Viwanda vya kuunda mabasi vilazimishwe kuzalishia mabasi Tanzania

1. Kama mnavyojua sekta ya USAFIRISHAJI imekua kwa kiasi kikubwa. Lakini la kusikitisha mabasi yaliyo Mengi huagizwa China na Kenya.

2. Je haiwezekani kuwalazimisha wenye viwanda hivyo kujenga "Assembly plant" nchini kuongeza ajira, Kodi na ukuzaji/urithishaji teknolojia/maarifa kwa wazawa?

NB: waagizaji nao walazimishwe kununua basi nchini Tu.

**SIDO, NIT, UDSM (CoET), DIT amkeni
Mambo ya kulazimisha kwenye biashara hayaleti matokeo. Muhimu ni kuweka mazingira bora kuwezesha mafanikio.
Tanzania ilikua na viwanda vya kuuunda mabodi ya mabasi miaka ya zamani sana. Tafiti sababu za mafanikio Kenya Ili upate ufumbuzi wa tatizo
 
1. Kama mnavyojua sekta ya USAFIRISHAJI imekua kwa kiasi kikubwa. Lakini la kusikitisha mabasi yaliyo Mengi huagizwa China na Kenya.

2. Je haiwezekani kuwalazimisha wenye viwanda hivyo kujenga "Assembly plant" nchini kuongeza ajira, Kodi na ukuzaji/urithishaji teknolojia/maarifa kwa wazawa?

NB: waagizaji nao walazimishwe kununua basi nchini Tu.

**SIDO, NIT, UDSM (CoET), DIT amkeni
Waundaji wa body za mabus mbona wapo,mfano kuna Dar coach,kuna Quality group
 
Zamani kulikuwa na kampuni zinachonga bodi za mabasi lakini kwa sasa zimepotea.
Quality Garage, Kartar Singh and Hari Singh na Scania.
Lakini nadhani kwa sasa hazifanyi kazi hiyo tena.
 
Zamani kulikuwa na kampuni zinachonga bodi za mabasi lakini kwa sasa zimepotea.
Quality Garage, Kartar Singh and Hari Singh na Scania.
Lakini nadhani kwa sasa hazifanyi kazi hiyo tena.
Ni janga Hilo tusikubali
 
1. Kama mnavyojua sekta ya USAFIRISHAJI imekua kwa kiasi kikubwa. Lakini la kusikitisha mabasi yaliyo Mengi huagizwa China na Kenya.

2. Je haiwezekani kuwalazimisha wenye viwanda hivyo kujenga "Assembly plant" nchini kuongeza ajira, Kodi na ukuzaji/urithishaji teknolojia/maarifa kwa wazawa?

NB: waagizaji nao walazimishwe kununua basi nchini Tu.

**SIDO, NIT, UDSM (CoET), DIT amkeni
Kuna masingasinga wa Khatar Singh & Hari Singh walikuwa mtu na kaka yake, walikuwa na kiwanda cha kutengenezea ma body ya malori na mabasi. Unaagiza engine na kichwa wanatengeneza body.

Sijui kile kiwanda chao Pugu Road kimeishia wapi.

Pia kulikuwa na kiwanda cha Auto Mech walikuwa wanatengeneza parts nyingi za magari nchini.

Sijui kimeishia wapi.

Hiyo ni Tanzania ya miaka ya 1970 mpaka 1980 tulishafikia huko.
 
Zamani kulikuwa na kampuni zinachonga bodi za mabasi lakini kwa sasa zimepotea.
Quality Garage, Kartar Singh and Hari Singh na Scania.
Lakini nadhani kwa sasa hazifanyi kazi hiyo tena.
Mkuu na mimi nimetoka kuwataja hawa baadhi, wale wahindi wa Khatar Singh & Hari Singh walitupigia kazi moja quality ya kimataifa kabisa.

Sijui kama kile kiwanda kipo bado.
 
Mkuu na mimi nimetoka kuwataja hawa baadhi, wale wahindi wa Khatar Singh & Hari Singh walitupigia kazi moja quality ya kimataifa kabisa.

Sijui kama kile kiwanda kipo bado.
Hawa walipaswa kulindwa
 
1. Kama mnavyojua sekta ya USAFIRISHAJI imekua kwa kiasi kikubwa. Lakini la kusikitisha mabasi yaliyo Mengi huagizwa China, Brazil na Kenya.

2. Je haiwezekani kuwalazimisha wenye viwanda hivyo kujenga "Assembly plant" nchini kuongeza ajira, Kodi na ukuzaji/urithishaji teknolojia/maarifa kwa wazawa?

NB: waagizaji nao walazimishwe kununua basi nchini Tu.

**SIDO, NIT, UDSM (CoET), DIT amkeni
Sidhani kama kuna manufacturer wa nje anayeweza KULAZIMISHWA kuja kutengenezea chochote hapa nchini.
 
Shida ni kodi kubwa na hatuna Sera nzuri kwenye uwekezaji wa viwanda maana makampuni mengi ya nje wangekuja wenyewe maana wafanyakazi wapo ni wao na bidhaa zao..
 
Changamoto kubwa ni fikra tegemezi kuanzia kwa wananchi hadi viongozi.
Kwa kukua kwa teknolojia ya mawasiliano ilivyo sasa, tunatakiwa kushawisi watu wetu waige na kutengeneza vitu vingi sana badala ya kuwapa wageni kipaumbele.
Hoja yako ya kuwalazimisha watengenezaji haiwezelani na ni ya hovyo kwa sababu biashara ni huria.
SAHIHI

Hata mazungumzo yanayoendelea katika huu uzi ni jukwaa zuri tu kulishughulikia suala la "Changamoto kubwa iliyo ni fikra tegemezi kuanzia kwa wananchi hadi viongozi".

Ikiwapo NIA THABITI ya kuyabadilisha mambo, NJIA THABITI nayo haikombali na ukweli/uthabiti wa mashauri.

Labda wakati mmoja, humu wanajamii wanawezakudhamiria 'kufanya jambo lao' na likaja kuchipua kwenye nyanja za jamii na uchumi na maendeleo--JF, kama taasisi wameaanza na jukwaa la 'Kushindanisha Mawazo': 'Simulizi za Mabadiliko'...

Bado ipo nafasi zaidi ya 'amsha amsha' ya kifikra na maendeleo ya jamii; labda inahitajika 'itikadi' fasaha ya kuongozea mageuzi ya kijamii na kiuchumi--itikadi ambayo inaweza kutungwa na kufuatishwa na sisi wote tunaotaka kuona mabadiliko na si tu 'kuyasikia' ama kuoteshwa ndoto za kuonekana kama ni jambo gumu/jambo linalosubiri serikali/viongozi/matajiri/wageni wenye mitaji n.k

Humu JF kuna kundi la sisi watu wa makamu ama hata 'Wazee'; tunaoweza kubuni utaratibu wa kuwaunganisha vijana wenye adabu na nidhamu na kuwafadhili shughuli zao kwa maadili na miiko tunayowapangia na kuwataka; kuwajenga kiakili na kuwaongoza hadi pale wanapojengeka na kuimarika kiuwezo na utendaji...

Kuna mambo kwenye jamii yetu kuwaachia vijana bila kuwaaongoza, kusaidiana kuwalea na kuwajenga kiakili ni kama vile tunajihujumu sisi wenyewe. Sisi wenyewe wengi wetu ni 'Wahanga' wa maisha ya kukosa 'Miongozo thabiti' ya maisha--kuishi tukitafuta 'kutoboa kwa kudra za Mwenyezi Mungu'... Jambo hili kuna namna 'siyo jema'; tunaweza kudhamiria utubora kwa kusaidiana kuwajenga vijana wengine wasio na msaada wa kiroho na kiakili...

Humu JF, watoto wadogo, vijana na watu wa makamu wanazungumza kwa 'uhuru' na kumbe ingelikuwa vema sana humu kuwe na nasibu ya watu kufahamika na kuheshimiana kwa rika, busara na nidhamu ya kujiheshimu--kwa wale wanajifahamu kuwa ni watu wazima na basi kudhamiria michango yenye akili na busara.

SASA, siyo lazima kila kitu tuwe ni watu wa 'kuiga mifano'--kwani inatugharimu kipi/lipi sisi watu wa taifa la Tanzania kuwa mfano wenyewe khasa--ikibidi hata kwa Afrika na Dunia nzima?

Tuthubutu jambo--nawahakikishia wakiwemo 'watu wazima timamu'; nidhamu na adabu sahihi ya vijana, maarifa ya kusanifu na kujenga taasisi za kazi na utendaji yatakuwepo hata kupitia humu humu kwenye jukwaa hili la mazungumzo ya Kijamii. Sisi ndiyo waamuzi wa jukwaa hili libaki ni jamvi la soga ama jamvi linasonga mbele kupita soga...

Humu wadau, wamezungumza kuhusu 'fibre glass'--laiti, ingelikuwa kuna 'wazee wa marifaa na nia njema', kwa hili la rasilimali 'faibaglasi' tunaweza kujipanga na kuwaongoza vijana watengeneze karakana ndogondogo za uundaji wa vyombo vya uchukuzi kwa manufaa ya jamii zao; hata kama sisi wenyewe wazee hatujawahi kujishughulisha na faibaglasi moja kwa moja....

View: https://www.youtube.com/watch?v=RihBn0mP9hI&t=10s

Tuna vijana wengi walio ni nguvu kazi, wakiwa ni wakazi wakuishi karibu na maeneo ya mito, mabonde, maziwa na bahari--hawa wakioneshwa ama/na kupewa mbinu za kazi wanaweza kuunda karakana ndogondogo za uundaji wa vyombo vya uchukuzi kama mitumbwi, vijigari, mikokoteni n.k inayotumia faibaglasi na nyenzo zingine za kitekinolojia kwa manufaa yao kiuchumi wa kila siku...

Inatugharibu kuhama kiparadaimu; si lazima tuache suala la ubunifu na utundu kwa vijana "Watuoneshe Maajabu"--tunaweza kuwa chachu ya maarifa, suluhu na miongozo kwa vijana wetu.

Sisi watu wazima na timamu, tunaloshauri la kuwapenda vijana na kuwathamini popote pale walipo pasipo kasumba za 'mtoto wangu/mtoto wa dada yangu'--mtoto wa jamaa yangu na mambo kama haya. Hata kama watoto wetu wenyewe wanatushinda/wametushinda isitufanye kukataa tamaa na vijana wengine walio ni wanajamii wetu na hata kokote kule. Kama tunaacha ubinafsi, kuwapenda na kuwajali vijana wote, basi na sisi kiufundi tunajichagulia fungu la kusameheana, kujisahihisha na kusahihishana makosa yetu. Mtoto niliyemshindwa mimi, mwingine anaweza kumsaidia kadiri hata miye ninawezakuwa ni wa msaada kwa mtoto wa mzazi mwingine aliyemshindwa wakwake wa kumzaa.

Hili si jambo la kuwa kana wanajamii wanafikiria serikali ndiyo daima 'yakutupiwa lawama'; kuna mambo ambayo sisi wanajamii tukipendana na kwenda sawa tunakuwa na 'mamlaka ya kimaadili' kuisema serikali; na yenyewe kwa uadilifu, itafanya tutakavyo kwa haki na wala siyo 'mkate na sarakasi'...

Ikiwa sisi wenyewe hatutumizi wajibu wetu wa kiraia katika upendo--serikali, na utumishi wa umma utaakisi hayo hayo ya sisi kuwa wenye ubinafsi usiyo na tumaini la kweli la maendeleo na ustawi bora wa jamii nzima. Watu wakuacha mambo yabakie 'stori' tu...

Vinavyoelea vimeundwa, lazima tujisuke na kuwa na mipango--mipango midogo kwa mikubwa ili tuyaishi na kuyaendea yale yaliyo ni bora kimaisha. Jitihada zetu kwa kila pumzi na shauri, ni vema ziwe ni nguvu ya kuiishi mikakati ya 'Uhuru' na kuvikomboa vizazi vyetu na adha ya 'Uteja' wa 'Statusi Kwou' iliyomushkeli.

Hmmm​
 
Back
Top Bottom