Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,745
- 40,882
Ndiyo tunaelekea Airport.. Mhe. keshatua... kwa hiyo shughuli itaanza baadaye kidogo...
Tunawashukuru watu wote waliojitokeza kwenye shughuli yetu fupi. Mambo yalienda more than expected ilikuwa ni kama "meet and greet" session lakini pia ilifanywa kwa mtindo wa kubadilishana mawazo.
Mhe. Zitto katumegea mambo mengi mazito na yenye hamu kubwa hasa kwa wale ambao wanasubiri kwa hamu ile ripoti ya madini. Lakini alizungumzia mambo mengi sana kutoka masuala ya kiuchumi na kisiasa. Na alitoa kauli kadhaa nzito ambazo natumaini mtazisoma kwenye magazeti ya nyumbani siku chache zijazo.
Tafrija yetu ilimalizika kwenye saa tano za usiku na tulimfikisha Mhe. Hotelini kwake umbali wa kama saa moja hivi kwenye majira ya saa sita za usiku.
Tunamshukuru sana kwa kutuheshimu na kutukubalia mwaliko wetu. Na sisi tulimuonesha shukrani ya watanzania Michigan na ni matumaini kuwa tumeweka alama ya kukumbukwa moyoni mwake.
M.M.
Mi nangoja picha, au soo?
Duh, shikaji langu Abdoul Kufakunoga kanyoa Mohawk ama macho yangu?..
Ab Titchaz,
hapana mkuu nilianza kushangaa manake hizi style za Arsenal na UK zimeingia mjini..nakuona kwa nyuma umejificha....haaa haaa haaa!
Nisalimie...
Mwanakijiji mwenye glasses hapo mbele kama sijakosea!
Mwafrika wa Kike yukwapi?