Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,887
- 119,754
Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huja na kwa maslahi ya taifa.
Maslahi ya leo ni hii issue ya SMZ kumiliki eneo la ekari 6000 Bagamoyo. Tangazo la SMZ Zanzibar: Hekta 6,000 zilizopo Bagamoyo ni mali yetu
limeleta taharuki na sintofahamu kubwa kwenye mitandao ya kijamii hadi baadhi ya watu kutoa povu!.
Kuna watu wanatafsiri potofu kuwa sehemu ya Ardhi ya Tanzania Bara ni sehemu ya Zanzibar!.
Ukweli ni huu
Anza na bandiko hili la mwaka 2014 iujue historia ya eneo hilo lilimilikiwa vipi na Zanzibar Zanzibar ndani ya Tanganyika ilianzia huku kisha soma majadiliano ya Bunge ya miaka ya nyuma kuhusu issue hii.
Shamba la Mifugo Linalomilikiwa na SMZ huko Bagamoyo
MHE. MOSSY SULEIMANI MUSSA aliuliza:-
Kwa kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliwahi kuwa na shamba kubwa la mifugo (ng’ombe) ranchi huko Bagamoyo:-
(a) Je, Serikali ya SMZ bado inamiliki shamba hilo? (b) Je, hadi kufikia kuboreshwa kwa shamba hilo SMZ ilitumia shilingi ngapi?
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na uvuvi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mossy Suleimani Mussa Mbunge wa Mfenesini lenye vipengele (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-
(a) Mheshimiwa Spika kwa kuzingatia Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA) iliyoko Makurunge katika Wilaya ya Bagamoyo inamilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ranchi hiyo ilianzishwa mwaka 1976 baada ya kupata kibali kutoka kwa Kamishna wa Ardhi chenye kumbukumbu namba LD/70254/12/TBR cha tarehe 24/09/1971, hivyo kwa taarifa hizo Wizara yangu bado inaamini shamba la RAZABA bado ni mali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hata hivyo kwa vile swali linaloulizwa na Mheshimiwa Mbunge linahusu mali zilizo chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi sio Wizara ya Muungano napenda kumjulisha Mheshimiwa kuwa Wizara yangu haiwajibiki kujua kama Serikali ya Mapinduzi Zanzibar bado inamiliki au haimiliki shamba hilo.
(b) Mheshimiwa Spika, Wizara yangu haijui kama shamba hilo ambalo liko chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lilitumia shilingi ngapi katika kuliboresha, namshauri Mheshimiwa Mbunge akapate majibu ya takwimu hizo Wizara inayohusika katika Serilkai ya Mapinduzi Zanzibar.
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI:
Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri naomba kutoa maelezo ya nyongeza kama ifuatavyo.
Mheshimiwa Spika, shamba hilo ambalo ni kweli kama alivyosema Naibu Waziri lilimilikishwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lakini kwa miaka mingi sana karibu 30 halitumiki, kwa hivi karibuni Serikali imemega sehemu na kuwapa wawekezaji, watawekeza katika mambo ya biofuel na Sehemu bado inaendelea kuwa mali ya SMZ.
My Take
Wakati wa kuumbika nchi, Zanzibar ilikuwa eneo la bara likamegeka kwa sea erosion, hivyo Visiwa vya Zanzibar ni sehemu halali ya Tanzania bara ndio maana dhima ya muungano wetu adhimu ni udugu, sisi ni ndugu moja, Waarabu walipokuja Zanzibar ile 1732 Sultan Seyyid Said alipohamoshia Sultanet take toka Oman kuja Zanzibar, aliwakuta wenyeji halisi ni Wahadimu, kutoka Bara, alivitwaa visiwa hivyo toka ukoo wa Mwinyimkuu, na waliompindua Sultan kwenye yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni wajukuu wa Mwinyimkuu wenye Zanzibar yao, ndio maana slogan ya Mapinduzi Daima ipo, na baada ya muungano tumekuwa kitu kimoja, ndio maana slogan ya muungano ni tutaulinda kwa gharama yoyote.
Miongoni mwa gharama hizo ni kumsamehe madeni, kumpa 4.5% ya fedha za mikopo na misaada, ajira na hata kumpa eneo lolote Wazanzibari watakalotaka.
Watanzania bara tujifunze kuwa na shukrani, tushukuru sana Zanzibar, ukanda wa eneo la maili 10 ya Pwani ya ya bahari ya hindi, lilikuwa eneo la Zanzibar, ikatugawia!, miji yote ya Pwani kuanzia Dar, Tanga, Bagamoyo imejengwa na Sultan of Zanzibar!
Hata mjengo wa Ikulu ya Magogoni, imejengwa na Sultan of Zanzibar, hata ile replica ya Ikulu pale Chamwino ni mjengo wa Kiarabu!, mbona watu mnakosa shukrani kwa mambo mazuri kama haya, mnaona nongwa Zanzibar kumiliki eneo huku Bara!
Mapinduzi Daima
Muungano Tutaulinda kwa gharama yoyote!.
Paskali.

- Wabara ondoeni shaka kuhusu umiliki wa SMZ eneo Bagamoyo, SMZ inalimiliki eneo hilo kihalali kabisa kwa vile walipewa na Mwalimu Nyerere.
- Kitendo cha SMZ kumiliki eneo huku Tanzania bara, hakulifanyi eneo hilo kuwa sehemu ya Zanzibar, ni eneo halali la SMZ ila ardhi ni ya Tanzania bara.
- Nchi yoyote inaweza kumiliki eneo nchi nyingine yoyote, umiliki huo haulifanyi hilo eneo kuwa sio sehemu ya nchi husika.
- Japo SMZ inalimiliki eneo hilo lililokuwa hekta 6,000, kwanza SMZ, haina hati ya umiliki bali ina kibali cha umiliki No. LD/70254/12/TBR cha tarehe 24/09/1971.
- SMZ ililitelekeza eneo hilo kwa miaka 45, hivyo serikali ikalimega kumpa mwekezaji, Halmashauri ya Bagamoyo imelipima viwanja inaviuza.
- Kwa vile ni eneo halali la SMZ, na sasa SMZ imeibuka kuonyesha ina interest na eneo lake, then itarudi serikalini kuelezea hiyo interest, serikali itakwenda kulipima limebakia kiasi gani, SMZ itapimiwa upya na kugawa.
- Iwapo SMZ bado italihitaji eneo lote la awali la ekari 6,000, then italazimika kuwalipa fidia watu wote waliomegewa kihalali.
- Kama pia limevamiwa na wananchi, then sheria yetu ya Ardhi ya Vijiji No. 5 ya mwaka 1999 will apply kwa mtu aliyetelekeza eneo lake kwa miaka 45, wale wavamizi wana haki fulani.
- Ikionekana madhara ya kuwaondoa wavamizi ni makubwa kuliko kuirejeshea SMZ eneo hilo, then kile kibali cha umiliki wa SMZ kinafutwa, wananchi wanapimiwa, na SMZ wanapewa eneo jingine, tuna mapori kibao ya kumwaga, hata wakitaka heka 10,000 wanapewa.
- Hii ya kuwagaiya wavamizi imefanyika sana kwenye maeneo ya jeshi na maeneo ya RTD, wavamizi wamepimiwa na kuhalalishiwa!.