TUKANA UONE
JF-Expert Member
- Jan 3, 2018
- 2,332
- 6,924
Ukihitaji salamu nenda mbeya kwao Lucas mwashambwa ukamsaidie kulima Mtama mkimaliza atakusalimia,kwangu utaambulia chuya Ukawalishe bata!
Sijajua siku hizi vijana wana matatizo gani!
Kwa mujibu wa Cheti changu cha Kuzaliwa(Birth Certificate) ni kwamba,nimezaliwa Tarehe 10/11/1989,Hivyo hivi sasa nina umri wa Miaka 34.
Vijana wengi wa sasa hivi wana Umri wa Miaka 18 - 30,Hivyo watu wengi wenye Umri wangu Vijana wa Kileo wanatuita "Wazee"🤣
Daaaah!,Hii dunia inakimbia sana walahi!
Sasa kuna kipindi nilikuwa naelekea Mkoa wa Arusha,Wilaya ya Karatu na nikaona niegeshe pale Mbezi mwisho karibu na stendi ya Magufuli ili nijipatie Vichwa kadhaa niende navyo uelekeo huo ili nipate kampani ya stori za hapa na pale,kiukweli sikuwatoza kabisa pesa na nilifanya hivyo kama sadaka tu ya Mwisho wa Mwaka kwasababu kipindi kile kulikuwa na shida kubwa ya usafiri kuelekea Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro,Hivyo nilitaka watu wa kubadirishana nao mawazo!.
Kwenye Gari yangu nilikuwa nasikiliza nyimbo za Kikongo za miaka hiyo(Nyimbo zilizonikuza),Nilikuwa nina flash kabisa ya nyimbo hizo!.
Muhimu
Mimi huwa ni mdau wa Muziki wa kikongo kwasababu ni muziki mzuri na huwa unanikumbusha mambo mengi sana,mimi huwa sisikilizi muziki wa Vijana wa kitanzania kwasababu huwa sivutiwi na aina ya miziki wanayofanya vijana wa kibongo!.
Ukikuta nasikiliza miziki ya kibongo basi itakuwa ya wasanii wa zamani lakini siyo wa kizazi kipya!.
Basi bana,pale mbezi wapiga debe wakaniletea watu kadhaa na kumbe wale watu walikuwa wa familia moja ikiyokuwa inaelekea Kilimanajaro maeneo ya Boma ng'ombe.
Wakati tukiwa njiani maeneo ya maili moja nikiendelea kula ngoma zangu za Kikongo ninazo zi-Admire, kuna dogo akataka nitoe nyimbo nazosikiliza nimuwekee wimbo uliokuwa unaitwa "Utatoa hutoi".
Nikajaribu kuwelesha dogo lakini nikaona kama kakomaa huku nikiwaangalia wazazi wake kila mmoja yuko bize na simu yake,nikasema "Wewe hunijui"!.
Nikamuuliza yule dogo huo wimbo kaimba msanii gani,dogo akadakia fasta hata kabla sijamaliza kumuuliza ya kwamba kauimba msanii anayejiita Dula Makabila!.
Mimi nikamwambia huo wimbo sina na sidhani kama nitakuwa nao,baada ya kumwambia vile yule dogo nikamtazama kwenye "Rear View Mirror" akamshitua mama yake huku akimnong'oneza jambo fulani!.
Maza mtu naye bila aibu akaaanza kujiongelesha eti nimuwekee wimbo wa Asha Mashauzi unaitwa "Siyo levo yako".
Kwa Upole na Staha nilijaribu kuwaeleza hizo nyimbo walizotaka wao sina kwenye flash yangu nikitegemea Mama na Baba watajiongeza! Kumbe nilikuwa nimebeba kondoo na siyo binadamu!
Baada ya kuona kero zimekuwa za kutosha,tulipofika sehemu inaitwa Lugoba niliwashusha wote watafute usafiri mwingine ambao watabadili nyimbo kadiri wapendavyo!,Mimi huyooooooooo nikaondoka zangu nikawaacha pale!.
Ingawa walitka kuwa wabishi nikawaambia nitawapiga bomba endapo wangeendelea kukatalia kwenye gari yangu!
Hebu fikiria vijana wa kileo wanasikiliza wimbo unaitwa "Chapati" 🤣🤣🤣
Aiseeee!
Ukipewa lifti vumilia hata kama nyimbo zinazopigwa huzipendi,Vinginevyo ni mwendo wa kuwashusha tu!
NB: UKIONA UNAONEWA,NUNUA GARI LAKO!