Half american
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 34,693
- 89,457
Habari zenu wakuu.
Tarehe 02/04/2024 kulikuwa na tukio la kuwasha mwenge wa uhuru mkoani kilimanjaro na mgeni rasmi alikuwa ni waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa.
Kama ilivyo kawaida kwa shughuli yeyote ile lazima yawepo maandalizi mazuri ili kuweza kufanikisha kwa ufanisi mkubwa.
Moja ya maandalizi ni pamoja na mafunzo ya halaiki kwa vijana waliochaguliwa kutoka shule mbalimbali ndani ya mkoa/wilaya husika. Zoezi la mafunzo kwa waliochaguliwa lilidumu kwa zaidi ya miezi miwili.
Je hawa vijana wa halaiki wananufaika na nini kitakachowatofautisha na vijana ambao hawakuchaguliwa baada ya shughuli ya kiserikali kufanyika? Kuna vyeti vitakavyowapa utambulisho kuwa walishiriki mafunzo hayo?
Kama hakuna nashauri kuwe na utaratibu huo wa kuwazawadia hata vyeti maana mpaka sasa naona vijana wameambulia kupewa track suti, raba na miamvuli. Ukizingatia walilazimika kusoma nusu siku na wakati mwingine kutokuingia darasani kabisa ili kushiriki mafunzo hayo ya halaiki.
Mheshimiwa Dkt. Gwajima D wizara yako inahusika na watoto naomba kama unaweza kutoa muongozo/maelekezo yoyote kwenye hili utusaidie. Tunaomba ufikishe na haya mapendekezo yetu kwa faida ya watoto. Ahsante.
NAWASILISHA....