Kidaya
Senior Member
- Dec 20, 2011
- 108
- 95
Sekta ya kilimo nchini Tanzania ni nguzo kuu ya uchumi wa taifa, ikiwa ni chanzo kikuu cha ajira. Kwa mujibu wa taarifa ya hotuba ya bajeti ya wizara ya kilimo 2023/2024, zaidi ya watanzania milioni 40 (65.6%) wanategemea moja kwa moja sekta hii kwa ajira. Kilimo pia kina jukumu muhimu katika kukidhi mahitaji ya chakula na kuhakikisha usalama wa chakula kitaifa. Hata hivyo, sekta hii muhimu nchini inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinazuia ukuaji wake na uwezo wake wa kuwapunguzia wakulima umaskini. Changamoto hizi ni tija na uzalishaji mdogo, matumizi madogo ya pembejeo za kilimo kama mbegu, mbolea, viuatilifu na zana za kilimo, upotevu wa mazao kabla na baada ya mavuno, huduma hafifu za ugani katika kilimo, ushiriki mdogo wa vijana na wanawake katika kilimo, na ukosefu wa masoko na ugharamiaji wa sekta ya kilimo.
Vituo vya kilimo vya wilaya (District Agricultural Support Centers) ni vituo vinavyokuwa katika ngazi ya wilaya kwa ajili ya kutoa msaada wa kilimo na huduma kwa wakulima ili kuboresha uzalishaji, kuhamasisha ushiriki wa kilimo biashara, na kuboresha usalama wa chakula. Vituo hivi vitatoa msaada kwa wakulima ambao tayari wanashiriki shughuli za kilimo kwakuwa wana mtaji wa ujuzi wa wawali kuhsu kilimo, maeneo na mashamba, mbegu, baadhi ya vitendea kazi na makazi hivyo kuwa rahisi kuwasaidia katika kutatua changamoto zinazowakwamisha kwa gharama ndogo tofauti na kuanza na wakulima wapya. Mfano, kuna mkulima changamoto yake ni kujua tuu kwenye udongo alionao atumie mbolea gani kwa zao gani linalomfaa zaidi, kuna mkulima changamoto yake ni utunzaji wa mazao baada ya kuvuna, kumsaidia mkulima huyu kutatua changamoto yake hakika itakuwa hatua kubwa kwake kufikia mafanikio.

Utatuzi wa Changamoto za Kilimo
Vituo hivi vitasaidia kutatua changamoto za kilimo kwa;
• Kuwa eneo la kusambaza mbinu za kisasa na bunifu za kilimo, kutoa mafunzo, na kutoa msaada wa kiufundi kwa wakulima ili kuboresha uzalishaji.
• Kupunguza hasara baada ya mavuno kwa kuwafundisha wakulima mbinu sahihi za kuhifadhi na kusindika mazao. Pia kuwaunganisha wakulima na viwanda vya usindikaji wa mazao ya kilimo ili kupunguza hasara na kuongeza thamani kwa mazao ya kilimo.
• Kuwarahisishia wakulima upatikanaji wa huduma za upimaji udongo, pembejeo kama mbolea, viuatilifu, mbegu, na vifaa vya kilimo kupitia mipango ya ununuzi na usambazaji wa pamoja.
• Kuhamasisha kilimo cha umwagiliaji kwa kufundisha na kusaidia upatikanaji wa miundombinu ya umwagiliaji kwa kutumia rasilimali za maji zinazopatikana kwenye maeneo ya wakulima.
• Kusaidia upatikanaji wa huduma za ugani kwa kutoa maonesho ya shambani na mafunzo ili kuboresha maarifa na ujuzi wa wakulima, hatimaye kuboresha shughuli za kilimo na uzalishaji.
• Kutoa mafunzo ya kuwawezesha na kuwahamasisha vijana na wanawake kushiriki kikamilifu katika shughuli za kilimo na ujasiriamali, kwa kufanya mafunzo ya kilimo kwenye maeneo yanapopatikana makundi hayo (outreach) kama mashuleni, vyuoni na vikundi vya vijana na wanawake, hivyo kukuza maendeleo ya kilimo jumuishi.
• Kuwezesha ufikiwaji wa masoko, kutoa taarifa za masoko, na kutoa mafunzo ya uelewa wa masuala ya kifedha kwa wakulima ili kuwawezesha kufikia masoko na fursa za kifedha hivyo kuboresha mapato na maisha ya wakulima.

Mahitaji ya Vituo vya Kilimo
Ili kutoa msaada wa kilimo kwa wakulima kwa ufanisi, vituo hivi vinahitaji;
• Mashamba ya maonesho: Mamlaka za wilaya kutoa hekta angalau heka 10 za ardhi zitakazotumika kama mashamba ya maonesho na malisho ya mifugo.
• Vituo vya mafunzo: Vituo vinaweza kutumia kumbi au madarasa ya shule zilizopo katika maeneo ya wakulima kwa ajili ya mafunzo na maonesho kwa wakulima.
• Vitalu vya miche: Kwa ajili ya kuzalishia miche ya bora za mazao inayofaa kwa eneo walipo wakulima.
• Mashine za kilimo: Matrekta, plau, mashine za kupandia mbegu, mashine za kuvunia, na mifumo ya umwagiliaji zitakodishwa au kuazimwa kutoka mamlaka za serikali kwa ajili ya matumizi ya wakulima na kwa maonesho.
• Maabara za kupima udongo na maji: Kuwa na chumba chenye vifaa vya kupimia rutuba ya udongo, viwango vya virutubisho, ubora wa maji n.k.
• Mabanda ya mifugo: Mabanda na miundombinu ya ufugaji kwa ajili ya uzalishaji, na usimamizi wa mifugo, na huduma za chanjo ili kuwafundishia wakulima.
• Vifaa vya usafiri: Kuwa na bajaji za mizigo kwa ajili ya kwa kusafirisha wafanyakazi wa mradi, vifaa vya mafunzo, na kusambaza pembejeo za kilimo, pamoja na kukusanya sampuli za maabara.
• Eneo la Utawala: Kukodisha nyumba itakayotumika kama ofisi itakayokuwa na teknolojia kwa ajili ya usimamizi wa data, mawasiliano, na ushirikiano na wadau.
• Wafanyakazi wa Mradi: Ili kutekeleza mradi kwa ufanisi, vijana 10 wenye kujituma wataajiriwa kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na utaalamu unaohitajika. Wataalam kama meneja wa mradi, mtaalamu wa ufuatiliaji na tathmini, meneja wa fedha, mtaalamu wa kilimo, daktari wa wanyama, mtaalamu wa maabara, afisa wa mawasiliano na wafanyakazi wa kazi za mikono, watafanya kazi kwa kila kituo. Wataalam hawa ambao tayari wapo katika ofisi za Mkuu wa Wilaya na au Ofisi za Halmashauri watakuwa ndio wafanyakazi wataalam wa vituo hivi hivyo ili kupunguza gharama ya kuajiri wataalam wengine ambao watahitaji mishahara na makazi.

Shughuli za Kuzalisha Mapato
Vituo vitakuwa na shughuli zifuatazo za kuzalisha mapato ili kugharamia gharama mbalimbali za uendeshaji na kufanya vituo hivi kuwa endelevu;
• Kutoa huduma za malipo kama vile upimaji wa udongo na maji, huduma za kutotolesha mayai, na kukodisha vifaa kwa wakulima
• Kuuza mazao ya kilimo yanayozalishwa katika shamba la maonesho kama vile mazao ya mimea na wanyama, miche, vifaranga na wanyama.
• Kutafuta ushirikiano na mashirika ya serikali, NGOs, mashirika ya maendeleo, taasisi za utafiti, na sekta binafsi ili kupata ufadhili wa miradi maalum, mafunzo, shughuli za utafiti na kupanua wigo wa huduma.
Wakulima wetu wengi wanalima kilimo cha kujikimu na cha mazoea kisichojali udongo wa eneo lake unafaa kwa kilimo cha zao gani hasa, changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa, na mwenendo wa bei za bidhaa ya kilimo masokoni hali inayochangia kupunguza tija katika kilimo.
Kuwa na vituo vya kilimo vya wilaya kutasogeza elimu, ujuzi na huduma nyingi za kilimo kwa wakulima hali itakayowasaidia kutatua changamoto wanazokutana nazo kwa ufanisi, na hatimae kuongeza uzalishaji na mafanikio ya sekta ya kilimo katika kutoa ajira zaidi na kuchangia pato la Taifa.