The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 738
- 1,191
Wasiojua kusoma na kuandika zaidi ya vijana 700 ikiwemo watu wenye umri zaidi ya Miaka 17 wakiwa 85 wasiojua kusoma na kuandika katika kijiji cha Ipazya wameandikishwa katika mfumo rasmi na mfumo usio rasmi (MEMKWA) Wilayani Mbozi Mkoani Songwe kuanzia mwezi Januari na Februari kupitia kampeni ya kumrudisha mtoto shule .
Ophilia Karumuna ni Mkuu wa Ofisi, UNICEF Mbeya amesema lengo ni kutaka watoto wote kurudishwa shuleni ili wapate elimu na kuwataka wazazi kuwapeleka watoto hao hata kama hawana mahitaji ya shule.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya mbozi Edward Lugongo ambaye ni afisa Tarafa ya Vwawa amesema lengo na adhma na serikali ni kuona watoto wanakuwa na uelewa wa kusoma,kuandika na kuhesabu huku akiwataka wazazi kuwapeleka watoto katika kampeni hiyo ilo wapate haki ya msingi ya elimu.