Vifo vya wanafunzi 32: Mh Rais atuma salamu za rambirambi kwa RC Gambo

Afadhali ameanza kuelewa labda nini maana ya matatizo,..!

Maana tungeshangaa anasema, "ajali haijaretwa na SEREKALI,...nilipochaguliza nilisema nitareta ajali..?"
 
Kwani pole ya Rais inasaidia nini? Sometimes acheni mambo yà kijinga hata kwenye matatizo. Hakuna pole yenye thamani zaidi ya nyingine. Ni roho za kishetani tu zinawaongoza.
Kwahiyo lowassa anafanana na magufuli kihadhi?
 
Ushauri tu kwa watanzania utofauti wa itikadi za kisiasa usifike mbali kiasi hicho ktk kipindi hiki ambacho wazazi wenzetu wamepoteza wapendwa Watoto wao ktk ajali huko Rhotia Karatu!!

Kila mmoja ni muhimu kwa mwingine ktk hii Dunia kwa muda wake.

Nikiangalia zile picha jinsi wale vijana waliojitoa kuingia huko korongoni na kila aina ya kifaa kuwatia mauti na hao majerui huku mvua zinanyesha bila kuulizana vyama vyao!!

Hata watalii walisimamisha safari zao na kumsaidia zoezi la ukoaji na kusaidia usafirishaji wa maiti.

Wana JF tusifike huko ktk chuki za kisiasa tuko ktk msiba mkubwa sana kitaifa tuungane kama Taifa moja!!
Ni kweli kabisa tukio la ajali mbaya kama hii halihitaji kugeuzwa ukumbi wa malumbano ya kisiasa. Sote tunapaswa kuungana na kuwaombea marehemu Mwenyezi Mungu awapokee katika ufalme wake na pia kuwafariji majeruhi na wazazi, ndugu, jamaa, na marafiki wa mareheremu Mungu awape nguvu za kuhimili kuondokewa na watoto na ndugu zao ghafla na kwa njia hii ya ajali. Lakini wakati huo huo, tukio kama hili liwe ni 'darasa' - tujiulize maswali na kupata majibu ni kwa vipi ajali za aina hii zinaweza kuepukika. Mimi swali langu la kwanza, ni kama vile hilo basi linaonekana kuwa dogo kiasi cha kubeba abiria zaidi ya 30, tena wanafunzi wa umri mdogo kama hao? Huu ni uvunjivu wa sheria ya usafirishaji wa wanafunzi, kama hiyo sheria tunayo Tz. Kama haipo, basi ndio 'darasa' la kuanza kutafakari ili kuizuia ajali kama hizi katika siku za usoni.
 
Hakuna mtu aliyefurahia na pia hakina mtu anayependa kuona kutowajibika kwa yeyote anayestahili kulichukulia jambo hilo uzito ..na hasa kitaifa!!
 
Back
Top Bottom