Viongozi wa Somalia wakubaliana kuhusu Uchaguzi wa Bunge

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,569
9,430
Viongozi wa kisiasa wa Somalia Jumapili wamesema kwamba wamefikia makubaliano ya kukamilisha uchaguzi wa bunge kufikia Februari 25 baada ya kucheleshwa kwa muda na kutishia udhabiti wa taifa hilo lililotatizika kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, hatua hiyo imefikiwa baada ya mashauriano ya siku kadhaa yakiongozwa na waziri Mkuu Hussein Roble na kuhudhuriwa na viongozi wa majimbo.

Taarifa iliyotolewa baada ya vikao hivyo imesema kwamba uchaguzi unaoendelea wa bunge la chini utafanyika kati ya Januari 15 na Februari 25 mwaka huu. Roble na rais Mohamed Abdullahi Mohamed au kwa jina lingine Farmajo, wamekuwa wakijibizana kutokana na kucheleweshwa kwa zoezi hilo, hali iliyozua wasiwasi wa kutokea kwa ghasia nchini humo.

Mwezi uliopita Farmajo alimsimamisha kazi Roble ingawa yeye mwenyewe ndiye aliyemteua kuwa waziri mkuu hapo Septemba 2020. Jumuiya ya kimataifa ilikuwa imeelezea wasiwasi wake kutokana na migogoro ya kisiasa nchini humo wakati kukiwa na changamoto ya makundi ya kiislamu kama vile Al Shabaab, miongoni mwa mengine.
 
Back
Top Bottom