benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,186
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Kawambwa, amewasihi vijana wasikubali kutumika na baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa au viongozi wa dini ambao wanakusudia kuharibu amani na utulivu uliopo nchini.
Sheikh Kawambwa alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza a waandishi wa habari kuhusu mwenendo unaoendelea wa kuwepo viashiria vya kutaka kuvunjaamani ya nchi.
"Kamati ya amani na viongozi wa dini madhehebu mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam, tutaendelea kulinda amani ya nchi na tunalaani matamshi yanayotaka kuleta machafuko katika chi vetu hasa vijana wasikubali kamwe kutumiwa na wanasiasa au viongozi wa dini mbalimbali," alisisitiza.
Pia, Sheikh Kawambwa alisema kamati yake ya amani wameipokea kauli ilitolewa hivi karibuni na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camilius Wambura, kuwaonya baadhi ya watu wanaotaka kuharibu amani kuacha mara moja.
Alisema IGP aliwaomba Watanzania kuwa watulivu kwani wasikubali kutumiwa na baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema ya amani nchini kwa kuwashawishi kufanya maandamano.
"Vyombo vya ulinzi na usalama wasisite kufanya kazi ya kuimalisha ulinzi wa nchi yetu na kila Mtanzania anatakiwa kulinda amani iliyoko, endapo amani ya chi yetu ikivurugika hakuna hatakayesalia.
Aliongeza kuwa: "Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anadumisha amani na mshikamano ambao ulioasisiwa na wazee wetu kwani sisi ni jahazi moja linaloitwa Watanzania"