Vyama vya Siasa Msifuge Nyoka hata kama wametolewa meno. Huwa yanaota baada ya muda flani

Guru Master

JF-Expert Member
Jan 14, 2017
225
594
Ngosha huwa sikubaliani naye na kuna sehemu huwa nakubaliana naye. kuna sehemu anakuwa na ujasili na kuna sehemu anakosa ujasili. lakini nimejifunza kuwa katika vyama ni lazima tufaham katiba zinasemaje na ilani za vyama vyetu.

kama mwenyekiti mlimchagua kwa kuwa alisema sasa ni wakati wa kuelekeza tanga lielekee kusini basi wote inabidi kuelekeza huko na kupiga makasia kuelekea kusini. ikiwa katika hao wapiga makasia watajitokeza ambao wanaona kuwa kusini hakuna jema ni bora kuelekea kaskazini inaonekana ni bora mkawatosa baharini ili wao wasiwe kikwazo. hawa watu hupewa majina kem kem likiwepo moja kubw ala WASALITI. tumeona watu hawa katika vyama mbalimbali wakiitwa majina hayomna badaye wakatupwa baharini .

wazungu wanasema "give a dog a bad name then hang it" ni kuwabatiza tu majina ya kuudhi , ya kutisha na baadaye nahodha anatoa wazo kuwa hawa watupwe baharini. wanatupwa na safari inaendelea.

nyoka wakufugwa huwa wanatolewa meno na baada ya hapo wanakuwa hawana madhara kabisa. lakini hamna budi kukumbuka huwa nyoka hawa wanaota meno tena.si kwamba watakuwa vibogoyo milele. hivyo ni vyea kukumbuka kuwa ng'oa meno kila mara lakini ili usiwe na hofu na mashaka hayo kwa nini uendelee kufuga nyoka hao? wakate vichwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…