Vyama vya Siasa vya Upinzani vipo wapi?

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,958
3,887
Vimekwenda au kupotelea wapi? Yale majigambo na vishindo vya mikutano na maandamano hatuvioni tena? nauliza tu vipi vipooo?

Hata vinara wao hatuwasikii kwenye mahojiano hakuna muendelezo wa mbinu na mikakati ,imekuwa kama hawapo.

Hii ni 2024 tunahesabu miezi tu, au wanasubiri kesho uchaguzi ndio waje na sera za kutulaghai kutaka ibadilishwe tume ya Uchaguzi?

Wakimuachia CCM akitoa jibu muda hautoshi wa kubadili Tume ya Uchaguzi. Mwisho wasiku utawasikia hatuwezi kuwaachia CCM tutaingia kwenye uchaguzi kwa kutumia Tume hiohio iliokuwepo.
 
Waulize CCM wanaoogopa Tume huru, Katiba mpya, Mgombea binafsi, sheria mbovu za uchaguzi watakwambia vyama vya upinzani viko wapi particularly CHADEMA
 
Nikihandika huwaga nawekeza ,kwa maana haya wanayoyafanya Chadema ni kwa ajili ya ulaji hawana tofauti na waita vikao wa CCM au serikali nimekusudia posho.

Posho haina tofauti na ile ijulikanayo chauchau inabidi uzamie sana ndio utaiona.

Madai baba ni kuhusu uchaguzi ujao nini kinasemwa,nini kinaamuliwa na nini kimekubaliwa ,kwa muda tulionao sio wa kumjadili Manenepa ,mambo mengine ni yao wao ikiwa watasemwa watatukanwa ni yao CCM ,upinzani ni lazima kuwepo na ratiba ya mwendokasi kuelekea uchaguzi mkuu ,tusikwepeshwe uhalisia mara tunapelekwa Ukraine kutoka huko transit Gaza na sasa tunaelekezwa Iran ,hayo ni yao.
Hapa chumbani kwetu kiwavi jeshi ccm kila uchaguzi kinatumaliza kiurahisi sana,tatizo sugu ni Tume huru ,tena iwe huru kikwelikweli na kukubaliwa katika hatua zote,sio kututafutia Tume yenye mamluki, wallai CCM watatupiga bao kila uchaguzi.
 
Back
Top Bottom