Wabunge ni wanafiki, mbona hakuna aliyejitokeza kupeleka hoja binafsi Bungeni kupunguza posho zao

Enyi kizazi cha Nyoka CHADEMA walipokuja na sera ya kukataa sitting allowance 2010 Ndani ya Bunge hamkuwaunga mkono. Mungu anavyozidi kuwaumbua hadharani kwenye Bunge la Katiba wakasusuia zile posho na vikao matokeo yake CCM wakanywea pombe. Ndio raha yenu UKAWA wasusue ccm mkanywee pombe. Wacha waendelee kuzichukua zikawasaidie watanzania kwenye majimbo yao
 
Bora hizo posho mpaka pesa chafu za madili ukikuta wanavozifukuzia kwny kamati huwezi kutofautisha vyama vyao.
PAC na LAAC niliwahi kuelezwa Rafiki yangu mmoja kuwa alishuhudia 'Rais wa Mioyo ya Watanzania 2010-2015' akiwa Chairman wa LAAC akipewa Mlungula wa Mill 27 kupitia kwa dereva wake azime jaribio la Madiwani kuwaazimia Mkurugenzi na wakuu wa Idara. Nae baada ya kunywa mifuko mitatu hiyo ya Khaki akaagiza kuwaunga Mkono madiwani kwa Kuwakata Wakurugenzi 15% ya Mishahara ili kuwazuga madiwani!!!. Walipotibuana kwny kuwania madaraka hv karibuni ndo nikaanza kuafiki niliyoelezwa.
Leo hii naaminima kama yule Mzee alikuwa mpigaji simuamini mtu yoyote.
Tanzania nzima hakuna mwanasiasa msafi hata mmoja aliekwenda kupigiwa kura halafu akashinda akatudanganya kuwa hakushiriki michezo michafu ya kuhakikisha ushindi wake.
Wanatofautiana rafu,uchafu na Ujanja wa kuficha ushahidi.
Nadhani unalikumbuka lile ghorofa lililoanguka maeneo ya Chang'ombe halafu mzee mwenye mvi nyingi akaenda moja kwa moja kwenye tukio. Habari nyeti zinadai kuwa ile kesi imepotea mpaka leo kwani fedha zilikutana na mtu anayeifahamu vizuri harufu yake nzuri.
 
Sijui unafanya kazi gani kama umeajiriwa nenda kamuombe bosi wako apunguze mshahara wako ili uwe mfano wa kuigwa, pili kama mfanyabiashara wapunguzie wateja wako bei zaidi ya ile unayonunulia bidhaa ili tuende sawa! Ninacho jaribu kusema ni kuwa fanya kazi kwa bidii upate stahiki zako acha kuwa na roho ya kwa nini mbunge anapata posho. Hao raia maskini wanatakiwa kusaidiwa na serikali yao lakini zaidi wanatakiwa kujisaidia wao wenyewe.Serikali itemgeneze sera na mipango madhubuti ya kuboresha kipato na maisha yao na mbunge kazi yake iwe ya kiusimamia serikali ifanye vyema na sio kumsaidia kwa kutoa au kukataa kipato anachofanya kazi hata mbunge ni raia anataka kuishi maisha bora asomeshe watoto nk,usimchukulie kama ni mtu tofauti na wewe au allien.Ukishindwa hayo kuwa Mbunge. Get a life!
 
Hata ungekuwa wewe usingefanya hayo mkuu. Upunguziwe posho? Politics zetu ni kwa masilahi binafsi.
 
Eti kama wewe ungeweza?, unamtegemea mwanasiasa awe ndie rafiki yako kipenzi mda wote, nitakushangaa sana, wacha hiyo fikra, HAPA KAZI kwa maisha yake, naw kuwa na YAKO KAZI iwe kwa maisha yako ndugu, maisha ya nikipata nawe utapata yaliisha zamani sna.
 
Hata ungekuwa wewe usingefanya hayo mkuu. Upunguziwe posho? Politics zetu ni kwa masilahi binafsi.

Uko sahihi. Tatizo kuna watu wakianza kusifia 'Uzalendo na uadilifu' wa wanasiasa wao mpaka mishipa ya kichwa unawasimama na wanawaamini kuliko mtu yoyote.
Mkurugenzi mkuu wa Zamani wa Usalama wa Taifa Dr.Hassy Kitine kwa Masikio na macho yangu nimemsikia akisema kwenye Msiba wa Hayati Balozi Daud Mwakawago kuwa tangu uhuru kakutana na wanasiasa safi watatu tu (kwny Rushwa na Upigaji) tena kaongea mbele ya Mwinyi,Mkapa,Jk n.k
1)Mwl Nyerere
2) Balozi Mwakawago
3) Comrade Ibrahim Kaduma (yupo hai)
Yeye mwenyewe Hassy hakujitaja. Kama wakati wa Mwalimu kwenyewe kulikuwa na wapigaji mpaka kuhifadhi mapesa Uswiz kwa mujibu wa Report za World Bank (1972 ndo ufichaji fedha nje ulianza hapa nchini) itakuwa hiki kizazi cha Firauni
 
Mbunge Halisi pekee tutakae mkumbuka mpaka uzee wetu ni Dr. Wilbroad Peter Slaa. Sitaki kumuelezea sana wengi munamkumbuka wakati ni bunge.
 
kwenye suala la pesa wanasiasa wote sawa. hata john maghufuli hawezi thubutu kupunguza mshahara wake kamwe ili kusaidia wanyonge. pamoja na mbwembwe zake zake zooote. chezea hela www....
 
Enyi kizazi cha Nyoka CHADEMA walipokuja na sera ya kukataa sitting allowance 2010 Ndani ya Bunge hamkuwaunga mkono. Mungu anavyozidi kuwaumbua hadharani kwenye Bunge la Katiba wakasusuia zile posho na vikao matokeo yake CCM wakanywea pombe. Ndio raha yenu UKAWA wasusue ccm mkanywee pombe. Wacha waendelee kuzichukua zikawasaidie watanzania kwenye majimbo yao
Akufanyie kazi na posho aifute? We mwehu kweli
 
Back
Top Bottom