Ninayeandika hapa si mhanga wa ajira baada ya kumaliza chuo kikuu , maana hamchelewi kusema stress za unemployment zinanichanganya.
Nina elimu ya university mwenye shahada ya Usimamizi wa Rasilimali watu na vifani vingine vingi. Ingawa sifanyi kazi ya HRM.
Iwe na sharti kila mahali penye sekondari pawepo na chuo cha kati . Wanafunzi wa vyuo vya kati ndio wabunifu wa mambo mbalimbali na wenye uthubutu kuliko wanafunzi wa vyuo vikuu.
Wanafunzi wa vyuo vikuu wanawaza upigaji tu, yaani wanawaza wapate ajira waanze kuliibia Taifa.
Wahitimu wa universities hapa nchini wanakimbilia siasa wengi wao, si kwa nia njema bali kwa nia ya kupata teuzi na ajira.
Wanafunzi wote wa kidato cha 4 wenye ufaulu wa angalau daraja la nne la alama 33 wapate fursa ya kujiunga na vyuo vya kati na 75% wajiunge na technical colleges.
Nilichogundua ni kwamba mwenye stashahada ya uhasibu anaweza kufanya kazi ya mwenye shahada, mwenye stashahada ya Uhandisi umeme anaweza kufanya kazi ya mwenye shahada ya uhandisi wa umeme.
Tena kwenye ufundi huko wenye stashahada wanaweza kufanya kazi nyingi ambazo wenye shahada hawawezi kufanya. Utofauti wao huyu wa shahada amesomea vitu vingi zaidi ya mwenye stashahada ingawa kuvipractice hawezi.
Kuna umuhimu gani wa shahada?
Mwenye stashahada ya manunuzi anaweza kufanya vizuri kazi ya mwenye shahada ya manunuzi.
Elimu katika kazi hapa Tanzania inatumika tu kutenganisha madaraja ya mishahara bila kujali impact ya mwajiriwa katika kazi.
Elimu hutumika kama kigezo cha kuchagua kiongozi katika kitengo.
Ninaumia sana ninapoona serikali inatumia gharama nyingi kusomesha watoto primary na secondary halafu baada ya hapo serikali inajitoa. Wahitimu wa kidato cha 4 na 6 wako tu mtaani bila ujuzi wowote. Sasa elimu ya sekondari inamsaidia nini mwananchi katika harakati za uzalishaji mali?
Kama serikali inaona mzigo wa kusomesha watoto colleges ni mkubwa wafute kidato cha 5 na 6 kisha nguvu wazipeleke colleges.
Miaka 2-3 ya college kijana anatoka akiwa safi kabisa kupambana mtaani.