Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati

Kariakoo 90 % biashara inatembea Kwa uaminifu , ili uuze mzigo kariakoo lazima uhusishe watu wengi sana na sharing ni kubwa , mawinga ndo catalyst ya biashara kariakoo Ila nguzo Yao kuu ni uaminifu , sasa njoo na tamaa zako uone , unakamuliwa kinyesi live live
 
Wengi wanaochangia wamemung'unya sana maneno kiasi asiyejua kinachoendelea hapati clue ya yanayotokea,vijana wanaopotea Kariakoo ni upande wa vitu kama simu laptop na tv na vitu mfanano wa hivyo pamoja na spare za magari.

Mimi nafanya biashara ya spare za magari,nyuma miaka saba nikiuza used kwanza Kariakoo kisha Ilala kule Lindi St so nikizungumza kwa upande huo nawajua vijana pamoja na watu wazima 11 wamepotea toka 2022 hadi leo hawajulikani walipo wa mwisho kwa upande huu walipotea wawili kwa pamoja mwaka jana mwezi wa tano na wote miaka ya nyuma wakati nafanya used walikuwa wanajihusisha sana na kununua vitu vilovyokuwa vikiibiwa kwenye magari ya watu wenyewe wakiita ”full",yaani gari inavunjwa kioo wanatoa lock wanachukua kuanzia dashboard show p/window switch radio side mirrors headrest nje wanang’oa taa zote bumpers nyuma na mbele kama mmiliki alisahau chochote cha thamani wanabeba so hawa jamaa walikuwa wanakaa pale mnada wa spare ulioungua moto nyuma ya Big Born p/station.

Jamaa walikuwa wanakula na askari wa Msimbazi na Central wakati fulani Mambosasa akiwa mkuu wa police Dar akalivalia njuga kwa kuwapa kitu kama offer (maana walikuwa wanajulikana kote police Msimbazi Stakishari Central Mabatini kwamba ndiyo wanaodhamini biashara hiyo hata picha zao zilibandikwa kutani) kwamba kuanzia pale hawana kesi ila wakiri kuacha mara moja mchezo huo kwani option iliyokuwa ifanyike baada ya kudhihirika wanaendelea na kazi hiyo ni kupotezwa moja kwa moja na kwamba jeshi la polisi halitakuwa na muda wa kwenda kutoa maelezo mahakamani,kilichoendelea wanakijua wenyewe baadae walipovunja hicho kiapo ndiyo wakapotea.

Baada ya hii ambush ndiyo matokeo tunayoyaona sasa wizi ule umepungua kama siyo kuisha kabisa nadhani hata Agrey baada ya wale watano kupotezwa kuna mabadiliko.
 
Nimeshaona post kadhaa siku za nyuma vijana wa Kariakoo kupotea wakati nipo kwenye daladala ilibidi nimuulize jamaa mmoja kipindi cha nyuma kwanini vijana wa Kariakoo wanapotea sana, akasema Kariakoo kuna mambo mengi…aliishia hapo…

Ila kuna neno alisema kuna mchezo wa mali zinaibiwa mbali unapewa uuze, kuna mali kauli, cha msingi alikua anaongea mambo mengi.

Kama pia mnakumbuka wale vijana waliopotea wakati wa sherehe za eid wote ni vijana wa Kariakoo
Chai
 
Hivi ishu za kutekana mda mwingine nyuma ya pazia hata serikali haijui kitu , kuna watu mafia sana hapa mjini ukifanya utapeli utajuta .
Kuna baadhi ya kesi huwa na mkono wa serikali japo wahusika huwa ni wale toppers wa vitengo fulani ili kujisafisha wasionekane hawafanyi kazi,udhaifu wa sheria au kuwa na adhabu ndogo huwapa mtihani polisi maana mtu anakamatwa leo ameiba akifika mahakamani mahakama inamuona hana hatia anaachiwa huru akirudi mtaani anaendelea kuiba so mazingira kama haya hukiweka cheo cha mtu mashakani that's why kamati ya siri huingia kazini.

Mjini kuna mambo mengi but tukiangalia mfano wale wanaopotea zaidi ya watatu kwa wakati mmoja na wanapiga mishe moja inayojulikana kwamba sometimes kuna ujanja ujanja hufanyika yumkini inawezekana wote wamemdhulumu mtu mmoja?au wote wametembea na wake za watu then kama siyo kwanini wapotee siku moja muda mmoja kwa kuchukuliwa pamoja?
 
Back
Top Bottom