Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 339
- 705
Mahakama ya juu ya Rufaa Nchini Afrika Kusini imetupilia mbali rufaa ya Vodacom dhidi ya mbunifu wa Huduma ya “Tafadhali nipigie”, Kenneth Makate ambaye alikuwa Mfanyakazi wa Vodacom
Aidha, Mahakama imeiamuru Vodacom imlipe Makate kati ya asilimia 5 hadi 7.5 ya jumla ya mapato yaliyotokana na Huduma hiyo kwa zaidi ya Miaka 18 iliyotumika, pamoja na riba.
Makate alikuja na wazo hilo zaidi ya Miaka 20 iliyopita alipokuwa na uhusiano wa mbali na Mkewe, ambaye wakati huo alikuwa Mwanafunzi. Mzozo kati yake na Vodacom ulianza Mwaka 2007
Mtendaji Mkuu wa zamani wa Vodacom alimuahidi Makate fidia kwa ubunifu wake, lakini baadaye Kampuni ilisitisha Mpango wa kufanya hivyo pale Huduma hiyo ilipofanikiwa.
Wazo la "Please Call Me" linamsaidia Mtumiaji asiye na muda wa Maongezi kuweza kutuma ujumbe wa Maandishi kwa mwingine ili kumshawishi ampigie Simu.