SoC03 Vifaa wezeshi vya watu wenye ulemavu wa macho(Vipofu) na masikio(Viziwi)

Stories of Change - 2023 Competition

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
1,039
1,574
UTANGULIZI.
Macho na Masikio ni milango muhimu ya fahamu inayotumika mara nyingi zaidi,Ikitokea ikapoteza uwezo wa kufanya kazi basi inakuwa changamoto kwa muhusika kupata haki zake za msingi kama kusoma,na kuajiriiwa,na kama atasoma basi ni kwa shida sana kutokana na ukosefu ama uchache wawataalamu wa lugha za alama sambamba na ukosefu wa teknoloji wezeshi.

Mimi ninaamini kwamba “Asiye ona lakinii anasikia ataona kwa kusikia,na asiye sikia lakini anaona atasikia kwa kuona” na nimejikita katika falsafa hii kuelezea teknolojia hii.

Ubunifu huu hautahusisha wale wenye matatizo mchanganyiko ya kutoona na kusikia(kiziwi nani kipofu kwa pamoja) kwa kuwa hili ni kundi linalohitaji kujifunza kwa hisia hivyo wanahitaji teknolojia tofauti.

AINA ZA VIFAA.
Kuna vifaa vya aina mbili kulingana na tatizo la muhusika,
1. Kitafsiri janja cha viziwi.
2. Miwani janja ya vipofu.

KITAFSIRI JANJA CHA VIZIWI (DST).

Kitakuwa katika aina mbili,vyote vitafanya kazi zinazofanana ya kutafsiri sauti kuwa katika lugha ya alama na maandishi,vitatofautiana ukubwa tu.
  • Kitafsiri janja cha viziwi katika kusanyiko (MSDT)
  • Kitafsiri janja cha viziwi cha mtu mmoja (ISDT).
Kitafsiri janja cha viziwi katika kusanyiko (MSDT).
Ni kitafsiri ambacho kitatumika kutafsiri sauti kuwa katika lugha ya alama na maandishi au lugha ya alama kuwa katika sauti ama maandishi katika makusanyiko kama darasa,kanisa,misikiti,kumbi za mikutano na makusanyiko mengine.

Muundo onekani wake utakuwa sawa na TV za kawaida zisizo na kisogo,na zitakuwepo katika ukubwa tofauti katika inchi kama ilivyo kwa TV za kawaida.

Kitakuwa na rimoti kwa ajili ya kufanyia mpangilio na kioo chake kitakuwa chakugusa na kuhisi kama ilivyo kwa vifaa janja vingine.

Kitafsiri janja cha viziwi cha mtu mmoja (ISDT)
Hiki ni kitafsiri ambacho kitatumika kutafsiri sauti kuwa katika lugha ya alama na maandishi au lugha ya alama kuwa katika lugha ya sauti na maandishi,kitatumiwa na mtu mmoja mmoja.

Kifaa hiki kitakuwa katika ukubwa wa aina mbili yaani kama kishikwambi cha ukubwa wa kati,na ukubwa wa juu.

Kitaongozwa kwa kioo mguso (touch screen),kiingiza taarifa ambacho kitakuwa kinaweza kubadirika kutoka kawaida na kwenda katika mfumo tambuzi wa herufi na namba kwa mguso, kitakuwa katika mpangilio maalumu na herufi na namba zitaweza kutambuliwa kwa njia ya mguso.

MUUNDO WA KITAFSIRI JANJA.
Vitafsiri janja vya aina zote vitaundwa na kioo kwa ajili ya kuonesha maandishi na ishara,Maikrofoni kwa ajili ya kurekodi sauti,Spika kwa ajili ya kutolea sauti,Kichakata na kitafsiri taarifa, kibadiri taarifa,kamera kwa ajaili ya kuzisoma taarifa za alama na kuzituma katika kichakata na kitafsiri taarifa.

Kitafsiri janja kwa ajili ya mtu mmoja kitakuwa na vitufe analojia upande mmoja kwa ajili kuweza kuruhusu mtumiaji kuingiza taarifa,kubadili aina ya kichapa taarifa “keyboard” kutoka cha kawaida na kwenda kichapa taarifa maalumu ambacho herufi na namba zake zitaweza kuhisiwa,kurejea taarifa iliyochapwa kwa ajili ya uhakiki na kuituma,hivi vitakuwa maalumu kwa ajili ya vipofu na vitapangwa kwa mpangilio thabiti na Kitasetiwa kulingana na mahitaji ya mtumiaji (kiziwi au kipofu)kwa kutumia analojia.

Kitafsiri janja kwa ajili ya kundi maalumu kitakuwa na kifaa maalumu kidogo ambacho muongeaji wa wakati ule ata kuwa nacho ili kufanya kifaa kuwa na mawasiliano ya aina moja tu,hakitaweza kurekodi sauti ama alama kutoka kwa mtu mwingine isipokuwa Yule aliye na kifaa hicho ambacho pia kinaweza kutambuliwa na kifaa cha mtu mmoja ambaye yupo eneo lile.

UTENDAJI KAZI.
Vifaa vitatumia kanuni ya kwamba “Sauti iwe ishara na maandishi na maandishi ama ishara iwe sauti” ili kukidhi falsafa ya kwamba ““Asiye ona lakinii anasikia ataona kwa kusikia,na asiye sikia lakini anaona atasikia kwa kuona” hii inategemeana na namna namna mtumiaji ameseti kifaa chake.

Sauti itarekodiwa kwa maikrofoni na kutumwa kwenye kichakata taarifa kisha kitafsiri taarifa ambacho kitaaibadiri lugha katika mfumo wa sauti na kuwa lugha ya alama na maandishi,taarifa itarudishwa katika kioo cha kifaa ambacho kitaonesha maana ya sauti ile katika lugha za alama ambazo tayari kifaa kinakuwa kimetengenezwa kutambua na kwa wakati huohuo,kioo kitaonesha maandishi ambapo lugha ya alama itakuwa na maana moja na yale maandishi yanayoonekana katika kioo na Hapo muhusika atakuwa amepata taarifa kamili.

Lugha za alama zitarekodiwa na kamera kisha kutumwa katika kichakata taarifa ambacho kitachakata kisha kutuma kwa kitafsiri taarifa ambacho kitaitafsiri lugha hizo za alama kuwa katika mfumo wa sauti na maandishi,sauti ya kitafsiri utachagua wewe kupitia mpangilio wa kifaa.
Mafunzo ya matumizi yatatolewa na msambazaji wa vifaa wakati wa manunuzi,Lugha za alama zitafundishwa kwa msaada wa kifaa maalumu kupitia mpangilio wake.
Kitafsiri janja cha kundi kitafungwa katika eneo husika la ukumbi,kanisa ama msikiti katika sehemu ambayo inaweza kupokea taarifa pasipo shida yeyote na kinaweza kuonwa na yeyote,ukubwa unaohitajika utategemeana na ukubwa wa ukumbi,na kile cha mtu mmoja atakuwa nacho mtumiaji mwenyewe.

MIWANI JANJA KWA AJILI YA KIPOFU (BSG)
Ni miwani maalumu kwa ajili ya kumuongoza kipofu anayeweza kuongea na kusikia ama kusikia tu,Itakuwa na uwezo wa kutafsiri kile kinacho onekana na umbali wake na kisha kutoa tafsiri kwa njia ya sauti ambayo itasikika na mtumiaji wa kifaa.

MUUNDO NA UTENDAJI KAZI WA MIWANI
Itakuwa na muonekano kama miwani ya kawaida lakini kwa utofauti kidogo kutokana na muunganiko wa vifaa wezeshi.

Itaundwa na lensi mbinuko mbili ambazo kazi yake itakuwa ni kukusanya miale ya mwanga kwa ajili ya kamera,kamera ndogo mbili zitakazo fungwa katika kila lensi pembeni kabisa,kamera hizi zinatakuwa ni “auto -focus”,CPU ambayo kazi yake itakua ni kuchakata taarifa kutoka kwenye kamera na kuifanyia maamuzi,maamuzi hayo yatatumwa kwenye kitafsiri maamuzi ambacho kitaitafsiri taarifa ile nakuibadili kuwa katika mfumo wa sauti ambayo itasikisa na mtumiaji wa kifaa kupitia spika ndogo ambazo zitakua jirani na masikio yake mawili(kulia na kushoto.

Taarifa katika CPU itatoka taarifa kamili,Baada ya hapo ubongo wa mtumiaji ndio utaamua maamuzi gani yachukuliwe.

Miwani hii itakuwa na uwezo wakutambua maandishi kwa mtiririko maalumu,maandishi hayo yatabadirishwa na kuwa sauti ambayo itasikika na mtumiaji katika lugha iliyoandikwa,itaweza kuzitambua lugha zote muhimu,lugha itakayotumika katika kupata taarifa itasetiwa na mtumiaji mwenyewe.Itatumia betri ndogo ya kuchaji itakayo dumu kwa masaa zaidi ya 168, itapatikana ndani ya sehemu maalumu iliyopo upande mmoja wa miwani,sehemu hiyo ndio ambayo vifaa wezeshi vya kielektroniki vitapatikana kwa lengo lakukamilisha kazi ya miwani husika.
 
Back
Top Bottom