Wabongo tupunguze kuweka mafaida makubwa katika bidhaa tunazouza

Poker

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
5,563
15,267
Jana kuna sehemu nimeenda, nikakuta ndala zile kandambili za 2000 zinauzwa 5000, kuuliza haipungui nkaambiwa haipungui alafu muuzaji akaendelea kujisnap.

Kuna maduka ukienda, bidhaa ambayo kariakoo kwa mchina unaipata labda kwa 5000 huko unaikuta 10,000 haswa maduka ya sinza.

Unaenda lodge, chumba 50k hakina maji moto, tv inaonyesha azam 2, vitanda vinatingishika ukiomba punguzo bado mtu anakaza.

Unaenda mgahawani, wali na nyama 2 unauziwa buku 5000. Haitoshi ugali dagaa unauziwa 3000 😳

Hii imeenda mbali zaidi saivi gb 1 unaipata kwa 2100 na huna cha kufanya.

Huu ujio wa wachina unaweza tusaidia kidogo maana kila kitu saivi kinapanda bei kiholela tu si kodi, si mpunga, si utelezi n.k

Tupe nawewe ushuhuda wako wa namna wabongo wanavyopandisha vitu bei kiholela mpaka unaona kabisa hapa napigwaa!
 
Na hizi stori za mitandaoni kila mtu amataka kitusua maisha ni balaa.

Stori za Madalali
Dalali 1: Juma amepiga hela san, Baba ́Mwenye nyumba kataka milioni 50, aisee Juma si akapata mteja wa mil 110? Juma kapiga milioni 60 cha juu.

Dalali 2: Mjini mipango akija fala unapiga tu, ile prado naifanyia mpango Sitakosa hata 10M hivi.

Mambo yako hivyo kwenye biashara zote.

Mwenye nyumba kasema anapangisha kwa laki 2, Dalali Juma anakupiga laki tatu 50.

Mtu kanunua Kuku elfu 7, anakupiga elfu 18😅😅😅
 
Mjini shule mkuu ukiwa unateseka na vyakusikia na kuona utaishi maisha ya shida sana.
 
Hata kwenye maji ya kunywa hivo hivo. Jumla lita moja na nusu ni 550 ila ukienda dukani unauziwa 1000 rejareja.

Ni kama watu wanataka kutajirika fasta fasta, ndo inafanya biashara nyingi zinakufa maana mimi huwaga sinunui
 
Wanasema tz🇹🇿 ni soko huria,,,,! Uza na nunua kadri unavyoona, kuna jeans k/koo ni 18, lakn ile ile jeans ukienda kino ama sinza kwenye duka lenye Ac utainunua kwa 45k,,,, ! Na same to super markets na maduka ya mangi,, utofauti wa bei ni mbingu na ardhi!! Serikali naona imelibariki hili,,,, zile bidhaa basics zikipanda bei hovyo ndo watapiga kelele na vitisho mfano sukari, unga, mchele, mafuta , petrol/diesel nk
 
Kwenye real estate ndiyo kumevamiwa kabisa. Hivi mtumishi wa umma anaweza kweli kujenga Dar? Maana kiwanja tu cha kawaida sana ni zaidi ya 10m. Hata vya serikali bado bei haishikiki.
 
Back
Top Bottom