Vijana jifunzeni kwa hawa wazee wenu wanao sota huko kwenye majiji na mijini huku wakijificha kwenye majuto makubwa ya kivuli cha wapambanaji

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
2,523
7,340
Ndugu zangu salaam

Enyi vijana wa kiume na kike jifunzeni kwenye makosa ya hawa wazee wanao bebeshwa vitu vizito huku mijini na kwenye majiji kwa malipo kiduchu yaliyo ambatana na dharau na matusi kedekede nao walikua vijana kama nyie

Vijana ili muwe na maisha mazuri uzeeni lazima uishi sasa . Maisha yako kijana wa kiume na wakike tambua ni sasa haijalishi umesoma au haujasoma kumbuka uzeeni ni fainali. Kama hutaki kuja kutumikishwa na watoto wako uzeeni pambana sasa

Vijana na waambieni ,Huu ni ukweli mchungu usiopingika kamwe japo ulilainishwa na kupakwa rangi kwa misemo isiyo na tija enzi zile ikiwemo

  • Vijana ni Taifa la kesho
  • Mvumilivu hula mbivu
  • Haraka haraka haina baraka
  • Simba mwenda pole ndiye mla nyama
  • Kupanga ni kuchagua

Ukweli ni kwamba ;-

* Vijana siyo Taifa la kesho. Kesho yako inajengwa leo na siyo usubirie kesho ifike ndiyo uanze kupambana. VIJANA NI TAIFA LA LEO TAIFA LA KESHO LINA VIJANA WENGINE WATAKAO KUA NA NGUVU KUSHINDA WEWE ULIYE ZEEKA , UMRI HAURUDI NYUMA UNASONGA MBELE NA NGUVU ZINA PUNGUA

* Hakuna aliye vumilia akala mbivu , zaidi ukijifanya mvumilivu utaishia kuugua, kutengwa, kusononeka na kujawa na msongo wa mawazo kupita kiasi na hatimaye kua masikini, ewe kijana wa kike na kiume epuka kuwa mvumilivu mjinga duniani

* Ukweli ni kwamba haraka haraka ina baraka na siyo kama walivyo tuaminisha kuwa haina baraka, kumbuka iliufanye vitu vingi lazima ufanye haraka, maana kufanya jambo haraka na kwa ushapu ndani ya muda sahihi ni kuokoa muda na kujilimbikizia utajiri wako binafsi na kwa Taifa lako. Vijana changamkieni fursa haraka haraka mkipata nafasi butua haswa huku ukijua wapo vijana wanaokuja kwa kasi nyuma yako.

* Hakuna simba anaye enda pole pole akala nyama hata siku moja. Nyie wenyewe angalieni kwenye uhalisia huko mbugani ili simba ale nyama ni lazima akimbize swala kwa bidii ndiyo amkamate akajilie nyama. Tofauti na hapo akileta mwendo wa pole atakufa njaa hakika na waambieni na kwenye maisha ndiyo ilivyo.

* Kupanga ni kuchagua, ukweli ni kwamba kupanga ni kuchagua ila kuchagua sio kupanga. Maana siyo kila anaye chagua amepanga

Ndugu zangu ukizunguka mitaani, mijini na vijijini utakuta asilimia 90 (90%) ya vijana hawaeleweki na wengi wao wameishia kwenye;-

1: Kukata tamaa huku wakifarijiwa na maombi yanayo ombwa na mitume na manabii kua ipo siku watatusua
2:Ulevi wa pombe kali , uvutaji bangi na sigara kupita kiasi
3: Stress za mapenzi na ngono uzembe, huku wakikimbizana kutafuta wanawake pisi kali na wenye mater-co makubwa ili wawaringishie wenzao
4: ushabiki wa michezo mbali mbali ikiwemo na kubet ili kukidhi mahitaji yao leo hii utakuta magenge kwa magenge ya vijana wamejaa badala ya kufanya kazi kwa bidii wanajadili mpira na maisha ya wasanii wakubwa siku nzima vijiweni
5: Uchawa, vijana wengi wa kiume wamekua machawa kiasi cha kushikwa makalio ili wapate japo mlo wa siku
6: Kukaa kwenye vijiwe na kupiga umbea siku nzima bila kujali watakula nini
7: Kurundikana kwenye magheto, magenge, kona za mito, vilipo vijiwe vya kushabikia mipira ( michezo mbali mbali) ,mabonde na vichochoro vilivyo jificha huko mitaani

8: Na vingine vinavyo fanana na hivyo..

Salaam kwa vijana wote..

**Ndugu zangu vijana mkumbuke kuwa hawa wazee tunaowaona huku mitaani wanatishwa mizigo mizito na mabebari kushinda nguvu zao walikua vijana kama nyie

**Hawa wazee waliochangamana na vijana kwenye vijiwe vya bodaboda na bajaji huku wakishindana na vijana kusaka note siyo kwamba wanapenda wanajutia sana kuchezea ujana wao, wana tamani wangekua vijana tena ili wajipange upya.

** Hawa wazee waliopo huku masokoni wabibi na mababu waliojichokea kwa kubebeshwa vitu vizito huku wanakimbizana kila siku na migambo nao walikua vijana kama nyie ni vile tuu walikosea kuchagua kama nyinyi mnavyokosea sasa.

** Hawa wazee mnao waita kero, kuwa dharau na kuwatusi mno huko kwenye vijiwe vya bajaji na bodaboda. mnao wacheka na kuwauliza walikua wapi enzi zao mpaka waje kuendesha bajaji na bodaboda za mikataba kaeni mkijua ya kua nao walikua vijana kama nyie ni vile tuu walikosea kuchagua na kupanga maisha yao ingali wakiwa na nguvu

** Hawa wazee mnao waona wana ng'ang'ania kusukuma mikokoteni na vijana kwa ujira kiduchu walikua vijana kama nyie

** Ndugu zangu vijana wa kiume na wakike ikumbukwe hawa wazee wasio na uhakika wa kula leo kutokana na maghala yao kukosa vyavyo vya kujipatia chakula walikua vijana kama nyie

** Hawa wazee mnao waona huku mitaani wanasota, waliendekeza mahusiano na ngono kama mnavyofanya nyie sasa hivi, waliendekeza kucheza miziki na ushabiki na fassion za enzi zile. Waliendekeza kuhonga na kuhogwa badala ya kuwekeza kwenye miradi itakayo msaidia uzeeni. Ikumbukwe na wewe utakua hivyo hivyo usipo amua kubadilika

Nb: Hawa wazee (babu na bibi zenu) mno waona wanateseka huku mitaani huku wamebeba mafurushi mazito kwa lengo la kujipatia kipato walikua vijana kama nyie enzi zao, Vijana ishini kwa kurekebisha makosa yao kamwe usitamani na wewe kuja kua kama wao
 
Uzi mzuri ila utakosa wachangiaji
 
Back
Top Bottom