Pre GE2025 Vijana wahamasishwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha Kupiga Kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Sep 4, 2024
166
180
Wakati Tume ya Huru ya Uchaguzi nchini (INEC) ikiendelea na uandikishaji wa daftari la kudumu la wapigakura katika mikoa mbalimbali, vijana wametakiwa kuwa mstari wa mbele kujiandikisha ili wapate haki hiyo ya msingi.

1741875642162.jpeg
Hayo yamesemwa leo Alhamisi Machi 13, 2025 na Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa Mkoa wa Kagera, Leodger Kachebonaho katika hafla ya kukabidhi Sh3.85 milioni kwa ajili ya ununuzi wa kiwanja kitakachojengwa nyumba ya mtendaji wa jumuiya hiyo wilayani Kyerwa.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama chetu, lakini pia nitoe rai kwa vijana kuhakikisha tunavyokwenda katika uchaguzi tuwe tumejiandikisha kwenye daftari la kudumu pia tujitokeze kwa wingi kupiga kura, kwa sababu ni miongoni mwa haki zetu na itasaidia katika kuleta maendeleo ya nchi," amesema Kachebonaho
 
Walijiandikisha wengi kwa ajili ya namba za simu, Sasa hivi hawana time na kitambilisho Cha mpga kura!
 
Na wakitoka hapo waende kusoma VETA.Mhe: majaliwa kasema
KAZI ni kipimo cha utu
 
Wakati Tume ya Huru ya Uchaguzi nchini (INEC) ikiendelea na uandikishaji wa daftari la kudumu la wapigakura katika mikoa mbalimbali, vijana wametakiwa kuwa mstari wa mbele kujiandikisha ili wapate haki hiyo ya msingi.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Machi 13, 2025 na Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa Mkoa wa Kagera, Leodger Kachebonaho katika hafla ya kukabidhi Sh3.85 milioni kwa ajili ya ununuzi wa kiwanja kitakachojengwa nyumba ya mtendaji wa jumuiya hiyo wilayani Kyerwa.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama chetu, lakini pia nitoe rai kwa vijana kuhakikisha tunavyokwenda katika uchaguzi tuwe tumejiandikisha kwenye daftari la kudumu pia tujitokeze kwa wingi kupiga kura, kwa sababu ni miongoni mwa haki zetu na itasaidia katika kuleta maendeleo ya nchi," amesema Kachebonaho
Ili iweje!?
 
Wanataka tuwapigie kura waendelee kula, sisi tukitaka tupigiwe kura pia hatupati nafasi. Imagine kupiga kura hakuna masharti ya kuwa kwenye chama cha siasa, ila kupigiwa kura lazima uwe kwenye chama cha siasi. Watupe haki hata sisi ambao hatuna party affiliations tuweze kuchagua na kuchaguliwa pia. Private Candidates is a must.
 
Back
Top Bottom