Mtanzania Tajiri
JF-Expert Member
- Aug 31, 2024
- 254
- 243
Tofauti sana na watu wengi walivyofikiri kuwa Hayati Mwl JK. Nyerere hakutaka sekta binafsi PPP, Hii si kweli,
Ukweli wa wazi MwL JK. Nyerere aliamini zaidi katika sekta binafsi kuwa ni ndio msingi pekee wa kuleta mtaji na zaidi sana kuchochea ufanisi katika usimamizi na uendeshaji wa Serikali yake Leo ni zaidi ya miaka sitini (60) imepita mawazo ya Mzee huyu yanaingia katika utekelezwaji rasmi.
Kwa msiofahamu moja ya jambo ambalo Mzee huyu alilikiri hadharani tena Waziwazi kufanya makosa katika awamu yake ni kupoka Mali za sekta binafsi kama Mashamba ya mkonge, Pamba, Kahawa kutoka sekta binafsi na kuyarudisha Serikalini, hili lilikuwa ni kosa kubwa la kiufundi mtakumbuka kabla ya hiki Tanzania tulikuwa ndio vinara wa Mkonge duniani leo majibu sote tunayo.
Swala jingine ambalo Mzee alijutia baada ya kung'atuka madarakani ni kuufanya ushirika uendeshwe na Serikali badala ya kujiendesha wenyewe kama sekta binafsi nadhani madhara haya hata Leo bado yanaonekana.
Wakati flani nikimkumbuka Hayati Mwl JK Nyerere, nikikumbuka maono yake hasa haya ya Ubia huwa napata faraja sana ninapomwona Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akipita mulemule na hii ni baada ya miaka 60 kupita Leo hakika hakuna kama Samia.
Hoja fikirishi zaidi kwa wasomaji wangu, "Kama Muasisi wa Taifa hili hakuwa na Wasiwasi juu ya wahindi wala Wapemba au Wawekezaji wengine wowote wazawa wa Ubia nyie wengine hofu yenu mnaitoa wapi juu ya hii PPP kama sio kutuchelewesha kama Taifa?"