Waafrika Upendo wa Dhati hatuna

Kaunara

JF-Expert Member
Feb 4, 2013
240
431
Kiukweli sisi waafrika hatuna upendo kabisa. Ni kitu ambacho kama tunajilazimisha tu kuwa nacho ila ndani yetu hakipo. Sio kwa wote ila kwa wengi wetu hatuna upendo.

Badala ya upendo mwafrika kaumbiwa sifa. Aisee sisi watu tunapenda sifa haijawahi tokea duniani. Angalia tu misafara ya viongozi wa kiafrika ni vichekesho mtu anatembea na msafara wa billion moja kwenda kufungua zahanati ya million 50.

Mwananchi nae unamkuta ana haribu miundo mbinu ya serikali makusudi tu. Kuna jamaa alishikwa anapasua bomba kubwa la maji kisa jirani yake kaunganisha maji na yeye hana.

Magaidi wengi duniani hawaangaiki na waafrika sababu wanajua hawana upendo.

Mfano huwezi kumteka mtoto wa mwafrika au mke wake au mume umwambie atoe kiasi flani cha hela ili aachiwe. Wanajua kabisa hapo mission lazima ifeli tu. Uwezi mwambia mwafrika auze nyumba yake akamkomboe mke.

Soma Pia: Karibu tujadiliane: Changamoto ya tabia zetu Waafrika ukilinganisha na watu wa Mataifa mengine Duniani


Hatuna upendo hata kwa Taifa letu. Mtu unakuta ana kazi nzuri ana maisha mazuri ila bado anauza rasilimali za nchi nje kwa bei nafuu sana. Inafika stage mtu anataman kuingia mkataba wa milele kana kwamba hamna vizazi vijavyo.

Familia nyingi watu wanaishi kama maadui kabisa wa kuombeana vifo. Ukija kwa ndugu unakuta watoto wa baba mmoja na mama mmoja hawaongei. Kwenye ridhiki ndo usiseme kuna vita ya hatari, ushirikina kama wote umejaa.

Hiki kitu kimetufanya mataifa makubwa kutupelekesha sana wanaleta dawa hatari, bidhaa zenye chemicals hatari wanajua kabisa zitaingizwa Africa. Mfano mfanyabiashara anaenda kuleta vitu feki makusudi. Vingine vinahatarisha hata maisha ya watu. Mfano vifaa vya umeme vingi vimeleta maafa na kuharibu mali za watu.

Mtu anaendesha chombo cha moto vibaya barabarani hajali maisha ya watu makusudi huko kote ni kukosa upendo. Unamfanyia ubaya leo mtu usiemjua kesho mtu kwenye familia yako nae anafanyiwa kitu fulani.

Tubadilike Waafrika Yangu ni Hayo.
 
Tujikubali tu hakuna namna,

Ndivyo tulivyo

Wewe ukijipambania ukiwa smart inatosha
 
Mnateseka sana.

Na muendelee vivyo hivyo.

Mimi ni Muafrika na najivunia Utamaduni na Uafrika wangu!

========
This is a typical "Digital
blackface"


Digital blackface is a term used to describe the phenomenon of non-Black individuals using digital media, such as GIFs, memes, or audio clips featuring Black individuals, to express emotions or convey ideas. This behavior has sparked debate and criticism due to concerns about cultural appropriation and the perpetuation of stereotypes.
========

Mleta mada anajinasibu kama Muafrika. Ukweli ni kwamha sio.

Hakuna mwafrika mwenye akili akasema hana Upendo wa Dhati. Hakuna.
 
wenye upendo kila siku wanaunda siraha mpya huko!
Tunazidiana viwango vya ubinafsi tu, maana wao uzalendo kwao ni viwango vya taifa ila sisi huku ni viwango vya familia kila mmoja anahangaikia na tumbo lake na familia yake ninyi wengine mtajijua.

Hizo silaha wanatengeneza ni kwa ajili ya wabinafsi wanaojijali wao na familia zao tu, wanawagombanisha wanawaibia maana bila ubinafsi huwezi ukagombanishwa.
 
Back
Top Bottom