Viwanda vya kuunda mabasi vilazimishwe kuzalishia mabasi Tanzania

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
7,954
7,858
1. Kama mnavyojua sekta ya USAFIRISHAJI imekua kwa kiasi kikubwa. Lakini la kusikitisha mabasi yaliyo Mengi huagizwa China, Brazil na Kenya.

2. Je haiwezekani kuwalazimisha wenye viwanda hivyo kujenga "Assembly plant" nchini kuongeza ajira, Kodi na ukuzaji/urithishaji teknolojia/maarifa kwa wazawa?

NB: waagizaji nao walazimishwe kununua basi nchini Tu.

**SIDO, NIT, UDSM (CoET), DIT amkeni.
Ikishindikana viwanda vya mabasi tuwekeze kwenye viwanda vya Kondomu!
 
Siku nikiwa Rais wa hii nchi kila bidhaa inayoagizwa kwa wingi nje ya nchi itategenezewa Tanzania. Kama wawekezaji watakataa kuuza kuleta teknolojia nitajenga kiwanda kimoja kila baada ya miezi mitatu.

Ninaamini 100% Africa hatuendelei sio kwasababu ya ujinga tuliolishwa miaka mingi shida ni hatuzalishi tunavyotumia. The largest importer ni USA, China , Germany.......na ndizo nchi tajiri duniani
 
1. Kama mnavyojua sekta ya USAFIRISHAJI imekua kwa kiasi kikubwa. Lakini la kusikitisha mabasi yaliyo Mengi huagizwa China na Kenya.

2. Je haiwezekani kuwalazimisha wenye viwanda hivyo kujenga "Assembly plant" nchini kuongeza ajira, Kodi na ukuzaji/urithishaji teknolojia/maarifa kwa wazawa?

**SIDO, NIT, UDSM (CoET), DIT amkeni
Umeongea jambo la maana sana.

Viwanda vya kuunda mabasi vikiwepo kila mkoa vitazalisha mabasi ya aina tofauti na kuondokana na vibajaji na pikipiki pamoja na vibasi vidogo.

Mabasi yakiwepo yataleta pia usafi mijini na kuwepo kwa clean cities.

Pia viwanda hivyo vitakuza ajira na kuboresha uvumbuzi na ubunifu.

Hapo utakuwa umetatua tatizo la ajira, usafi mijini, mipango safi ya miji kwa maaa ya vituo maalum vya mabasi na pia viwanda hivyo vitazalisha viwanda vingine vidogo vya vipuri na vifaa na vile vya vitu kama viti vya kwenye mabasi.

Haya yataletwa tu na watu wakiwa na utashi.

Big up sana
 
Siku nikiwa Rais wa hii nchi kila bidhaa inayoagizwa kwa wingi nje ya nchi itategenezewa Tanzania. Kama wawekezaji watakataa kuuza kuleta teknolojia nitajenga kiwanda kimoja kila baada ya miezi mitatu.

Ninaamini 100% Africa hatuendelei sio kwasababu ya ujinga tuliolishwa miaka mingi shida ni hatuzalishi tunavyotumia. The largest importer ni USA, China , Germany.......na ndizo nchi tajiri duniani
Mkuu, its nice to see you back, Merry Christmas.
 
Zamani Mabasi yalikuwa yakitengenezwa humu humu Nchini, baadae katika miaka 90 ndio tukaanza kuona Mabasi ya Kenya, tena Mkoa wa Tanga ndio waanzilishi.

Tanroads walipoanzisha Mizani za Barabarani yale Mabasi yetu na ya Kenya yakawa ni mazito, ndio Mchina na Brasil wakaingia sokoni na Double axle na body za Fiberglass.

Sasa hivi Mchina Brasil ndio wanaongoza
 
Siku nikiwa Rais wa hii nchi kila bidhaa inayoagizwa kwa wingi nje ya nchi itategenezewa Tanzania. Kama wawekezaji watakataa kuuza kuleta teknolojia nitajenga kiwanda kimoja kila baada ya miezi mitatu.

Ninaamini 100% Africa hatuendelei sio kwasababu ya ujinga tuliolishwa miaka mingi shida ni hatuzalishi tunavyotumia. The largest importer ni USA, China , Germany.......na ndizo nchi tajiri duniani
Hizo nchi ulozitaja zalinda sana viwanda vyao na zote zina chambers of commerce ambazo hatuwezi kuzilinganisha na Dar-es-Salaam Chambers of commerce.

Pili, kwa kuwa dunia imebadilika sana yabidi kuwa makini ni aina ipi ya kiwanda wataka kuwa nacho nchini mwako ila kwa viwanda vyote vya kuzalisha basic needs ni lazima viwe protected.

Tatu, teknolojia ni kukazania vyuoni kuhakikisha wanafunzi bora wanapelekwa nje ili wakirudi wapewe majukumu ya kuendeleza nchi kimkakati.
 
Zamani Mabasi yalikuwa yakitengezwa humu humu Nchini, baadae katika miaka 90 ndio tukaanza kuona Mabasi ya Kenya, tena Mkoa wa Tanga ndio waanzilishi.

Tanroads walipoanzisha Mizani za Barabarani yale Mabasi yetu na ya Kenya yakawa ni mazito, ndio Mchina na Brasil wakaingia sokoni na Double axle na body za Fiberglass.

Sasa hivi Mchina Brasil ndio anaongoza
Pia bei, mchina anauza bei ndogo
 
Back
Top Bottom