VIDEO: Prof. Lipumba akiri kumsaidia Rais Kikwete katika Uchaguzi 2010

Kama Serikali haitamchukulia hatua Lipumba itakuwa ushara nyingine ya Udhaifu wa Kikwete
 
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameibua suala zito akikihusisha chama chake na “kumnusuru” Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu uliopita.

VIDEO:

Prof. Lipumba akiwa Msikitini na Siasa za Tanzania - YouTube


Tanzania Daima limefahamishwa kuwa Profesa Lipumba alitoboa siri hiyo katika Msikiti wa Idrissa, Kariakoo, jijini Dar es Salaam, alikokwenda kuswali swala ya Ijumaa, miezi kadhaa iliyopita.


Kwa mujibu wa video ya tukio hilo, ambayo gazeti hili lina nakala yake, Profesa Lipumba alikaribishwa kuzungumza na waumini hao mara baada ya utangulizi uliotolewa na Imamu wa msikiti huo, Sheikh Ali Basaleh, aliyemtaka awaeleze Waislamu hali ya kisiasa nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015.


Huku akisisitiza juu ya umuhimu wa mshikamano wa kiimani, Profesa Lipumba alianza kwa kuzungumzia matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010, na ushindani mkali wa kisiasa uliokuwapo.


Alisema hawaoni matunda ya jitihada walizofanya kumnusuru Rais Kikwete asishindwe, kwani hata chini ya uongozi wake, Waislamu wameendelea kutothaminiwa.


“Ninyi masheikh mnajua vizuri zaidi hali ya kisiasa ilivyokuwa, kwamba ilibidi zifanyike juhudi za makusudi ili kuokoa jahazi. Lakini pamoja na kuliokoa jahazi, hali halisi inaonyesha mpaka sasa hakuna matunda yoyote yaliyopatikana, na tupo katika mtihani mgumu zaidi,” alisema.


Katika hali ambayo inasemekana ushindi wa Rais Kikwete ulipatikana kwa mbinu, huku wengine wakiituhumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa ilimnusuru mgombea wa CCM, kauli hii ya Profesa Lipumba inadokeza kwamba anajua mkakati zaidi wa kazi ya Tume ya Uchaguzi.


Katika hali isiyo ya kawaida, Profesa Lipumba anaonekana kuhamasisha Waislamu kujipanga akisema “wenzetu wameanza kujipanga” kuelekea 2015.


“Kwahiyo kama Waislamu tunataka kupata haki zetu, kama tunataka kuishi kama raia wa daraja la kwanza katika nchi yetu, lazima tujipange kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015; na sisi tuanze kujipanga kwa sababu wenzetu wameanza kujipanga, vinginevyo tutaendelea kubaki maskini na raia wa daraja la nne katika nchi yetu wenyewe.

 
“Mwaka 2010 wakati mshindi wa uchaguzi wa rais alipotangazwa, mimi nilikwenda kwenye hafla ya kutangazwa matokeo, na nilikwenda makusudi tu, siyo kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, ila nilikwenda makusudi kwa kujua hali ya kisiasa ilivyokuwa wakati huo.


“Huku nilikutana na Sheikh Basaleh. Nilipokutana naye, alinipongeza; sijui kama yeye anakumbuka, akaniambia ‘umeweka mbele imani yako na umekuwa mwelewa wa mambo.’”


Hata hivyo, licha ya Profesa Lipumba kuwaambia Waislamu wajipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu, hakusema wajipange kupitia chama kipi.


Lakini alisisitiza kwamba uchaguzi ujao ni zaidi ya siasa au rais yupi anafaa, bali maslahi, hasa ya rasilimali nyeti zinazopatikana katika ukanda wa Pwani ya Mashariki, eneo ambalo alisema linakaliwa zaidi na watu wenye imani ya Kiislamu.


Katika moja ya kauli zake, Profesa Lipumba alisema kwamba kuna chama kimoja kinataka kuchukua madaraka ya nchi, lakini kinasaidiwa na mataifa ya magharibi, yasiyoenzi wala kuthamini imani ya Kiislamu.


Kwa muda sasa, zimekuwapo tetesi kwamba CCM imekuwa inafanya siasa za udini dhidi ya vyama vya upinzani, hasa inapoona maslahi yake yapo hatarini.


Mwaka 2010 makada kadhaa wa CCM walitumia mitandao ya simu kuchonga (spoofing) ujumbe wa simu ulioshambulia mgombea mmoja wa upinzani, ukimhusisha na imani yake.


Kauli ya Lipumba imethibitisha pia minong’ono iliyokuwapo muda mrefu kuwa baadhi ya kura za Profesa Lipumba zilipotelea kwa Rais Kikwete.


Katika uchaguzi huo, Lipumba alitangazwa kushika namba ya tatu, nyuma ya Rais Kikwete na Dk. Willibrod Slaa wa CHADEMA.


Alipoulizwa kuhusu ziara yake msikitini na kauli aliyotoa, Profesa Lipumba alikiri kwamba alikwenda kuzungumzia hali ya kisiasa nchini. Hata hivyo alisema inawezekana video hiyo imechakachuliwa kwa kuungaunga vipande vya matamshi wanavyovitaka badala ya hotuba nzima.


Hata hivyo, video iliyotazamwa na waandishi wa habari hii, ambayo nakala yake imetunzwa na gazeti hili, haionekani kukatwakatwa.


Katika tukio hilo, Sheikh Baseleh ndiye anayeanza kuzungumza huku akisoma kipande cha gazeti lililomnukuu Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji, Dk. Mary Nagu, akizungumzia mchakato wa katiba, kwamba Tume ya Katiba “haitazingatia maoni ya wachache”, na kwamba mambo ya dini yasiingizwe kwenye katiba.


Katika ufafanuzi wake, Sheikh Basaleh anasema Dk. Nagu alizungumza mambo haya mbele ya waumini wa Kanisa la Chang’ombe kwenye uzinduzi wa kwaya; na kwamba miongoni mwa mambo ambayo yanaitwa ya kidini yasiyotakiwa kuingizwa kwenye katiba ni Mahakama ya Kadhi Mkuu.


Baadaye anamkaribisha Profesa Lipumba, ambaye naye katika hotuba yake, pamoja na mambo mengine, anakosoa msimamo wa serikali kutaka Waislamu waanzishe mahakama yao ya kadhi, akisema mahakama ni chombo cha dola ambacho hakipaswi kuwa nje ya mfumo wa serikali.


Mara baada ya Profesa Lipumba kuhitimisha hotuba yake, Sheikh Basaleh alimkaribisha Sheikh Musa Kundecha, ambaye naye alisisitiza kauli ya Profesa Lipumba kuwataka Waislamu wajipange kwa ajili ya 2015.


Vile vile alifafanua kuwa “wachache” waliozungumzwa na Dk. Nagu ni Waislamu, kwani zilishatoka taarifa katika kituo cha TBC kuwa idadi ya wasiokuwa Waislamu nchini ni asilimia 52.


“Mimi sijaiona hiyo video ila nimeisikia tu kuwa ipo inauzwa mitaani na makanisani, lakini inawezekana waliorekodi wamenichakachua maana imekuwa siku nyingi kidogo tangu niende kuongea pale Msikiti wa Idrissa. Yamewezekana wameungaunga vipande wanavyovitaka ili kunipaka matope mimi na CUF kuwa tuna udini,” alifafanua Profesa Lipumba.


Alipotakiwa akutane na waandishi wa habari hii ili waiangalie kwa pamoja video hiyo ili kujua ukweli kama ni video halisi au ya kuchakachua, Profesa Lipumba alisema waandishi waende kumwona Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma, Abdul Kambaya.


Alipopigiwa simu, Kambaya hakutoa ushirikiano kwa waandishi. Badala yake aliwashambulia kuwa wana ajenda ya siri dhidi ya CUF, akisema wanafuatilia na kuona makosa ya viongozi wa CUF tu na kufumbia macho vitendo vya wanasiasa wengine wanapokwenda makanisani.


“Nyie waandishi wa Tanzania mmezidi, yaani ninyi mnaona matendo ya viongozi wa CUF tu, wengine wakienda makanisani mbona hawafuatiliwi? Mbona hamumfuatilii Lowassa akienda makanisani? Au mbona hamsemi Dk. Slaa akienda kanisani? Sasa Profesa akienda msikitini kuongea na Waislamu wenzake kuna kosa gani? Sasa ninyi andikeni chochote,” alifoka na kukata simu.


Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro alipotakiwa kuzungumzia video hiyo, alikataa katakata na kuwashauri waandishi wawasiliane na ama Profesa Lipumba mwenyewe au Kambaya.


Itakumbukwa kuwa kumekuwepo tuhuma dhidi ya Rais Kikwete na CCM kuwa mwaka 2010 waliendesha propaganda chafu za udini zenye lengo la kuwagawa Watanzania hususan Wakristo na Waislamu kwa manufaa yao ya kisiasa.


Mwelekeo huo wa kisiasa wa Rais Kikwete na CCM unadaiwa kutokana na hatua ya viongozi wa Kanisa Katoliki nchini kupitia Idara ya Uchungaji kutoa waraka maalumu uliowataka Watanzania kuchagua viongozi waadilifu.


Waraka huo haukuifurahisha CCM, ambayo imekuwa inagubikwa na tuhuma nyingi za ufisadi. Makada na viongozi wa CCM walijaribu kuupinga kwa kuupotosha, wakisema unaingiza mambo ya dini katika siasa.


Kanisa Katoliki lina utaratibu wa muda mrefu wa kutoka nyaraka kuelekeza waamini na wananchi juu ya mambo ya msingi katika jamii.


Katika hali hiyo, Rais Kikwete na CCM wanadaiwa kukimbilia kwa viongozi wa Kiislamu na kuwaomba wawaunge mkono kwa kuwajaza maneno ya uongo, kwamba Wakatoliki walikuwa wamewaagiza waumini wao kupigia kura wagombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Inadaiwa waliwafitinisha zaidi kwa kuwaeleza kuwa aliyekuwa mgombea kiti cha rais wa CHADEMA katika uchaguzi huo, Dk. Willibrod Slaa ambaye ameshawahi kuwa Padri, alikuwa ametumwa na Kanisa Katoliki ili kuendeleza utawala wa Kikristo nchini.


Propaganda hizo hazikuishia kwa viongozi na waumini wa Kiislamu tu, bali zilielekezwa pia kwa viongozi na wafuasi wa CUF ambao walirubuniwa na kushawishiwa kumpigia kura “Muislamu mwenzao” Rais Kikwete, huku wakiahidiwa kuwa mwaka 2015 Waislamu wa CCM nao watampigia kura mgombea wa CUF kwa hoja kuwa CCM watakuwa wamesimamisha mgombea Mkristo.


Licha ya madai hayo ya udini kuwa wazi kwa muda mrefu, lakini wakati wote Rais Kikwete na CCM wamekuwa wakikanusha tuhuma hizo na kuziita kuwa uongo na uzushi.



CHANZO: Tanzania Daima
 
haya basi polisi wa said mwema mlisema mnapitia mitandao ya jamii basi mkamateni na prof lipumba, mmfungulie mashitaka ya uchochezi km mnavyofanya kwa viongozi wengine wa upinzani? Au kwa kuwa yeye kasema aliisaidia ccm na mgombea wa dini yake kushinda uchaguzi mkuu wa 2010 basi prof lipumba hawezi kukamatwa? Tunasubiri mashitaka haya haraka mahakamani vinginevyo tutaendelea kuamini kweli kuwa jeshi la polisi halifuati sheria bali linapata maelekezo toka juu ya nini mfanye juu ya uhalifu.
 
Dah!! Sijui nimtetee vipi prof lipumba, maana kusema kweli hadhi yake haiendani na matamko haya labda ni ile fursa anaiyoiona kwa kupitia waumini wenzake, nimesikitika kusema kweli..
 
Nilisita kuiangalia iyo video baada ya kuona ni 43 minutes long, duh itanimalizia bundle yangu
Lakini nikapata tena link ya the same kwenye email, sikuwa na option ila kuiangalia.
Pathetic Lipumba,
Ni ngumu kuamini kuwa ni video ya Lipumba Profesa wa "uchumi"
au ni filamu nyingine kama ile ya "Lwakatare"
 
Nitashangaa sana endapo Mtatiro na watu wengine makini wote waliopo CUF watakubali kuendelea kuwa chini ya uenyeketi wa huyu bwana.
.
Lipumba kawaambia machoni mwao bila kumung'unya tena kwa kiswahili safi.
Kazi kwao kama wana bongo zimesalia, au wana minazi wamejiywika juu ya shingo wanaiita vichwa.
 
duuh am speechless kwa kweli, all i can say wabongo we can end this udini things mazima ikabaki stry, haya yaliletwa na wakoloni kwann yatukae na kutugawa namna hii, fanya kazi kwa bidii jifunze kwa bidii piga vita udini na ukabila lets be one tusake maendeleo hii karne si ya kuanza gombana kisa dini kabila, adui yetu ni umaskini na ujinga na maradhi tu, let us unite tuwashinde hao adui wa3, no need for hate speeches, comments etc kisa dini tuloletewa na foreigners, tuchague viongozi wataofaa kwa maendeleo yetu sio dini yake, ni hayo tu mazee tuweni makini sana. One love
 
Ningekuwa Mtatiro ningejiuzulu Nyadhifa Zote Ndani ya CUF.
Pia Ningerudisha Kadi yao ya Uanachama maana Mwenyekiti wa CUF amesmea Kuwa yeye Yupo Kwa ajili ya Maslahi ya Waislam.
Thats to Say, Chama cha CUF Kipo kwa ajli ya Dini ya Kiislam.
Pia nitawashangaa sana kama still Wanachama wote wa CUF (Wa Kristo, including Magdalenna Sakaya) Kama Bado wataendelea Kujiona nao ni Sehemu ya Kutekeleza Mipango michafu ya CUF
My Take
CCM Walipokuja na Propaganda ya CUF kuwa ni Chama cha Kiislam, walikuwa sahihi 100000%
Hiyo wala haikuwa propaganda.
wala hawakufanya homework kujua hilo.
Ni fact iliyokuwepo tangu baada ya kufukuzwa waanzilishi wa CUF kina James Mapalala.
Na CUF waliweka wazi kuwa kina mrengo gani kwa kila walichokifanya na namna walivofanya..
Leo Lipumba kama Mwenyekiti wa Taifa wa CUF na Mgombea mara zote wa CUF, kaamua kuukumbusha tu umma wa Tanzania kuwa "msihangaike na CHADEMA, dini iko huku"
 
Kabla ya kuangalia video hii nilikuwa namchukulia Profesa Lipumba kuwa ni mtu wa maana, ambaye ahata akishinda uchaguzi tunaweza kusema tuna mtu makini na mwenye akili anayeweza kutuongoza, lakini kutokana na kujiingiza kwenye cheap politics na kukubali kuwa yeye ni mtu wa kuwa used, naona ameshusha hadi yake sana na kubaki kuwa a schooled fool.

Kama hajui Tanzania inataka nini, na watanzania wanataka nini, na kama anakitumia chama cha CUF kwa maslahi ya kuokoa jahazi basi hana maana hata kidogo.
 
Lipumba hafai hata kuwa Imamu wa msikiti, akiwa Imamu atataka awe Imamu wa Maisha kama alivyokuwa Mwenyekiti wa Maisha huko CUF

Waislam for 50 yrs bado tunalalamika na kuendelea kuichagua CCM badala ya kuangalia maendeleo ya nchi, sisi tunakadhania Uislam na Ukiristo huku Rasilimali zetu zinaibiwa na Wawekezaji walioletwa na Kikwete na CCM yake

Rais
Jaji Mkuu
Mkubwa wa Usalama wa Taifa
IGP
Hao wote ni waislam na bado tunalalamika kuwa tunaonewa, ni nani hasa anayetuonea kama sio sisi wenyewe tunaoneana? Tusitafute mchawi wakati mchawi wetu tunamchua kuwa ni CCM.

Badala ya kufikiria Maendeleo ya Taifa letu bado tumegubigwa udini na kunyooshea wenyewe kwa wenyewe vidole, sisi wote ni Watanzania na tuna haki ya kuishi katika Taifa letu bila ya kujali dini. Adui wa Muislan ni CCM hakuna mwengine.

Kikwete nchi imemshinda asitafute mchawi, aondoke kabla halijaangamia hili Taifa.

Sisi Waislam tujue kuwa Ukiristo, Uislam, Ubaniani, Ugalatia na dini nyingine zitakuwepo Tanzania na zitaendele kuwepo, as long the world still exist na hizo dini zitakuwepo.

Kwa hiyo wahubiri wa dini, Get lost

Adui wa Waislam ni CCM, tukifanikiwa kumtoa hii nchi itatulia na maendeleo ya nchi yatapatikana

Bado Nina Mashaka na Elimu ya Prof Lipumba naona haiimsaidi kujua lipi ni zuri na lipi ni baya kulisema kwenye jamii, hafai hata kuwa Kiongozi wa Mtaa. Shame on him.

Huyu Lipumba hana lolote anajitia anatatea haki za dini kumbe uchu wa madaraka kama alivyo Kikwete, Lipumba hafai hata kuongoza kwao urambo hatoweza.

Asante Kwa ufasaha wa hali ya juu wa kuchambua mambo....ila CCM ina sera nzuri tatito wanachama wake haswa wale ambao ni wasimamizi wa sera
 
Sishangai sana kwa profesa Lipumba kuongea pumba nama hii; sehemu kubwa ya maprofesa wa kiislamu wamekuwa wanajua sana kuwatumia wailsmau katika ajenda zao. Profesa Malima alianza hivyo, baada ya hapo wamefuatia kama wawili au watatu hivi na leo hii Profesa Lipumba naye kajiunga kwenye listi. Inawezekana maprofsa hawa wanajua sana pande zote mbili za shilingi, na hivyo kuamua namna ya kuzitumia pande hizo.
 
Najiuliza kama Dr Slaa angekuwa ameyasema hayo sijui media ingekuwa katika style gani kwasasa!
 
bongo hali ya madarasa mjengwablog 8-3-12.jpg
Prof Lipumba hii ni mojawapo ya shule za msingi wilayani Ilala. Swali kwako: je hawa watoto ni Waislamu au Wakristo? Je hawa watoto ni raia wa daraja la kwanza au la nne? Je mafisadi wanachagua dini au kabila au rangi? Mhe Prof. au mwakilishi wake tupe majibu ya kujitosheleza ndio tuweze kukubaliana na ideology yako ya kuwa na "tujipange na sisi tuweze kuwa raia wa daraja la kwanza."
 
  • Ni Sheikhe Mwendawazimu tu ndio ambaye angependa/anapenda/atapenda kumuona Padre yupo Ikulu anaongoza nchi


  • Ni Padre/Askofu/Mchungaji Mwendawazimu tu ambaye angependa/anapenda/atapenda kumuona Sheikhe yupo Ikulu anaongoza Nchi.


  • Si jambo la kushangaza kumuona Askofu/Padre/Mchungaji akimpigia kampeni Padre ili aingie Ikulu kuongoza Nchi.

Haya ndio yaliyotokea 2010 na Prof.Lipumba alikuwa anayaanika.Kosa alilolifanya Prof.Lipumba ni kwenda kuyaanika haya mambo Misikitini.Kichomsukuma kufanya hivi ni hiki:


  • Wanachama na mashabiki wengi wa CUF ni Waislamu


  • Wanachama na washabiki wengi wa CHADEMA ni Wakristo
Ni kichaa tu ndio atakayekataa ukweli huu


Na hili ndilo linaloliangamiza Taifa letu. Imetokea bahati mbaya tu hii video imevuja kwa Lipumba lakini siasa za udini zimetawala kwenye vyama vyote vikubwa vya siasa hapa Tanzania.
 
Back
Top Bottom