Tatizo ni kwamba hawatoshi.Toka upinzani umeanza nchini wabunge wa upinzani wamekuwa wakijijengea umaarufu katika mambo ya kitaifa na sio ya kijimbo kama eneo lao la kazi.
Leo ikisisikika njaa wote wanaweka kambi, mafuriko au janga wote wanaweka kambi. Ninavyofahamu chama cha siasa kinaviongozi wa kitaifa kwa ajili ya mambo ya kitaifa. Kuzungumzia mambo ya kitaifa sio dhambi lakini ni heshima iliyotukuka kwa mbunge kuwa maarufu kwa kile alichokitenda jimboni zaidi.
Mtazamo huu unalengo la kukosoa kwa kujenga kwa maana kama kila mbunge akiwekeza katika mafanikio ya jimbo basi taifa litakuwa kwa kasi huku wale wa kitaifa wakishughulika na mambo ya kitaifa.