Vita ya Kagera na Uganda haikuitwa vita ya Tanzania na Uganda?

Kwanini Vita ya Kagera na Uganda haikuitwa Vita ya Tanzania na Uganda..?
Kwa sababu hakujawahi kuwepo na vita ya Kagera na Uganda.

Vita ambayo ilikuwepo, ni kati Ya Tanzania na Uganda, baada ya Serikali ya Idd Amini kutaka kuimega Kagera. Kwa Muktadha wa kivita na kitanzania, vita hiyo pia inahafamika kama "vita ya Kagera" na sio "vita ya Kagera na Uganda"
 
Kimataifa ikiwamo katika maandishi inaitwa pia vita ya Tanzania na Uganda.

Ila pia inaitwa vita ya Kagera kwa sababu ugomvi ukianza kugombania sehemu inaitwa "The Kagera Salient", kisehemu cha ardhi ya Tanzania kilicho kaskazini ya mto Kagera. Idi Amin alitaka kuufanya mto Kagera kuwa ndiyo mpaka wa Tanzania na Uganda hata pale mpaka ulipokuwa kaskazini ya mto Kagera.
 
Chanzo cha vita ni Nyerere kulidisha rafiki yake obote, watanzania tulilipia gharama kubwa
Mara nyingi wanaoamini hivi ni wale waliochukulia vita kwa mtazamo wa kidini. Kwamba Nyerere alikuwa anapmbana na dini ya kiongozi wa Uganda. Unfortunately, hizi stories ni za vijiweni japo zimesambaa sana kwa baadhi ya watu.
 
Muache kuingiza udini eti kwa sababu Iddi alikuwa ni muislam na ndio maana baba la uislam Afrika lilijitolea kumsaidia ndugu yake huyo wa dini majeshi yake yakaishia kutekwa na mashujaa wa Tanzania kisha mateka hao Nyerere akawarudisha kwao kiroho safi bila kuwadhuru
 
Mara nyingi wanaoamini hivi ni wale waliochukulia vita kwa mtazamo wa kidini. Kwamba Nyerere alikuwa anapmbana na dini ya kiongozi wa Uganda. Unfortunately, hizi stories ni za vijiweni japo zimesambaa sana kwa baadhi ya watu.
Chanzo halisi cha vita ya Kagera ni Mwalimu Nyerere kuleta uswahiba kwenye masuala ya kidiplomasia na kiulinzi. Milton Obote alipopinduliwa, Nyerere akampa hifadhi Tanzania. Na hapa Obote alikuja na wafuasi wake na wengine waliponyanyaswa kidogo wakaja kuunga juhudi huku, si ni suala la kuvuka mpaka tu.

Museveni mwenyewe alikimbilia Tanzania na mwanae Muhoozi huyu msumbufu alizaliwa huku. Museveni kapewa mafunzo mengine na mipango na serikali ya Nyerere, pale Tanga walijichimbia. Tangu Iddi Amin anafanya mapinduzi maadui zake wanafugwa Tanzania na wanatokea huku wakienda kufanya majaribio ya kumuua au kumpindua wakishindwa wanakimbilia Tanzania.
 
Bahati nzuri, vita inatokea mimi nilikuwa mkubwa tayari.
Ulichoandika kina ukweli kidogo na hisia nyingi. Na hisia zilienezwa na kukuzwa na wasiompenda Nyerere ama kwa itikadi zake za kisiasa au kwa dini yake.
Ukweli ni kuwa Idd Amini alipanga kuimega Kagera na kuna wakati alikuwa anaongelea kuchukua hadi Mwanza. Na wakati huo yeye hakuwai kusema anavamia Tanzania kwa sababu ya Obote kutunzwa kama mkimbizi. Na hata internal strife ndani ya serikali yake, haikuanzishwa na tukio la Obote kuja Tanzania, bali na general dissatisfaction ya watu wake. Hii ina maana kuwa vikundi vya kumpinga vilikuwepo tu na vingekuwepo hata kama Obote angeenda ukimbizini kwenye nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom