Vyakula bei juu, hakuna njaa?

Nakubaliana na wewe, swali langu watavuna nini wakati mazao yamekauka mashambani kutokana na ukame unaoendelea? Nchi inakabiliwa na ukame, labda tusubiri wanaopata mvua kuanzia April/March kama mvua zitaenda vizuri, kwa maeneo ambayo mvua zinaanza November hakuna matumaini mimea ilishanyauka, na kumbuka maeneo ambayo huwa na mvua za vuli mwaka uliopita hayakupata kitu kufuatia ukame mkubwa uliyoyakumba maeneo hayo
Mkuu hapo unatwanga maji ndani ya kinu, anajua kila kitu lakini ameamua kua mnafki kuufunika ukweli. Watu wa aina hii ndio waliolifikisha taifa letu hapa lilipo.
 
Tunachoshindwa kuelewa ni kwamba mkilima hua hatunzi Chakula cha kuuza, anatunza kiasi kidogo tu cha kukidhi mahitaji yake na familia yake kwa muda flani, sasa inapofikia muda wa Chakula chake kuisha ndipo matatizo yanapoanza.Mtunza Chakula cha kuuza ni mfanyabiashsra ambayo hununua nafaka mapema kabisa msimu unapoanza.
Nakubali mkuu, shida ninayoiona ni mkulima alitegemea angevuna baada ya mvua za vuli kwa bahati mbaya mvua hazikutosha na maeneo mengi mazao yalinyauka, ikaja wanaopata mvua za masika October/November nazo maeneo mengi mvua zikawa haba nao mazao yamenyauka sasa tunasubiri wanaopata masika ya February/march pengine ndio itakua mkombozi na majuzi nikiwasikia hali ya hewa wakisisitiza wakulima wapande mazao yanayostahimili ukame, hii inaashiria mvua hazitokua nzuri sana kama utabiri wao utakua sahihi
 
Hivi vyakula nafaka aina zote kwa sasa bei iko juu inayoendea kua mara mbili ya bei ya mwaka Jana, hivi ni kweli hakuna njaa au ni mabadiliko ya mfumo wa msisha? Mfano kilo moja ya unga wa mahindi kwa sasa ni 1600 hapa mkoani Arusha, hiki ni kiashiria cha nini? hii ni January lakini kufikia Aprili hali itakuaje?

Nakumbuka Mh Rais aliwahi kuwaambia wakulima wauze vyakula kwa bei waitakayo, kwahiyo inawezekana kabisa hata udhibiti wa bei hizi inaweza kua ni tatizo kwa sababu ya kauli kutoka juu! Kuwaambia wakulima wauze mazao kwa bei watakazo wao ni sawa na kuwapa rungu kuwaponda walaji hasa zile familia zinazoshindia mlo moja kwa siku.

Kiuhalisia hali si salama kabisa upande wa vyakula kwa sasa, bei zinapaaa kwa kasi na hakuna udhibiti wowote Kama ilivyokua kwenye sukari na wananchi hawana cha kusema.Sio wakulima kuuza vyakula kwa bei watakazo tu bali ni uhaba wa bidhaa hizo, hatuwezi kuendelea kusema tuna Chakula cha kutosha huko kumbe tuapigia mahesabu ya bidhaa za wafanyabiashara bila hata udhibiti wa bai zake.

Sisi makabwela huku mitaani hatuna uwezo wa kusema kwamba kuna njaa kwa sababu ni kauli ya kuudhi ila lazima tuseme ukweli kua hali ni ngumu sana huku. Mtu unaweza kusema kua huna maradhi flani lakini unashindwa hata kutembea watu wanaweza kukushangaa.Hivyo sisi huku mtaami hali halisi ya vyakula Mungu anaijua.
Hayo niabadiliko ya mfumo wa msisha wala hamna jingine
 
Mkuu kwanza elewa kuwa kwa sasaiv hamna mkulima mwenye maindi yakuwa anapandisha bei hamna mkulima hata mmoja ..maindi yote yapo kwenywe matajiri wafanya biashara walinunua maindi yapo kwenywe go down zao wao ndio wanauzza wanavyotaka kwa saiz ila hali ni mbaya maindi kilo ni alfu 1
Huo ndo ukweli...na walioshangilia lile tamko LA ajabu kuwa mahindi(chakula) watu wauze bei waitakayo ni wafanyabiashara wakubwa ambao tayari walikuwa na stock kubwa walonunua kwa wakulima kwa bei ya chini....wanaoumia asilimia kubwa ni wakulima..mimi sijui hawa watawala wetu huwa hawajui uhalisia au wenyewe ndo wenye biashara ya vyakula?
 
Nakubaliana na wewe, swali langu watavuna nini wakati mazao yamekauka mashambani kutokana na ukame unaoendelea? Nchi inakabiliwa na ukame, labda tusubiri wanaopata mvua kuanzia April/March kama mvua zitaenda vizuri, kwa maeneo ambayo mvua zinaanza November hakuna matumaini mimea ilishanyauka, na kumbuka maeneo ambayo huwa na mvua za vuli mwaka uliopita hayakupata kitu kufuatia ukame mkubwa uliyoyakumba maeneo hayo
Hizo porojo tu,njoo huku Rungemba,mvua mahindi yamestawi.Tanzania tuna mikoa inaitwa Big4.Rukwa,Iringa,Mbeya na Ruvuma ndio inalisha nchi.wewe uko sehemu gani ya Jamhuri hii?mie nipo Rungemba huku mvua kede kede na tutavuna haswa
 
Usiwe mjinga kiasi hicho, unakataa kitu gani sasa? Kwa kawaida hata kama kuna demand kubwa kiasi gani lakini bei mpya hua hauzi nusu ya bei ya awali. Tazama bei ya vyakula ya January mwaka Jana na October mwaka juzi. Yaani bei ya kitu ikifikia zaidi ya nusu ya bei ya ujue kuna tatizo kwenye production na sio kama unavyodhani kwa unafki wako. Hii bei ya kiolo moja ya mahindi ya sasa ambayo swali ilikua Tshs 900 hata Kama demani ikipungua haiwezi hata kufikia 1200.
Utumie akili kufikiri na sio siasa uchwara muda wote kwakua huna kazi ya kufanya.
Kwenye demand,inategemea na supply ilivyo.huwezi kupanga bei kwamba kwa kuwa mwaka jana,ilikuwa 900,basi mwaka huu isifike 1500!hiyo ni commerce haipingiki mkuu,waliotunza mahindi kwa sasa ndio wanatajirika,hapo ndio maana mliambiwa muanzishe mfumo wa stakabadhi ghalani.Na mtatia akili sasa,badala ya kutengenezea pombe mahindi na kuchezea ngoma,msimu ujao kila mtu atakumbuka kuweka akiba,baada ya kuambiwa hakuna chakula cha msaada.
Sie tulio Rungemba hatuna wasiwasi mvua nyingi sana,na tutavuna sana msimu huu,kazi kwako wewe unaeishi manzese
 
Back
Top Bottom