KERO Vodacom wamekuwa na makato yasiyoeleweka kwa mawakala wa mitandao ya kifedha hasa Mbeya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Vodacom wamekuwa na makato yasiyoeleweka kwa mawakala wa mitandao ya kifedha hasa mkoa wa Mbeya, inapokaribia mwisho wa mwezi wanakata pesa kwenye faida ya wakala ambayo angeipata, ukiwapigia na kuwauliza hawana sababu za msingi zaidi ya kusema kuna miamala feki imefanyika, zaidi ukiwauliza miamala feki ni ipi wanakuwa hawana majibu rasmi zaidi ya kusema eti ukituma pesa nje ya wilaya au mkoa basi huo muamala unahesabika kama muamala feki, sasa unajiuliza kwamba unatakiwa kila mteja umuulize anaituma fedha kwenda wilaya gani au mkoa gani?

Kitu ambacho siyo rahisi na kinaweza kisilete taswira nzuri kwa mteja kumuuliza mana atahisi unamdadisi, lakini pia najiuliza kwanini ni kwa mtandao mmoja tu wa Vodacom na isiwe kwa mitandao yote?

Hii inaleta hofu kwa mawakala kuwa yawezekana kuna mazingira fulani yanatengenezwa kupitia mtandao huo, Naomba uongozi wa juu wa Vodacom utupe ufafanuzi kidogo kuhusu hili na serikali iliangalie kwa jicho la pili mana linaturudisha nyuma wafanyabiashara wa miamala ya simu, mana wanakata hela nyingi kupitia sababu Yao ya miamala feki.

Naomba kuwasilisha
 
Biashara ya.uwakala nasikia.mnamtajirisha yule super.dealer wenu mnagawana.nae anachukua.cha.juu.

Alex mlay.njoo.utoe.ufanunuzi.haraka
 
Back
Top Bottom