Wabunge wahoji uhalali wa Magufuli kuhamamisha fedha za Muungano, kujengea barabara Mwanza

Huu muungano jinsi wanavyo udharau cha ajabu wanau ng'ang'ania kupita kiasi..
why wasiuvunje?
 
Kuna Bomu linapikwa na wahafidhina hapa, tusijeshangaa bajeti kukwama, na bunge kuvunjwa, na uchaguzi kuitishwa na chama flani kikateuwa mgombea mwingine.
hiyo hawawezi kwanza hao chama chao ndiyo kula yao,bila chama kufa njaa ni kugusa tu.
 
Ila ukweli, Mh. Anaendesha nchi kama anaendesha familia yake, kilichopatikana mda huo huo kinapangiwa matumizi, hamna plan wala nini, sikosoi utendaji wake, hakika tumepata raisi, ila tunataka mpango madhubuti wa mda mrefu

Majipu endelea kuyatumbua baba, ila mambo ya fedha na mengineyo pia jaribu kuachia wahusika, kila mtu awajibike panapostahili, mkono wako unagusa kila mahali sidhani kama kuna ambaye ataenda kinyume au tofauti na inavyokusudiwa
Kuna fact moja kuhusu nchi hizi za dunia ya chini. Tukiwa na rais mwenye maono ni rahisi sana kuendelea na siyo lazima kusubiri vyombo vya maamuzi kama Bunge ambalo pia mara nyingi liko na watu wa hovyo kabisa! Na kwa mamlaka aliyonayao Rais mara nyingi havunji sheria. Ana kazi nyingi sana alizopewa kikatiba.

tatizo ni kama tunapata Rais wa hovyo. Rais wa hovyo anatupeleka kusikotakiwa kiurahisi kabisa na nchi inaanguka. Tukumbuke kwamba jamaa huyu alikuwa mbunge na waziri wakati bajeti iliyopita ilipopitishwa. Lazima aliona vile vifungi vya kipuuzi vinavyopitishwa kwa sauti kubwa. Hata mimi nisingeweza kutojua kwamba pesa ya safari inaweza kuokoa roho za watu hospitali.
 
Kuna Bomu linapikwa na wahafidhina hapa, tusijeshangaa bajeti kukwama, na bunge kuvunjwa, na uchaguzi kuitishwa na chama flani kikateuwa mgombea mwingine.
Kumbuka kura za wabunge zote kwa zote hata mia tano hazifiki, kuna huhakika hao hao waafidhina wasirudi bungeni na magufuli akajiunga na chama kingine akapita kwa jinsi wanainchi na wazalendo wa kweli walio nje na ndani ya serikali walivyo kuwa na imani na mweshimiwa rais. Waafidhina wakijaribu wao ndiyo watakuwa wahanga wa hiyo plan B yao.
 
Baadhi ya Wabunge wamehoji uhalali wa kisheria wa Rais John Magufuli kuhamisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe ya Muungano na kuzipeleka kwenye ujenzi wa barabara katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Wabunge hao walihoji hilo wakati wa semina iliyofanyika jana katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini hapa Dar es Salaam, iliyoendeshwa na Dk Haji Semboja kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Harold Sungusia wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali alihoji juu ya mamlaka ya Rais katika kutumia fedha ambazo zilishapangiwa bajeti na Bunge na kuzipeleka kwenye maeneo mengine.

Alihoji pia juu ya nidhamu ya Serikali katika usimamizi wa Bajeti iliyopitishwa na Bunge.

Mbunge huyo alisema dhana ya mgawanyo wa madaraka haipo kwa sababu Serikali ina nguvu kuliko Bunge na Mahakama hivi sasa.

Alisisitiza kuwa nguvu hiyo ndiyo inayomfanya Rais afanye kitu chochote anachotaka.

Mbunge wa Viti Maalumu, Lucia Mlowe alisema moja ya majukumu ya Bunge ni kuisimamia Serikali, lakini anashangaa kuona yenyewe ikilisimamia Bunge katika mambo mbalimbali.

Alisema hata suala la Rais kuhamisha fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe ya Muungano, ni kuingilia madaraka ya Bunge, kwa sababu fedha hizo tayari zilikuwa zimeidhinishwa kwa ajili ya matumizi hayo.

“Naomba kupata ufafanuzi kutoka kwa wataalamu hapa, Rais ana mamlaka gani ya kuhamisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya jambo fulani? Pia, ni namna gani wabunge tunaweza kuisimamia Serikali kama hamna uwiano kati ya mihimili hii mitatu,” alihoji mbunge huyo.

Akijibu hoja hizo, Dk Semboja alisema Sheria ya Bajeti ya 2015, inampa mamlaka Rais kupeleka fedha katika eneo analoona inafaa.

Alisema sheria hiyo inatoa sharti moja, kwamba Rais kupitia Waziri wa Fedha, atatoa taarifa bungeni juu ya matumizi ya fedha hizo.

Dk Semboja alisema mamlaka hayo yanatambuliwa pia katika Ibara ya 137 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, hivyo Rais hajakosea kuhamisha fedha hizo kwenda kujenga barabara isipokuwa taarifa ya matumizi itolewe bungeni hata kama matumizi yanaonekana.

“Bunge lazima lifahamishwe kuhusu matumizi ya fedha hizo. Kama ni udhaifu wa kipengele hiki, basi unaanzia kwenye Katiba,” alisema Dk Semboja.

Pia, Sungusia alisema, “Fedha ambazo Rais hawezi kuziingilia ni zile zilizo kwenye consolidated fund (mfuko hodhi), nje ya hapo anaweza kufanya lolote,” alisema mwanasheria huyo.

Source: Mwananchi
achananao hao CCM wasituchanga
nye ,Baba magu endelea kuelekeza sehemu unazoona kuwa zinafaa.mabunge ya ccm yamezoea kulakula tu mastomachi makubwa yamejaa haki za maskini,kwa hiyo wanataka kuzila hela za muungano
 
Ila ukweli, Mh. Anaendesha nchi kama anaendesha familia yake, kilichopatikana mda huo huo kinapangiwa matumizi, hamna plan wala nini, sikosoi utendaji wake, hakika tumepata raisi, ila tunataka mpango madhubuti wa mda mrefu

Majipu endelea kuyatumbua baba, ila mambo ya fedha na mengineyo pia jaribu kuachia wahusika, kila mtu awajibike panapostahili, mkono wako unagusa kila mahali sidhani kama kuna ambaye ataenda kinyume au tofauti na inavyokusudiwa
Status quo sio?????
 
Nimeuliza wakati bajeti za hovyo zinapitishwa walikuwa wapi? Kila mwaka bajeti inayopitishwa siyo hiyo inayotumika. Kila mbunge anaelewa na hakuna aliyewahi hoji matumizi ya hovyo na misururu ya safari za US pesa ilikuwa inatoka wapi.

Kwa wema wa magufuli leo hii eti mbunge anauliza juu ya maamuzi ya Rais. Wakati wa Kikwete hakuna aliyeuliza na hata jina lake kutajwa Bungeni ilikuwa marufuku kwa kanuni za Bunge. Lukuvi alikuwa pale kila siku kuzuia jina la rais kutajwa.

Nafikiri nilishakujibu swali lako: "kama huko nyuma kulitokea makosa na wabunge hawakuhoji matumizi ya fedha haina maana hawana haki ya kuhoji maamuzi ya rais hivi sasa...". Pia nimeelezea kufurahishwa na utendaji wa rais (MPAKA SASA), lakini haimaanishi rais awe juu ya sheria. Pili, kama hatafuata sheria yeye mwenyewe ataifanya kazi yake kuwa ngumu zaidi. Kama rais anataka watu wawe na nidhamu makazini kwamfano, kufuata kanuni za kazi au kotopokea rushwa basi yapaswa hata na yeye pia azingatie utawala wa sheria. Anatakiwa aongoze kwa mfano. Ukiwaambia watu wafuate kanuni halafu wewe ukawa unazipindisha inakuwa vigumu kuwashawishi watu ndio maana nikaandika kuwa anaweza kuifanya kazi yake kuwa ngumu.
 
Wabunge wenyewe ni hawa watuhumiwa wa rushwa? Wajifanye kwenda kuleta ujinga wao bungeni waone kitakachowapata baada ya hapa, halafu kuna mazezeta ya upinzani yanawaunga mkono haya mafisi ya ccm kwa ujinga wao, Ccm ina vibaka wengi sana, nusu ya viongozi wa ccm ni majangili, wala rushwa, wapiga dili, hawa ndio wameifikisha nchii hii hapa tulipo, umasikini wa Tanzania una uhusiano wa 99% na ccm, chama kimejaa majinga mengi sasa haya majitu hayapo tayari kuona mambo yao yanafutika.
Mtu anayeweza kusimama kuhoji uhalali wa Rais kupeleka pesa zilizotengwa na hili genge kwenye shughuli za maendeleo ni kirusi kibaya kwa nchi masikini kama hii, haya majitu hayafai kuungwa mkono kwa njia yoyote ile tena watu wenye mbunge wabunge wa namna hii wanatakiwa kuona aibubkuongozwa na jangili. Maamuzi magumu ni pamoja na kufumbia macho visheria vya ajabuajabu vilivyotungwa na genge hili. Tujiukize kwanini walipinga katiba ya Warioba? Ilikuwa kwa maslah ya watu gani na kwanini leo hii.
 
fedha ya nchi anapeleka usukumani kwao uku arusha barabara mashimo matupu
 
Inaonekana watu walishatega Mahomu yao humo sasa wanaisoma namba. Magu waonyeshe maujuzi.
 
Kama wabunge wanahoji tu kwa nini pesa iliyopitishwa na Bunge imehamishwa basi hawana hoja. Tena wanatafuta kuonekana wa ovyo. Serikali, akiwemo, rais inaweza kutaka kubadili matumizi kulingana na dharura au mabadiliko ya vipaumbele.

Wao waishie tu kuhoji kama taratibu zilizoandikwa zimefuatwa. Kwanza wanao ubavu wa kumhoji rais? Na wakitaka Bunge liwe na madaraka yake ya kuisimamia serikali jibu ni kuwa na Katiba sahihi. Nje ya hapo ni porojo.
 
Nyerere aliwahi kusema Katiba hii rais anaweza kuitumia kuwa dictator. Naona magufuli kaamua kuitumia hivyo
Wakati mwingine udikteta una make sense. Barabara ya Moroko-Mwenge hivi sasa iko poa baada ya Magu kuamua tu.
Asingeamua, bilioni 2 zilizokuwa zimetengwa hivi sasa zingekuwa chooni.
 
Sasa kama Zanzibar inachangia kwenye mfuko wa pamoja wa Muungano,tena inachangia zaidi kuliko hako kaasilimia 3 anakopewaga..
inakuwaje hela zinazohusu Muungano ziishie bara,kama yalivyoishia mabilioni ya Zanzibar yaliyokuwepo kwenye bank ya East Afrika,yaliyoishia huko BOTanganyika na hela nyengine kutoka FIFA,UN n.k. eti hata foreign exchange,utalii,ushuru wa bandari ya zanzibar,makusanyo yote kuishia bara..
zamani wabara walienda zanzibar kuchukua vitu..
mtanganyika kaenda mbali zaidi kwa kuigomea zanzibar isijiunge na OIC ili ikose mikopo isio riba na bidhaa muhimu kama matrekta..
Mtanganyika tunaelewa kwa nini unalilia Muungano..
mkuu nakuona ulivyoandika kwa hisia kali. pole sana.
 
Kama huko nyuma kulitokea makosa na wabunge hawakuhoji matumizi ya fedha haina maana hawana haki ya kuhoji maamuzi ya rais hivi sasa. Mimi namsifu rais Magufuli kwa kazi anayoifanya mpaka sasa lakini haina maana asifuate sheria kwenye maamuzi yake. Sina uhakika kama amevunja sheria au la, lakini nategemea yeye kama rais atakuwa na wataalam wa kumshauri kisheria.

Rais wa Tz havunji sheria.
 
Wakati mwingine udikteta una make sense. Barabara ya Moroko-Mwenge hivi sasa iko poa baada ya Magu kuamua tu.
Asingeamua, bilioni 2 zilizokuwa zimetengwa hivi sasa zingekuwa chooni.
jiulize baada ya rais kuamua barabara ijengwe, tender iliitishwa lini, analysis ilifanyika lini, je sheria ya manunuzi ya uma ilizingatiwa na je hakuna ufisadi hapo?
 
Hao wabunge hawana jipya kabisa. Kwa miaka yote ni lini bajeti imeheshimiwa? Mara zote wanaruhusu pesa inatumiwa kwenye vifungu vya hovyo. Miaka iliyopita bajeti ilichotwa kwa ajili ya safari na hakuna mbunge aliyerefusha mdomo.
Kwa sasa pesa inapelekwa kwenye matumizi ya maana wao wanahoji. Hiyo pesa ingeongezea posho zao wangeuliza?

Waambie
 
Nafikiri nilishakujibu swali lako: "kama huko nyuma kulitokea makosa na wabunge hawakuhoji matumizi ya fedha haina maana hawana haki ya kuhoji maamuzi ya rais hivi sasa...". Pia nimeelezea kufurahishwa na utendaji wa rais (MPAKA SASA), lakini haimaanishi rais awe juu ya sheria. Pili, kama hatafuata sheria yeye mwenyewe ataifanya kazi yake kuwa ngumu zaidi. Kama rais anataka watu wawe na nidhamu makazini kwamfano, kufuata kanuni za kazi au kotopokea rushwa basi yapaswa hata na yeye pia azingatie utawala wa sheria. Anatakiwa aongoze kwa mfano. Ukiwaambia watu wafuate kanuni halafu wewe ukawa unazipindisha inakuwa vigumu kuwashawishi watu ndio maana nikaandika kuwa anaweza kuifanya kazi yake kuwa ngumu.
Naamini unaelewa utaratibu wa utawala ktk nchi hii. Naamini hujawahi kusikia taarifa yoyote ya ukaguzi wa mahesabu ya fedha za ikulu. Hakuna audit report ya ikulu, inayosomwa kwa wabunge. Huo ni mtindo wa miaka yote na hakuna legal body inayohoji matumizi ya rais. Hiyo ndo njia ambayo kigurunyembe aliitumia kudhalilisha taifa hili.

Leo hii tumepata mtu anayezitumia kwa mambo ya maana tena kwa kutangaza, wabunge wanajidai kuhoji. Jiulize kuna sababu gani. Komesha ya mambo yote haya ilikuwa ni katiba kuweka ukomo wa madaraka kwa kila mtu. Ni hao hao wabunge walio panua midomo na wengine kunengua bungeni wakishangilia ujinga. Naomba tusiwaruhusu kuwa na akili wanapoona pesa inatumiwa vizuri na wanakuwa hovyo wanapoona posho zao zikiongezwa nje ya bajeti.

Leo si umeona bilioni zikirudishwa kwa rais toka ofisi ya bunge? Lini uliwahi kusikia bunge likisaza pesa? Miaka yote hiyo, hizo bilioni zilienda wapi? They are senseless!
 
Baadhi ya Wabunge wamehoji uhalali wa kisheria wa Rais John Magufuli kuhamisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe ya Muungano na kuzipeleka kwenye ujenzi wa barabara katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Wabunge hao walihoji hilo wakati wa semina iliyofanyika jana katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini hapa Dar es Salaam, iliyoendeshwa na Dk Haji Semboja kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Harold Sungusia wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali alihoji juu ya mamlaka ya Rais katika kutumia fedha ambazo zilishapangiwa bajeti na Bunge na kuzipeleka kwenye maeneo mengine.

Alihoji pia juu ya nidhamu ya Serikali katika usimamizi wa Bajeti iliyopitishwa na Bunge.

Mbunge huyo alisema dhana ya mgawanyo wa madaraka haipo kwa sababu Serikali ina nguvu kuliko Bunge na Mahakama hivi sasa.

Alisisitiza kuwa nguvu hiyo ndiyo inayomfanya Rais afanye kitu chochote anachotaka.

Mbunge wa Viti Maalumu, Lucia Mlowe alisema moja ya majukumu ya Bunge ni kuisimamia Serikali, lakini anashangaa kuona yenyewe ikilisimamia Bunge katika mambo mbalimbali.

Alisema hata suala la Rais kuhamisha fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe ya Muungano, ni kuingilia madaraka ya Bunge, kwa sababu fedha hizo tayari zilikuwa zimeidhinishwa kwa ajili ya matumizi hayo.

“Naomba kupata ufafanuzi kutoka kwa wataalamu hapa, Rais ana mamlaka gani ya kuhamisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya jambo fulani? Pia, ni namna gani wabunge tunaweza kuisimamia Serikali kama hamna uwiano kati ya mihimili hii mitatu,” alihoji mbunge huyo.

Akijibu hoja hizo, Dk Semboja alisema Sheria ya Bajeti ya 2015, inampa mamlaka Rais kupeleka fedha katika eneo analoona inafaa.

Alisema sheria hiyo inatoa sharti moja, kwamba Rais kupitia Waziri wa Fedha, atatoa taarifa bungeni juu ya matumizi ya fedha hizo.

Dk Semboja alisema mamlaka hayo yanatambuliwa pia katika Ibara ya 137 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, hivyo Rais hajakosea kuhamisha fedha hizo kwenda kujenga barabara isipokuwa taarifa ya matumizi itolewe bungeni hata kama matumizi yanaonekana.

“Bunge lazima lifahamishwe kuhusu matumizi ya fedha hizo. Kama ni udhaifu wa kipengele hiki, basi unaanzia kwenye Katiba,” alisema Dk Semboja.

Pia, Sungusia alisema, “Fedha ambazo Rais hawezi kuziingilia ni zile zilizo kwenye consolidated fund (mfuko hodhi), nje ya hapo anaweza kufanya lolote,” alisema mwanasheria huyo.

Source: Mwananchi
Wale jamaa wa maigizo na live tv wameanza tena. Iliobaki ni kuwapuuza iko siku watajiona wamekuwa wapuuzi mbele ya jamii
 
Back
Top Bottom