Sami Omary Khamis
Member
- Sep 8, 2020
- 67
- 133
NA MWANDISHI WETU
JUMUIYA ya Watendaji Wakuu Vijana (The Young CEO Forum) wamemtaka Mgombea wa nafasi ya Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, kuacha mara moja upotoshaji kuhusu kupandishwa mishahara ya wafanyakazi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Habib Mchange, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ador Tanzania Limited alisema Lissu pamoja na kuwa ni mwanasheria lakini anapotosha kwa makusudi mambo ambayo yako wazi.
“Serikali ya Awamu ya Tano tangu iingie madarakani mwezi Novemba, 2015 imekuwa ikichukua hatua mbalimbali zinazolenga kuboresha maslahi ya watumishi wa umma na Sekta Binafsi, baadhi ya watu kwa maslahi yao binafsi wamekuwa wakiupotosha umma.
Alisema hatua zilizochukuliwa na Serikali ni pamoja na kulipa mishahara ya watumishi kwa wakati, kulipa malimbikizo ya mishahara, kupandisha kiwango cha mshahara kisichotozwa kodi na kupandisha madaraja/vyeo watumishi wenye stahili hiyo, kulipa nyongeza ya mwaka (Annual increment) ambayo kwa muda mrefu ilikuwa haijalipwa na kutoa ajira mpya kwa vijana waliomaliza vyuo mbalimbali.
ONGEZEKO LA MISHAHARA KWA KUPANDISHA KIWANGO AMBACHO HAKITOZWI KODI YAPATO LA MSHAHARA KWA WAFANYAKAZI WA UMMA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SEKTA BINAFSI KWA TAZANIA BARA
Mchange alisema sambamba na watumishi wa umma kupandishwa vyeo, kulipa malimbikizo ya madai ya watumishi yaliyorithiwa kutoka awamu ya nne, kutoa nyongeza za mishahara na kuajiri maelfu ya vijana waliohitimu vyuo; Serikali ya awamu ya tano imepandisha kiwango cha pato la mshahara usiotozwa kodi. Hatua hiyo imeongeza pato halisi la mshahara kwa wastani wa Sh. 100,000 kwa kila mfanyakazi wa Serikali na Sekta Binafsi na hivyo kufanya pato hilo kuongezeka kwa jumla ya Trilioni 6.207 kwa mwaka kama ifuatavyo:-
i. Ongezeko kwa wafanyakazi wa Sekta Binafsi ni Trilioni 3.538; na
ii. Ongezeko kwa wafanyakazi wa Serikali ni Trilioni 2.669.
Ongezeko hilo limeanza Julai 2020.
MALIPO YA MALIMBIKIZO YA MSHAHARA
Akifafanua kuhusu malimbikizo ya mishahara Mchange amesema Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha Mwezi Novemba 2015 hadi Agosti 2020 imelipa malimbikizo ya mishahara kwa watumishi wake yenye jumla ya Shilingi bilioni 137.1 kwa watumishi 76,332.
Amesema kati ya kiasi hicho, Shilingi bilioni 45.5 zililipwa kwa watumishi walimu 41,385 na Shilingi bilioni 91.6 zililipwa kwa watumishi wasio walimu 34,947. Ulipaji wa kiwango hicho kikubwa cha malimbikizo ya mishahara kimefikiwa kufuatia juhudi za Serikali kufanikiwa baada ya kuwabaini na kuwaondoa watumishi hewa katika orodha ya malipo ya mishahara ya Serikali. Baadhi ya waliokuwa watumishi hewa walikuwa wakipokea mishahara zaidi ya mmoja.
KUPANDISHA WATUMISHI VYEO
Aidhaalisema katika kipindi cha kuanzia Novemba, 2015 hadi Agosti, 2020 Serikali ya Awamu ya Tano imewapandisha vyeo watumishi 246,637 na kupelekea kuwapo kwa ongezeko la mishahara la Shilingi bilioni 60.75 kwa mwezi. Kati ya watumishi hao, walimu 161,655 walipandishwa vyeo na kulipwa jumla ya Shilingi bilioni 33.28 nawatumishi wasio walimu 91,982 waliolipwa jumla ya Shilingi bilioni 27.47. Aidha, Serikali itaendelea kuwapandisha vyeo watumishi wake watakaokidhi vigezo kwa mujibu wa taratibu zilizopo.
KULIPA NYONGEZA YA MWAKA YA MSHAHARA (ANNUAL INCREMENT)
Alifafanua kuwa baada ya zoezi la kuhakiki watumishi na kuwaondoa wenye vyeti vya kughushi na hewa, mwezi Novemba, 2017 serikali ilitoa nyongeza ya mwaka ya mshahara (Annual Increment) kwa watumishi wa Umma 505,985 ambapo Shilingi bilioni 72.8 ziliongezeka. Kati ya kiasi hicho Shilingi bilioni 37.2 zililipwa kwa watumishi walimu 270,878 na Shilingi bilioni 35.7 kwa watumishi wasio walimu 235,107.
“Utolewaji wa nyongeza za mishahara ni sehemu ya motisha ambayo hutegemeana na vigezo kama utendaji kazi wa mtumishi baada ya kufanyiwa tathmini ya wazi juu ya utendaji wake na wala si lazima,” alisisitiza Mchange.
AJIRA MPYA
Baada ya Serikali ya Awamu ya ziada za kuzalisha ajira mpya katika Sekta zote na kufanikiwa kuzalisha jumla ya ajira 12,602,526 zimezalishwa. Kati ya ajira hizo, ajira wahitimu wa vyuo mbalimbali 66,178 wameajiriwa na Serikali ambapo jumla ya bilioni 54.9 zimeongezeka kwa kila mwezi ikiwa ni gharama za mishahara kwa ajira mpya.
Ongezeko hilo la ajira katika Sekta binafsi na Umma ni kubwa kuweza kufikiwa na nchi yoyote.
KULIPA MADAI MENGINE YA WATUMISHI YASIYO YA MISHHARA PAMOJA NA MALIPO YA UHAMISHO WA KUHAMIA MAKAO MAKUU YA SERIKALI DODOMA
Mchange amesema hadi Agosti 2020, Serikali ya Awamu ya Tano imelipa madai ya watumishi yasiyo ya mishahara ya kiasi cha Shilingi bilioni 358.1. Malipo hayo yamefanyika baada ya kuhakikiwa na kuyaondoa madai yaliyokuwa yameghushiwa. Serikali itaendelea kulipa madeni ya watumishi kadiri yanavyojitokeza na kuhakikiwa.
“Kufuatia ufafanuzi huu, hakuna mtumishi aliyehamia Dodoma pasipo kulipwa fedha zote za uhamisho wake.” Alisisitiza Mchange.
STAHILI ZA UHAMISHO WA KUHAMIA DODOMA
Amesema wakati Lissu anapotosha kuhusu wafanyakazi kulazimishwa kuhamia Dodoma, ukweli ni kwamba Serikali ilifanya uhamisho wa watumishi wa Wizara na Taasisi zake kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ambapo watumishi 17,080 walihamishwa. Katika uhamisho huo, jumla ya bilioni 134.3 zilitumika kulipa gharama za uhamisho ambazo ni posho ya usumbufu, posho ya kujikimu, posho ya kusafirishia mizigo na posho za nauli kwa familia za watumishi hao.
Watumishi hao walilipwa fedha hizo kabla ya kuhamia Dodoma.
Aidha, Serikali iliendesha zoezi la kuhakiki vyeti vya watumishi ili kujiridhisha kwamba watumishi walioshikilia ajira kwenye utumishi wa umma ni wale wenye sifa stahiki. Uhakiki huo uliwezesha kuwaondoa watumishi hewa kama vile waliofariki, waliotoroka kazini, wenye vyeti vya kughushi na kuwapandisha madaraja watumishi wenye sifa.