usatrumpjr
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 2,237
- 2,898
Kwl hawa wabunge wapo madarakani miaka 50+ nchi bado iko vile vile tu
Elimu elimu elimu asante lowasa
Elimu elimu elimu asante lowasa
Hili ni jambo la kusikitisha sana na sio la kulichekea hata kidogo.
Kama Taifa tunaukilema wa kuwa na upinzani usio na malengo ya kulikuza Taifa kupitia changamoto zao za wazi na chanya kwa serikali yetu.
Napenda kusema kwamba Upinzani tulionao ni ule ambao wahusika wapo kwaajili ya maslahi binafsi na sio kwa ajili ya wale walio wachagua.
Maslahi ambayo wanayapigania sana wabunge wa upinzani ni pamoja na umaarufu wao , gusa jambo jingine lakini usiguse jambo ambalo litaathiri umaarufu wake moja kwa moja.
Hali hii imekua mbaya sana kiasi kwamba imehamia mpaka kwenye matukio yenye nature ya huzuni. Mfano mzuri hivi karibuni Mbunge wa Arusha mjini alipotoashutuma za wazi wazi kisa tu hakupewa nafasi ya kuonekana mbele ya watu wa Arusha. Kumbuka ule ulikuwa msiba wa kitaifa lakini wenzetu wao walikuwa wanataka kuonekana tu.
Tabia hii ya kupenda kuonekana tu na kupalilia umaarufu wao ilianza taratibu pale Bunge live lilipopigwa pini kutokana na mzigo wa gharama uliokuwepo, lengo jema la kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima na kuyapeleka kule kunakostahili, iligeuzwa na kuwa kosa kubwa kwani ile nafasi ya kuonekana ilikuwa haipo tena.
Marufuku ya Siasa za majukwaani zisizo na mpango nayo ukawa mwiba mwingine kwa wabunge wa Upinzani, kwani waliozea kuzunguka nchi nzima na kupoteza muda wa nguvu kazi za Taifa, at the expense ya kupalilia umaarufu wao.
Jambo hili ni baya sana kwa demokrasia ya nchi na maendeleo kama Taifa kwani tuna watu wanaotaka kuonekana na kupata umaarufu badala ya kuangalia hali za hao waliowapa nafasi za umaarufu.
Wabunge wa upinzani inabidi mbadilike bila hivyo mtazidi kupukutisha majimbo yenu 2020, kwani wananchi wanaendelea kuwachoka kwa ahadi zenu hewa ambazo hazionekani na badala yake nyie tu ndio mnaoendelea kuwa maarufu kupitia mogongo yao na kura zao.
Nakuunga mkono hakuna si tu jipya ila ndio pumba sanaNimejitahidi kutafuta hoja yenye mashiko katika andiko lako nichogundua ni UJINGA MTUPU
Unazidi kujipambanuani kawaida kwa mjinga kuona ujinga; haiwezekani mjinga akaona ujanja popote. bila shaka wewe ni mjinga. na hapa umethibitisha ujinga wako.
Katikati ya huzuni za watu, mtu analilia kuuza sura. Very sad indeed. Yaani hajua hata presence tu kwenye eneo la tukio ni ishara tosha ya kuguswa na msiba?wapenda kiki
Hayo hawezi fanya mkuu, alikuwa busy kumtukana Spika..ili apate kiki..Sisi wa BunjuB tunaye Mheshimwa @halimamdee tumemlalamikia kinoma kuhusu wachuuzi kukimbia soko jipya na kurudi barabarani kuendeleza kuweka uchafu, magenge na fujo, wapi! Tumemlalamikia soko jipya halina matundu ya choo ya kutosha, kimya! Tumelalamika soko jipya halina umeme, na maji liko bomba moja, halitoshelezi, kimya! Tumelalamika kuna ufisadi soko jipya bunjub hasa katika ujenzi wake, kimya! Kukicha anaishia kutukanana na Spika wetu wa bunge?! Wapi na wapi..Twakubaliana nawe, wao KIKI zaidi kuliko kusaidia jamii...