Vijana wa CCM nani aliyewaroga?? Sasa ndo mada gani hizi mnaleta hapa JF!!Mbunge yoyote ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Anaweza akawa Mbunge kwa kuteuliwa ,Viti maalum au kupitia Jimbo.
Sasa kwa hoja yako ulitaka wabunge wa kuteuliwa ndio wazungumzie mijadala ya kitaifa kwa sababu hawana majimbo au??
Kama ingekuwa hivyo vipi kuhusu kutunga sheria ambayo ndiyo kazi ya msingi ya Bunge? Kaa ukijua sheria hizo zinahusu Tanzania bara yote bila kujali jimbo na wakati mwingine zinahusu Tanzania nzima.
Vipi kuhusu kazi ya kuisimamia Serikali? Unataka wabunge waisimamie serikali kwenye mambo yahusuyo majimbo yao tu?
Sio lazima uanzhishe uzi kama huna jambo la maana.