Anatakiwa kuwa Kiungo kati ya Wabunge wa Chama Tawala na wa Upinzani au?Anakuwa kiungo katika mzingira yapi?Ameongoza migomo ipi Bungeni?Au anaamua tu peke yake?Mbona katika hili na Zito Kabwe yupo?MBOWE ameshindwa kabisa kuwa KIONGOZI WA UPINZANI na badala yake amekuwa ni KIONGOZI wa MIGOMO BUNGENI. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani anatakiwa awe kiungo kati ya Wabunge wa chama tawala na wale wa Upinzani katika kuisimamia Serikali.
Ushasema yeye ni KUB?Kwani KUB maana ake nini?Na hao wabunge ulitaka wamsikilize nani sasa?Mbowe ndio Kiongozi wao au wewe ulitaka wamsikilize Spika?Kauli za MBOWE zimekuwa ni kauli za Mwisho kwa Wabunge wa Upinzani wachukue hatua gani. Kuanzia Bunge la Katiba, sakata la TBC1 kuonesha vikao vya Bunge na hata hili la UDOM , wabunge wamefuata kauli za Mbowe, hii ni hatari sana. Siku Mbowe akisema Wabunge wote wampige kiongozi wa Bunge aliyeko meza ya Spika watafanya hivyo
Taja msimamo mmoja wa KUB usio na tija na sio kuropoka tu hapa jamavini, msimamo upi ambao hauna tija?Misimamo isiyo na tija ya KUB ndiyo inayopelekea Serikali isisimamiwe vyema.
Akili nyingine bwana?sasa wanang'ang'aniaje na naibu spika keshakataa hoja?Ulitaka wampindue Spika?Binafsi nilitegemea Wabunge wang'ang'anie kuomba suala la Wanafunzi wa UDOM lijadiliwe kama suala la dharura kuliko kukimbia na kutangaza kususia vikao, haya wamekimbia na watasusia vikao, nini mchango wao katika hatima ya wanafunzo hao?
Umejitahidi kupoteza muda wako na kuandika but hoja zako zote hazina mashiko ebu kajipange upya uje na jambo la maana