCM twende na nani kwenye ubunge 2025?
Spika Tulia ana wakati mgumu jimboni Mbeya (M) mwakani

Baadhi ya Majimbo kama jimbo langu upinzani hauwezi kushinda kabisa sio kwa sababu ya fitina bali wananchi wanaambiwa ukweli kuhusu miradi itakayofanyika na ambayo haitafanyika, Hakuna porojo.

Ukweli unabaki ukweli mwezi wa pili, tatu na huu nne Nimewaambia wananchi wangu kuna shida ya dollar za kimarekani tukitaka kuagiza bidhaa hivyo wananchi wangu wote wanafahamu wafanyabiashara wana shilingi lakini dollar za kuagiza bidhaa unapata kwa mgao.
 
Mimi ni mwana ccm hivyo hata wakishinda hakuna tatizo, Nina ongelea kugombana na wana ccm wenzao na kuwasagia kunguni hakutowasaidia

Ukiwa ndani ya ccm kwa sisi wazee tunasoma upepo na kuchagua upande kwa tahadhari kubwa
Kwa hiyo GUSSIE unataka tukuamini kwamba huna upande CCM?

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo GUSSIE unataka tukuamini kwamba huna upande CCM?

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
Kila mtu anatafuta pesa na anataka awe na maisha atakayo

Upande una kuwa nao lakini kwa akili kubwa sana

Mfano Leo Samia ni Rais, Unapaswa kumsifia sana Samia lakini usijaribu kumtukana mtu mwingine hujui kesho yako ni ipi

Mrisho Gambo anawasagia kunguni viongozi wa ccm Arusha

Dkt Tulia anataka kuonyesha Mwigulu Nchemba ni mtu wa hovyo
 
Kwa neno SUKUMA GANG kwako ni neno la heshima kumuuita mwana CCM mwenzie?
 
Kwa neno SUKUMA GANG kwako ni neno la heshima kumuuita mwana CCM mwenzie?

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
Mimi nilimsifia JPM sana hapa JF lakini sikuwahi kukubaliana na watu wanaopotea

Sukuma Gang sio tusi, Ni neno linaloakisi falsafa ya mtu fulani yaani tabia na mwenendo hivyo wafuasi wa hiyo falsafa huitwa hivyo

Kuna falsafa za Max, Aristote, Mao Zedong na Wengine wengi

Mimi sio muumini wa ukabila na udini, Nakubali ukiniuliza dini yangu na kabila langu kwa lengo la utani na kutaniana maana kuna makabila wapenda pesa, makabila wapenda mademu, Makabila ngangari au ngunguli na makabila rojo rojo kama watu wa pwani

Sukuma Gang ni falsafa ambayo watu kama Mrisho Gambo, Makonda na Sabaya waliifuata na kufanya waliyoyafanya
 
Kwanini iwe SUKUMA GANG, naona hapo juu umetaja falsafa za watu sio kabila au jamii fulani.
 
Mfano Leo Samia ni Rais, Unapaswa kumsifia sana Samia lakini usijaribu kumtukana mtu mwingine hujui kesho yako ni ipi

Mrisho Gambo anawasagia kunguni viongozi wa ccm Arusha

Dkt Tulia anataka kuonyesha Mwigulu Nchemba ni mtu wa hovyo
Kama Ccm Arusha inamfanyia Gambo fitina, ana haki ya kulalamika....japo na yeye alitumia hizo hizo fitna kuupata Ubunge.

Ccm ndio itakayolinda Ubunge wa Tulia hapo Mbeya... uchaguzi hauwezi kumzuia katu.
 
Kwa nini iwe SUKUMA GANG, naona hapo juu umetaja falsafa za watu sio kabila au jamii fulani.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
Sukuma Gang ni watu waliamini hakuna kufa yaani kiongozi wao ni alfa na omega

Waliamini hakuna mwenye akili nchi hii zaidi yao

Waliamini Maendeleo ya nchi hii yameletwa na mtu mmoja tu wa awamu ya tano na Wengine hawakufanya kitu awamu zote

Hawa waliamini wapo juu ya sheria na katiba ya nchi

Wana mambo mengi Sukuma Gang nikisema yatakuchefua
 
Kwanini watanabishwe na kabila la watu na sio wao wenyewe na matendo yao?
 
Mimi ni mwana ccm hivyo hata wakishinda hakuna tatizo, Nina ongelea kugombana na wana ccm wenzao na kuwasagia kunguni hakutowasaidia

Ukiwa ndani ya ccm kwa sisi wazee tunasoma upepo na kuchagua upande kwa tahadhari kubwa
kwa point izo skubishii mkuu🙏
 
Dollar za kimarekani ziliadimika hivyo ilifanya biashara kwetu wakinga kuwa ngumu kidogo na Mimi pia nilikaa kimya kutafuta dollar ili kuweza kuagiza mizigo ya biashara, Kwa bahati nzuri hata Nairobi nao dollar ilikuwa shida kwao

Turudi kwenye mada kwa sisi wana ccm na mambo yanayoendelea

Mrisho Gambo wa Arusha mjini na Dkt Tulia Ackson wa Mbeya mjini kuwashambulia wana ccm wenzenu hakuwezi kuwasaidia kushinda ubunge 2025,Mngeyafanya hayo wakati ule Rais ni Rais na Mwenyekiti ni Mwenyekiti kweli kweli

Ndani ya ccm hali ni shwari na bahari imetulia, Hali ni mbaya na tete kwa wabunge waliobebwa kwa mbeleko ya Mwenyekiti wa wakati huo mwaka 2020 na Bashiru Ally, Hili ni kundi lililoingia bungeni kwa kulazimisha matokeo

Hawa watu hawakuwa na Sera wala ushawishi wowote ule mbele ya wajumbe wa ccm asilia na mbele ya wapiga kura bali nguvu na hofu ya Mwenyekiti kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 ndio walipata nafasi za ubunge

Sasa wameanza kupinga kila kitu na kuhoji ili kuonyesha utofauti kuwa wao si wa kundi la mbeleko

Mimi ni muhanga niliyeponea chupu chupu kukatwa kwenye kura za awali za wajumbe ingawa wajumbe walinikubali hivyo sikubebwa kwa mbeleko bali uwezo wangu binafsi na wala siogopi uchaguzi wa 2025

Jambo kubwa alilolifanya Samia ni kuhitimisha mpango wa pale Lindi, Rais Samia aliamua kulizika rasmi kundi la Sukuma Gang kwa kumuondoa mtendaji mkuu na mratibishaji muhimu wa pale lindi,

Kuondolewa kwa Katibu tawala pale lindi bwana Ngusa Samike ndio ilihitimisha rasmi kambi ya kubebwa kwa mbeleko yaani Sukuma Gang

Katika hali ya kawaida kwenye kura za maoni hakuna mtu wa kuweza kumkata Andrew Chenge ubunge ni mwenyekiti tu

Arusha mjini na Mbeya mjini ni ngumu sana kwa ccm kushinda, Arusha mjini na Mbeya mjini sio maeneo ya kuleta porojo kama Singida au Newala huko

Arusha mjini na Mbeya mjini watu wametengeneza loyalty kwa upinzani iwe shida au raha

Katika maeneo ambayo upinzani hautumii nguvu ni Kawe Dar es Salaam na maeneo yote yenye watu wanaojitambua

Ahaaa Nakumbuka Mwita waitara alivyoamua kukimbia ukonga Dar na kwenda porini huko alifahamu fika Ukonga Dar sio sehemu za poroja za ccm

Baadhi ya majimbo kama jimbo langu upinzani hauwezi kushinda kabisa sio kwa sababu ya fitina bali wananchi wanaambiwa ukweli kuhusu miradi itakayofanyika na ambayo haitafanyika, Hakuna porojo

Ukweli unabaki ukweli mwezi wa pili, tatu na huu nne Nimewaambia wananchi wangu kuna shida ya dollar za kimarekani tukitaka kuagiza bidhaa hivyo wananchi wangu wote wanafahamu wafanyabiashara wana shilingi lakini dollar za kuagiza bidhaa unapata kwa mgao
Dogo acha uongo na vijihabari vya kuungaunga. Kuna jamaa ana hela anakuja hapo kwa wapiga kura masikini. Umechota mafao yako yote sasa hivi unawakimbia waliokukopesha.

Kusanya Kandambili urudi porini
 
Kila mtu anatafuta pesa na anataka awe na maisha atakayo

Upande una kuwa nao lakini kwa akili kubwa sana

Mfano Leo Samia ni Rais, Unapaswa kumsifia sana Samia lakini usijaribu kumtukana mtu mwingine hujui kesho yako ni ipi

Mrisho Gambo anawasagia kunguni viongozi wa ccm Arusha

Dkt Tulia anataka kuonyesha Mwigulu Nchemba ni mtu wa hovyo
Yah ndivyo mlivyo wana CCM, mpo kwa ajili ya matumbo yenu tu yaani mpo kwa ajili ya kujinufaisha binafsi.

Huwa nashangaa sana wale wanaosema WANASIASA fulani fulani wapo kwa ajili ya kutetea maskini!! HAO WATU HAWAPO !

KILA MTU NI MBINAFSI.
 
Jitetee wewe mwenyewe kwanza

Jifunze kusoma kwanza halafu utasaidiwa vitabu

Unataka vitabu wakati kusoma hujui
 
Back
Top Bottom