Vladimir Vetrov, jasusi aliyejitakia kifo chake mwenyewe

mcTobby

JF-Expert Member
Feb 16, 2018
4,313
12,686
Mtu mpaka anafikia kiwango cha kuitwa Jasusi , huyo sio mwenzako tena. Amini nakwambia .Anyway leo nakupa kisa kimoja hivi;

Siku moja Kwenye moja ya mitaa ya jiji la Moscow, maafisa wa polisi walifika eneo la parking ya magari. Hii na baada ya kutaarifiwa kuna tukio la mauaji limetokea muda mchache uliopita. Hapa nazungumzia mwezi February ,1982. Hawa mapoti walichokiona eneo la tukio kilikuwa kinatisha kiasi.

Ni baada ya kukutana na maiti ya bwana "mmoja" imelala chini ikitokwa damu kutokana na majeraha ya kuchomwa visu vya kutosha. Pembeni alikuwa amelala mwanamke ambaye naye alikuwa amechomwa visu akiugulia majeraha ila hakuwa amekufa.

Katika harakati za kufanya uchunguzi wa awali , hawa maafisa walishtuka baada ya kugundua aliyeuawa ni mmoja wa maafisa wa ngazi za juu wa KGB na pia huyo mwanamke ni mwajiriwa wa KGB akifanya kazi kama secretary. Katika huu mkasa ikumbukwe tayari wazee wa KITENGO chao tayari nao walikuwa wamewasili eneo la mkasa kujua nini kinaendelea la kutaka kujua nini kimemkumba afisa kipenyo mwenzao.

Katika harakati za hapa na pale huyu madam aliyejeruhiwa na kisu alimpoint mtu mmoja miongoni mwa wale waliofika kwenye mkasa huu akimhusisha na tukio hili la mauaji na kumjeruhi yeye.

Mtu aliyepointiwa ni mwanaume mmoja umri wa makamo wa miaka 54 ambaye naye ni afisa wa KGB mwenye chao cha luteni kanali kwa jina Vladimir Vetrov.

Vladimir_Vetrov.jpg

Baada ya polisi kuonyeshwa huyu mtu, alitiwa pingu haraka haraka na baada ya hapo akakutwa na kisu butu mfukoni kilichotumika kuufanya huu unyama .

Sasa hii kesi ilionekana kuwa ngumu Kutokana na kuusisha watu wa kitengo kimoja , hivyo kwa upande wa polisi wa kawaida ingekuwa ngumu kumeza kudili na kesi ya aina hii.

Wazee wa kitengo yaani KGB wakaamua kuisimamia hii kesi wenyewe huku wakijaribu kuifichaficha isiende Viral/yaani isijulikane na Umma. Huyu bwana vetrov baada ya kakabidhiwa kwa KGB wenzake na kufanyiwa interrogation HEAVY alichukuliwa maelezo ya kukiri kosa CONFESSION.

Katika maelezo yake , huyu bwana alikiri Hivi; ni kweli alikuwa akitoka kimapenzi na workmate mwenzake ambaye ni secretary. Sasa wakiwa wamepark gari pembezoni mwa barabara yeye na mpenzi wake huyo wakipata shampeni alitokea mwanaume mwingine amabaye naye alikuwa ni afisa wa KGB, akagonga dirishani ili wasalimiane kwakuwa walikuwa wanafahamiana na wote ni wafanyakazi wa KGB.

Huyu bwana vetrov akapaniki akiamini na kuhisi labda anakamatwa kwa kuwa huyo bwana alikuwa mkubwa kicheo kushinda yeye. Akaamua kutoa kisu na kumchoma huyu afisa mwenzake na kumuua hapohapo. Sasa huyu bidada ambaye naye ni secretary aliyekuwa na vetrov akataka kukimbia kwa kuona hali hii ya msala .

Farewell-Vetrov.jpg

Sasa huyu vetrov akamuwahi na kumchoma visu kadhaa ,na kumuacha na majeraha na kuondoka eneo la tukio akiamini naye amekufa. Lakini baadaye alirudi (kujiridhisha) na wenzake waliosikia habari kuhusu mauaji ya mwenzao. Sasa hapo ndipo huyu secretary akawaonyesha polisi kwamba huyu vetrov ndio mhusika mkuu na hapo ndipo alikamatwa
.
Sasa kitengo cha kukabiliana na ujasusi ,ndani ya KGB COUNTERINTELLIGENCE UNIT wakaamua kuivalia njuga hii kesi kijasusi zaidi. Wakaanza kujiuliza maswali , imekuwaje amemuua afisa mwenzake kirahisi hivyo ? maana basi kama ingekuwa labda ni ishu ya wivu kimapenzi kwa kutoka na secretary wa kitengo isingekuwa kosa ambalo lingeweza kuzua big dili sana hata kama huyo secretary alikuwa anatoka wakubwa wa kitengo. (kiuhalisia huyu Vetrov alikuwa ameoa na ana familia yake na ilikuwa kosa ambalo ungeweza kuadhibiwa na wakubwa wa KGB kama ungekuwa na mahusiano ya nje huko na of course wale walio maafisa wa ngazi za chini yaani KGB junior officers ndio kidogo hii sheria ilikuwa ikiwabana. Lakini ukiwa na cheo hata level ya ukanali kuna mambo au makosa wangepotezea ikiwemo hili).

Sasa maafisa wa kitengo hiki cha counterintelligence wakandelea kujiuliza sasa nini kilijiri baina ya hawa maafisa wawili yaani vetrov na marehemu? Nini kinafichwa? Hawa jamaa hawakuwa na majibu ya haraka haraka katika kutegua kitendawili hiki cha mauaji. Waliamua kumfuatilia huyu bwana Vetrov mienendo yake .

Na kweli kwa kuwa huyu bwana vetrov alitenda kosa la jinai alipatikana na hatia na akafungwa miaka 12 kwenda jela. Sasa akiwa jela huyu bwana vetrov aliendelea kufuatiliwa nyendo zake zote kimya kimya. Sasa unajua mtu ukifungwa kwa hizi nchi za wenzetu unaruhusiwa kupokea au kutuma barua kutoka kwa uwapendao mfano mke ndugu n.k. kwa kuwa bwana vetrov alikuwa anachunguzwa na kufuatiliwa mienendo yake akiwa jela,automatically hata barua pepe alizokuwa akituma au kupokea kutoka kwa mkewe zikawa zinasomwa na KGB.

Katika kusoma moja ya barua ya vetrov kwenda kwa mke wake , hawa KGB walipata "clue" moja ya sababu zilizokuwa nyuma ya mauaji haya. Vetrov katika barua hiyo kwenda kwa mkewe aliandika na kusema sababu ya yeye kuawa ilikuwa ni kuficha "SOMETHING BIG". KGB wakaanzia hapo kuisolve hii kesi upya kutaka kujua hiyo something big iliyotakiwa kufichwa ni nini?.....Haijulikani sana huyu bwana vetrov alifanyiwa nini na hawa KGB wenzake huko sero ,kama ni kuteswa au kunyweshwa TRUTH SERUM, no body knows ...lakini alijikuta anaropoka yotee kwa kuandika kwa mkono wake mwenyewe maelezo ya kukiri kosa yenye kichwa kinasema CONFESSION OF A TRAITOR.. sababu za yeye kumuua afisa mwenzake wa KGB tena wa cheo cha juu.

Maelezo yake haya yaliposomwa na maafisa wenzake wa KGB... OHHH MY GADE walipatwa na mshtuko wa karne. Kama walikuwa wanawake basi matumbo ya uzazi yaliwacheza.

Katika waraka wa kukiri kosa , bwana vetrov alikiri na kufunguka kwamba yeye alikuwa ni "MOLE" au pandikizi , akiifanyia kazi shirika la kijasusi la Ufaransa kwa kuwauzia Classified documents za KGB kwa miaka kadhaa. Na mbaya zaidi alikiri kutoa siri ambayo Kwa KGB ilikuwa ni kama jeraha la moyo ambalo halikuwahi kupona hadi Dola ya sovieti ,USSR inaanguka .

Kwanza kulichowashtua ni kwamba huyu vetrov alikuwa ni mmoja wa maafisa ndaniya KGB walioheshimika zaidi katika kujitoa kwake kuitumikia serikali ya soviet na zaidi shirika la kijasusi la KGB,na sasa amegeuka msaliti kwa nchi yake mwenyewe.

Huyu bwana vetrov kitaaluma alikuwa mhandisi na alipohitimu tu chuo kikuu aliajiriwa na KGB na kupewa jukumu la kusimamia kitengo maalumu ndani ya KGB kilichojulikana kama LINE X kilichoanzishwa punde tu alipojiunga na KGB.

Kitengo hiki kiliundwa mahsusi baada ya bunge la soviet kuambiwa kwamba serikali ya USSR ipo nyuma kwa miaka 30 kiteknolojia dhidi ya marekani karibia kila nyanja. Sasa kitengo hiki kikaundwa kwa ajili ya kuiba teknolojia ya nchi za magharibi ikiwemo U.S. ili ku "match" au kuwapita mbali. Sasa ikawa kwamba hiki kitengo kikaajiri majasusi wenye taaluma mbalimbali kwa ajili ya kuiba kila nukta ya teknolojia ya magharibi.

Na kweli ndani ya mwaka mmoja kitengo hiki cha Line X kikawa kimepata nyaraka za siri kuhusiana na western technology zaidi ya 5000 wenyewe kwa lugha ya kijasusi zikiitwa "industrial samples" walizozipata kwenye nchi za magharibi.

Sasa ghafla nchi za magharibi zikaanza kushtuka ,mbona kama Mrusi anakuja kwa kasi kiviwanda? Tena kwa muda mfupi? Wazungu wa magharibi wakawa wanajiuliza huyu mrusi ametoa wapi teknolojia ambayo wao walikubaliana iisiwahi uzwa kwa nchi yoyote yenye mfungamano na Soviet bloc? Hili swali halikuwa rahisi kulijibu.

Sasa kwa upande wa bwana vetrov aliyekuwa na jukumu la kusimamia hii unit ya line X ndani ya KGB alifurahishwa jinsi soviet ilivyokuwa inapata "upper hand" kiteknolojia . Viwanda vikubwa vya kutengeneza ndege za kisasa , kurusha satellite kwenye anga za juu ,kustawi kwa makampuni makubwa ya kisoviet, haya yote yalimfurahisha huyu bwana Vetrov.

Lakini huyu bwana kuna jambo lilimfanya kuwa na mashaka sana au self doubts. Katika mafanikio haya yote ya nchi yake kiteknolojia kuanzia ya kutengeneza kijiko hadi teknolojia ya kurusha satellite inayoizunguka dunia ya soviet, matunda haya yote yalikuwa hayamnufaishi mwananchi hata kidogo. Wa Russia wenzake waliendelea kubaki kwenye umaskini na ufukara ule ule .

Kama ni kupanga foleni kwenye maduka kwa masaa kadhaa ili wapate mkate kulikuwa palepale huku roketi kubwakubwa zikipitishwa mbele ya magwaride makubwa ya kijeshi kila ifikapo siku ya wafanyakazi ya mei mosi. Hii ilimfanya awe na doubts sana. Mafanikio haya yote ya nini ikiwa tabaka la raia wa kawaida hawafaidi matunda yake? Haya aliyahifadhi moyoni mwake tu .

Sasa huyu bwana vetrov akiwa kwenye mission ya kikazi jijini Paris mwaka 1965 akisimamia moja ya operesheni za Kitengo cha Line X ,alijikuta akilinganisha maisha ya raia wa kawaida wa ufaransa na yale maisha ya wa Russia wenzake huko kwao. Akagundua kwamba kumbe raia wa kimaskini wa kifaransa ana maisha mazuri ambayo standard ni kama ndoto kwa raia wa kawaida wa urusi.

Katika harakati za hapa na pale huyu bwana siku moja alijikuta amepata ajali baada ya kugongana na gari nyingine ya mfaransa aliyokuwa akiiendesha. Bahati nzuri hakupata majeraha ila gari ilipata uharibifu kiasi. Sasa huyu mfaransa alikuwa mtu poa sana . Ile kiuanaume huyu Frenchman akalipa gharama ya kuifanyia service hiyo gari ya vetrov na hapo urafiki wao ndipo ukaanzia. Sasa hapo ikawa kwamba huyu bwana vetrov akaanza kufunguka kuhusu DOUBTS alizokuwa nazo dhidi ya nchi yake mbele ya huyu rafiki yake mpya wa kifaransa.

Asichokuwa anakifahamu bwana vetrov kwa wakati huo ni kwamba huyo rafiki yake mfaransa ambaye alijitambulisha kwa vetrov kama mfanyabiashara alikuwa ni "ASSET" maalumu aliyeajiriwa na shirika la kijasusi la Ufaransa la DST kwa ajili ya kufuatilia nyendo za huyu Vetrov. Hata ajali ilyotokea ilikuwa imetengenezwa mahsusi "STAGED" kwa ajili kumjua vetrov kiundani zaidi.

Maana hapo ufaransa alionekana tu kama "Russian diplomat" tena mwenye cheo kidogo ila alianza kuhisiwa yawezekana ni KGB agent tena mwenye cheo kikubwa kiasi. Sasa DST baadaye walikuja kugundua kumbe huyu vetrov ni afisa mkubwa tu kwenye rank za KGB baada ya vetrov kuwaambia kwamba anahusika na kitengo maalumu cha KGB kinachohusika katika kuiba teknolojia mbalimbali za nchi za magharibi, hivyo wakawa wanachukua tahadhari zote zile katika kumpeleleza na "kumCULTIVATE" ili asijekuwa ni mtego au "DANGLE". ....

Hebu kabla ya kuendelea nikupe maana ya hayo maneno mawili yanayotumika kwenye ulimwengu wa kijasusi. Cultivate ni neno la kiingereza likiwa na maana rahisi ya "kuvuna" labda mazao n.k. Sasa kwenye ulimwengu wa kijasusi cultivate ni ile kupata taarifa za kiintelejensia kutoka kwa Agent au mole aliyewekwa au aliyeamua kwa mapenzi yake kuifanyia kazi idara fulani kwa kuanza kumpa pesa, kujenga urafiki yaani ile personal bond n.k.

Kwa mfano CIA Wawe na mole ndani ya shirika la kijasusi la China akiwapa taarifa za kijasusi , hapo ndio ina maana ya kuvuna yaani "cultivate " baada ya kujenga mahusiano naye, kumpa pesa na kila anachokihitaji. Sasa neno la pili "DANGLE" lina maana ya kuning'inia , yaani something hanging loosely.

Kwa mfano embe likiwa mtini pale juu lina "dangle" . Yaani dangle, dangling, dangled. Au kwa sisi wanaume kitendo cha mapumbu kuning'inia ile inaitwa dangle japo ni neno la kihuni .

Slang!Nadhani nimeeleweka. Sasa kijasusi lina maana ya Jasusi aliye mguu nje mguu ndani anaweza kujifanya ni mole anayetaka kuifanyia kazi idara fulani kumbe lengo lake ni kutaka kupata info za upande mmoja akijifanya kuwafanyia kazi na kuzipeleka upande huu. Simple like that.
tuendelee.........

Sasa ilipofika mwaka 1970, majukumu yake ndani ya ufaransa yalikamilika na alihitajika kurudi makao makuu ya KGB nyumbani Russia. Lakini aliendelea ku maintain mawasiliano baina yake na huyu rafiki "mfanyabiashara" wa kifaransa. Huyu mfanyabiashara ambaye kiuhalisia alikuwa ni agent wa DST hakutaka kumrecruit au kumtumia moja kwa moja bwana vetrov kupata infos za kijasusi kuhusiana na mipango ya Russia kiteknolojia ila tu alimwahidi kusaidiana kiundugu tu endapo wangehitajiana hata kama angerudi Russia. DST walijipa muda kujiridhisha kabla ya kumtumia huyu vetrov.

Na kweli hawa DST uvumulivu wao uliwalipa ilipofika mwaka 1980. Hii ni baada ya vetrov kumuandikia huyu rafiki yake wa kifaransa barua akitaka wakutane jijini Moscow.

Na kweli baada ya kukutana kama walivyopanga huyu Vetrov aliamua kuwa mole akiwafanyia kazi hawa DST wa ufaransa akiwapa infos za kilichokuwa kikiendelea kwenye korido za kremlin. Na kweli alimkabidhi huyu "mfanyabiashara" nyaraka za siri zilizo na stempu ya PHOTOCOPY FORBIDDEN.

Hizo nyaraka zilifunua mipango yote kuhusiana na kuiba teknolojia ya magharibi kwa manufaa ya Russia.
Kwakuwa huyu vetrov hapo makao makuu ya KGB alikuwa kwenye idara iliyojulikana kama Department "T". au technological espionage department , alikuwa na access ya mafaili na nyaraka za siri zilizohusiana na technological issues, DST waliamua kumpa camera maalumu ya high speed ya siri ili aweze kupiga picha nyaraka zote za siri hapo ofisini.

Sasa mikanda ya kaseti yenye picha zote alizopiga alizikabidhi kwa DST kupitia kwa afisa mmoja ndani ya ubalozi wa ufaransa hapo Moscow ,ambaye aliwekwa spesho na DST kwa ajili ya kupokea 'mzigo' huo. Nyaraka alizozikabidhi vetrov pia zilifunua mipango yote ya Russia kwenye maeneo ambayo wapo weak kiteknolojia na wanayafanyia kazi kwa kuiba western technology na zaidi alitoa document yenye majina ya agents zaidi ya 300 waliopandikizwa sehemu mbalimbali za nchi za magharibi ikiwemo ufaransa wakiwa kwenye mission ya kuiba western technology katika maeneo wengi wakiwa maafisa wa KGB na GRU pamoja na wenzao ambao ni assets raia wa nchi hizo za magharibi wakifanikisha mipango hiyo kama 100.

Hili lilikuwa ni pigo moja takatifu kwenye shirika la KGB.Sasa wafaransa kwa maana ya DST Baada kugundua Mole wao vetrov amekamatwa na kufungwa, waliamua kupiga kwenye mshono wenye kidonda kibichi.

Nchi ya ufaransa iliamua kuwafukuza wanadiplomasia wa Russia 47, huku nchi nyingine za ulaya magharibi zikiwafukuza wanadiplomasia takriban150 wa Russia.

Russia kwa kuona hivi ili kupunguza maumivu haya iliamua kuwarudisha majasusi wake walioko kwenye mission zaidi ya 200 kutoka kwenye nchi za ulaya magharibi kabla ya kufukuzwa kwa aibu au kukamatwa.

Kwa maana hii ni kwamba kitengo cha LINE X automatically kikawa kimekufa au kusambararitika ,huku marekani mpinzani mkubwa wa Russia akijiimarisha zaidi kijeshi na kiviwanda haswa kipindi cha utawala wa Ronald Reagan.

Hapa sasa ikawa na maana kwamba Russia ikabidi atumie tu resources zake katika kujiimarisha kinyonge ambapo mwisho siku hii ikawa ni sababu mojawapo ya KUANGUKA kwa utawala wa soviet miaka michache baadaye.

Tukirudi kwa vetrov baada ya kugundulika na KGB pasipo na shaka kumbe yeye ni TRAITOR kwa nchi yake , waliamua kumfanyizia kama wanavyowafanyizia wasaliti wengine.

Katika sehemu ya mwisho ya waraka wake wa kukiri kosa alimalizia kwa kusema , nanukuu."My only regret is that I was not able to cause more dam- age to the Soviet Union and render more service to France.". Waraka wake haukuwashawishi KGB atleast kumsamehee.

Ni siku moja tu mwaka 1983 ilifika majira kuchipua(spring) , huyu bwana vetrov akiwa jela alifuatwa na kikosi kazi cha KGB na kupelekwa mahali pasipojulikana akaamriwa apige magoti kisha PAAH.... PAAH! risasi ya kisogoni then No more R.I.P. na kuzikwa kwenye kaburi lililojulikana hata alama. Hiyo ndio ilikuwa ultimate punishment kwa msaliti kama yeye. Huyu bwana alipewa jina la uficho ,codename na wafaransa akiitwa FAREWELL.
 
View attachment 3299507

View attachment 3299510

Kazi nzuri...
Nje na yote bwana vetrov alitumia njia mbaya ktk kutaka kuleta marekebisho ya maisha ya watu wa chini!, ninapata mashaka na uwezo wake wa akili ama ni aliona vita itakuwa kubwa kama angeanza kupambania kubadilisha ujamaa ktk nchi yake!.

Ahsante kwa bandiko zuri mkuu.
 
Ndioo maana alijitakia kifo kizembe
 
Back
Top Bottom