Vodacom kukubali kutoa ushahidi dhidi ya Lema ni dharau kubwa kwa watanzania

Habari wakuu.

Mwenzako akinyolewa wewe kazi tia maji kwani zamu yako yaja, vodacom wamekubali kutoa siri za mteja wao, leo limemkuta Lema, kesho hatufahamu itakuwa zamu ya nani.

Kwa maana hiyo ni dhahiri Vodacom wameshapoteza uaminifu kwa wateja wao, kilichobakia ni sisi kuanza kuwakataa wao mapema kabisa kabla hatujaadhirika, mitandao ya simu ipo mingi mizuri na huduma nzuri tu zinatoa, kuanzia leo tuanze kuikataa vodacom na tutafanya hivyo kwa kuacha kutumia line zao, wajulishe ndugu na jamaa na wazalendo wote tuihame vodacom tuende kwenye mitandao inayowajali wateja wao na kuwasitiri. Ipo mingi sana.

Kuna Halotel, Tigo, Zantel, Ttcl n.k

Sema hapana vodacom.........

Say NO to vodacom Tanzania.........

Renew line yako ile ile kwa mtandao mwingine......

[HASHTAG]#KampeniKataaVodacomTanzania[/HASHTAG]
kaka kwa usalama wa taifa usidhani unaweza jificha ndani ya mipaka ya nchi labda uwe nje ya nchi ndio unaweza kua huru,Tuwe makini tu na tuwaache vodacom wapige pesa
 
Nimepata sababu nyingine ya kukitupa ki simcard cha voda kikifuatiwa na vya wategemezi wangu pamoja na
marafiki zangu!!
Sababu ya kwanza- Network yao iko hovyo sana kwa upande wa internet!
(2)makato makubwa wakati wa kufanya Transactions

(3) Haina vifurushi rafiki kwa mtumiaji! Mfano sh 1000 unapata c
hini ya Mb 10 kwa siku moja wakati airtel kwa sh 700 unapata 1.2Gb+muda wa maongezi wa kutosha
(4) KUTOA SIRI ZA WATEJA wao kwa maadui
 
kaka kwa usalama wa taifa usidhani unaweza jificha ndani ya mipaka ya nchi labda uwe nje ya nchi ndio unaweza kua huru,Tuwe makini tu na tuwaache vodacom wapige pesa
Wapige pesa sijakataa mkuu ila mimi wameshanipoteza tiyari, nilikuwa mteja wao mzuri sana tena wa prepaid! sasa hii kampeni haiishii kwangu tu bali nitaipeleka kwa watu wangu wa karibu pia
 
Wapige pesa sijakataa mkuu ila mimi wameshanipoteza tiyari, nilikuwa mteja wao mzuri sana tena wa prepaid! sasa hii kampeni haiishii kwangu tu bali nitaipeleka kwa watu wangu wa karibu pia
ok boss pole sana
 
Vodacom hawawezi. Otherwise watu wataogopa sana kutumia laini za voda kwa mambo yao ya siri. Na ndo kupoteza wateja huko
 
Mm niliiacha siku nyingi sana
Wapige pesa sijakataa mkuu ila mimi wameshanipoteza tiyari, nilikuwa mteja wao mzuri sana tena wa prepaid! sasa hii kampeni haiishii kwangu tu bali nitaipeleka kwa watu wangu wa karibu pia
 
Back
Top Bottom