Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,969
- 20,762
Ndugu zangu Watanzania,
Nashindwa niandike nini ,nashindwa niseme nini ,nashindwa nieleze vipi juu ya uwezo mkubwa wa kiakili alionao na aliojaliwa kuwa nao Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Rais Samia ni Mpango wa Mungu,ni chaguo la Mungu na kapewa akili nyingi na maarifa Makubwa na Mungu Mwenyewe.
Sasa kumekucha ,sasa kumepambazuka, sasa mambo yameiva, sasa ushindi upo Mikononi Mwetu, sasa ni suala la muda tu kwa profesa Mohammedi Janabi kutangazwa kuwa mkurugenzi Mkuu wa WHO kanda ya Afrika , sasa bendera ya Tanzania ipo kileleni ikipepea katika mioyo ya wa Afrika na ma RAIS wa Afrika.
Sasa Tanzania ndio habari ya Mjini ,sasa Tanzania ndio inayoendelea kugonga na kuteka vichwa vya habari na habari mitandaoni.
Hii ni baada ya Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kuingia katika uwanja wa vita, kusogeza vifaa vya kivita katika uwanja wa mapambano, kuja mstari wa mbele katika uwanja wa mapambano katika kumuombea kura Professor Mohammedi Janabi anayewania ukurugenzi wa WHO kanda ya Afrika.
Jemedari mzuri ni yule anayejua ni wakati gani wa kwenda na kupeleka jeshi vitani ,ni wakati gani wa kurusha Makombora kwa adui na yatue wapi. Jemedari mzuri ni yule anayeshinda vita kabla ya kuingia vitani. Tayari Tanzania tumeshashinda vita hii chini ya uongozi Thabiti, madhubuti,imara na hodari wa Rais wetu Mpendwa Daktari Mama Samia.
Rais Samia ni jasusi,ni komandoo hodari, ni askari mwenye shabaha
.hajawahi kushindwa katika vita ya aina yoyote ile huyu Mama yetu Mpendwa. Akimpa mtu baraka ni lazima ashinde tu huyo mtu. Akiweka mkono wake mahali ni lazima baraka na Neema zitiririke,. Akitia neno mahali ni lazima matunda na matokeo chanya yapatikane.
Mama kwa upole ,unyenyekevu,utulivu, kwa hoja nzito na ujasiri wa hali ya juu kabisa kuwahi Kushuhudiwa amejitokeza mbele ya Bara la Afrika na macho ya Dunia nzima kumuombea kura profesa janabi. Ambapo kwa kiingereza safi na Kilichonyooka kama rula ameelezea uzoefu mkubwa alionao Prof janabi na mchango wake mkubwa katika secta ya Afya .na kuwa huyu ni mtu sahihi kabisa katika kuleta matokeo Chanya katika secta ya Afya Barani Afrika.
Kuna faida kubwa sana kwa Taifa kuongozwa na Rais mwenye ushawishi kwa watu wa Mataifa mbalimbali kama ilivyo kwa Rais Samia.kuna raha ya kuwa na kiongozi aina ya Rais Samia mwenye uwezo wa kujieleza na kujenga hoja zenye kugusa watu,mwenye akili kubwa na upeo wa juu.
Watanzania tuna kila sababu kuandaa akili kubwa na viongozi wenye ushawishi kama tulivyo bahatika kumpata Rais Samia. Viongozi ambao wakisimama kuzungumzia hadharani. Watu wote na Bara lote na vyombo vyote vya habari vinasimama kwa utulivu kumsikiliza. Ni neema kwa Taifa letu kuwa na RAIS Samia katika kiti cha Urais.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.