Wabunge wahoji fedha za Rambirambi Arusha kutumika kwenye matumizi ya serikali

Makosa yalifanyika 2015!wabunge wengine hawakupaswa kuchaguliwa/kuteuliwa kuingia bungeni!siamini kama wananchi jimboni kwake walimtuma kutoa hoja za kitoto kama hizi! !
Mimi ni mmoja kati ya waliompigia kura waitara.

Kuhusu rambi rambi, nakataa kutumika kwenye shughuri za maendeleo ya badala ya kuwafikia walengwa. Huo ni urafi na unyang'anyi.

Hivi inakuingia akilini kweli rambi rambi ikajenge monchwari?

Hapana jamani
 
Ndio zishaliwa sasa? Kwani nyinyi mnasemaje? Tushakula amueni mnachoamua? Wewe unafikiri yale magari yalikua yanatumia maji? Na ulitaka tukae njaa msibani? Acheni ujinga CHADEMA, zile hata nyinyi mngekula, kwanza kitendo cha nyinyi kufika pale msibani tu ni kwamba na nyinyi mlikula, maana kama uwanja na nyinyi mlichafua hela ya usafi ulitaka tutoe mifukoni mwetu? Acheni uzuzu!!
Mimi ninayepinga kuhusu rambi rambi kuliwa sio chadema.

Usiaminishe watu kuwa ccm hawana roho ya utu kwa kushabikia rambi rambi kuporwa.

Hiyo ni roho yako binafsi wala haina chama
 
Makosa yalifanyika 2015!wabunge wengine hawakupaswa kuchaguliwa/kuteuliwa kuingia bungeni!siamini kama wananchi jimboni kwake walimtuma kutoa hoja za kitoto kama hizi! !
Hoja ya kikubwa kwako ni serikali kutegemea rambirambi kama chanzo chake cha mapato?
 
Mfuko wa Maaafa? Kwanini tuchukue hela ya maafa wakati nyinyi mshachanga wenyewe? Huu mfuko wa maafa uache kwanza, hatuwezi kupeleka pesa za mfuko wa maafa Arusha hata siku moja, afe mtu afe mmasai... Ingekua dodoma sawa, tungepeleka, nyinyi Arusha bakini na ujuaji wenu..

Kwa hyo issue n kwa sababu msiba umetokea Arusha?

Kwa hyo nia yenu n kuwakomesha majimbo yanaongozwa na Upinzan kama ilivyo Bukoba??????
 
Makosa yalifanyika 2015!wabunge wengine hawakupaswa kuchaguliwa/kuteuliwa kuingia bungeni!siamini kama wananchi jimboni kwake walimtuma kutoa hoja za kitoto kama hizi! !
Mkuu, ni bora ungekaa kimya ili kuficha upumbavu wako.

Kumbuka anahoji KWA SABABU ALICHANGA. Na waliokufa ni watanzania wenzake. Wewe ulichanga au ulikaa tu kwenye screen nyumba ya jirani kuangalia maombolezo...!! Acha ufala sometyms
 
Mimi ninayepinga kuhusu rambi rambi kuliwa sio chadema.

Usiaminishe watu kuwa ccm hawana roho ya utu kwa kushabikia rambi rambi kuporwa.

Hiyo ni roho yako binafsi wala haina chama
Yaani mtu atoke alikota, akanunua smartphone/computer kwa gharama zake, sijui nani akamfanya aijue JF, akakutanana comment yangu halafu niwe nimemuaminisha mimi, ? Kama hivyo ndivyo mbona na wewe unataka kutuaminisha kua CCM hatujala rambirambi? Kwanini na mimi nisiseme kwamba hayo ni maoni yako binafsi wewe Mkuu ila sisi kama CCM rambirambi tumezila na tutazila sana as long as polisi wapo kutusaidia.
 
Kuna wengine wanayafurahia mambo haya hasa washabiki na wapenzi wa watawala.Hiyo pesa itawatokea puani swala ni wakati tu.Watu wameumia kwa kupteza vitu,kufiwa na wengine kujeruhiwa,halafu wewe unaleta maneno ya dhihaka na kejeli,bado unahamasisha watu kutoa pesa kwa lengo la kuwafariji wahusika halafu unazitumia unavyopenda eti kwa mamlaka uliyonayo,ni sawa na kula hella za yatima,wajane,walemavu na wazee wasiojiweza,Haponi mtu hapo Mungu hadhihakiwi swala ni mda tu.
 
Yaani mtu atoke alikota, akanunua smartphone/computer kwa gharama zake, sijui nani akamfanya aijue JF, akakutanana comment yangu halafu niwe nimemuaminisha mimi, ? Kama hivyo ndivyo mbona na wewe unataka kutuaminisha kua CCM hatujala rambirambi? Kwanini na mimi nisiseme kwamba hayo ni maoni yako binafsi wewe Mkuu ila sisi kama CCM rambirambi tumezila na tutazila sana as long as polisi wapo kutusaidia.

Nimekusoma
 
Wapigaji wa hela ndio walalamikaji.
Inanikumbusha zamani wakati wa kupanda bus pale stand panakuwepo wezi waliojulikana "vidole viwili" ili wawaibie abiria walikuwa wanaanza kupiga kelele, "mnaibiwa" ukijikagua wanajua kumbe unazo, watakufuatilia mpaka wakuibie. Sasa hawa wa sasa wanataka kutuaminisha kuwa utaratibu wa Ma RC kusimamia rambirambi za maafa ya kitaifa unawapa ulaji, kumbe hao hao wapiga kelele ndio hatari zaidi. Kelele hizi ni tamaa na uchoyo uliomo ndani. Rambirambi kwa utamaduni wetu huwa hazifuatwi fwatwi, ukiona mtu anafuatilia hizo ana ajenda yake na mara nyingi ni mbaya. Rambirambi hazina kanuni na matumizi yake nayo ni dharura na huwezi kuyahoji kwa nini walitumia hivi? na hasa mfiwa! Ikitokea atakuwa ni mvuta bangi au ana pepo mchafu. Na jamii yote humwogopa. Tabia wanayoanza kutuonyesha ndugu zetu wa Kagera na Arusha inaanza kunipa wasiwasi kama ajenda gani wanayo mpya ya viongozi wetu! Isipodhibitiwa itatutengenezea Taifa la wahuni na tutakuwa tukiwapa uongozi watatuloga. Mtumishi wa Mungu Musa hawakuweza kufika Kaanani kwa kuwa walikuwa wameharibika na kuwa walalamikaji na wanung'unikaji tu. Mungu akawafutilia mbali. Unapiga kelele kwa hela ambayo haina risiti inashikwa na wengi na maamuzi yake ni ya haraka haraka mpaka mnamtukana baba wa watu, amehangaika usiku na mchana, halali, akizuia walaji wa rambirambi. Badala ya kumtia moyo wakati huu wa majonzi. Ni ushetani kabisa!.
 
Tena ushetani Mkubwa sana Mkuu, rambirambi ni haki yetu sisi CCM tu, Chadema watu wa ajabu sana, jiji tumewaachia, wanapiga hela ya kutosha bado wanataka mpaka hizi hela ndogo za wanyonge, dah.. Hawana huruma kabisa, tena tumewasaidia hata kukarabati hosptal iliyopo ndani ya jiji lao.
 
Tatizo watanzania hajujifunzi. Siku nyingine ni vema usimamizi wa rambirambi uwe mikononi mwa waathirika wenyewe aau familia yenyewe. Huu mtindo wa viongozi wa serikali kuwa ndio washika hazina kwenye misiba ni mbaya. Serikali kama ina mchango wowote iuwasilishe kwa wafiwa. Sasa ona tumeshapigwa marufuku kwenda kuwafariji wafiwa majumbani mwao, eti tunalazimishwa twende kumfariji Gambo. Hii ni laana siyo bure. 2020 sitajaali nani kapiga push up jukwaani.
 
Tatizo watanzania hatujifunzi. Siku nyingine ni vema usimamizi wa rambirambi uwe mikononi mwa waathirika wenyewe aau familia yenyewe. Huu mtindo wa viongozi wa serikali kuwa ndio washika hazina kwenye misiba ni mbaya. Serikali kama ina mchango wowote iuwasilishe kwa wafiwa. Sasa ona tumeshapigwa marufuku kwenda kuwafariji wafiwa majumbani mwao, eti tunalazimishwa twende kumfariji Gambo. Hii ni laana siyo bure. 2020 sitajaali nani kapiga push up jukwaani.
 
Back
Top Bottom