Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,494
- 96,073
Vyeti vyeti vyeti vyetiHILI NITALISEMA, JAPO BAADHI YA WATU LINAWEZA KUWACHUKIZA!
Ni jambo la kushangaza na kusikitisha sana, kumuona mtu anaesema kuwa yeye ni Mtumishi wa Mungu tena mwenye kuchunga Kundi kubwa la Watu, LEO akirekodi VIDEO akimkemea pepo aliye ndani ya Wanamke, na kuliamuru PEPO, ili alisamehe basi likamwangie mtu fulani, anaemsema kuwa ni MSUMBUFU ndani ya Mkoa ambao mtumishi huyo anaishi cha ajabu PEPO linamjibu na kusema "Yule haingiliki"
Sasa kama unaliamuru JESHI lako kwenda kupigana na mtu fulani, halafu JESHI lako linakujibu kuwa, hatuna uwezo wa kumpiga mtu huyo, hapo utakuwa na nini tena kwa mtu huyo? maana wewe mwenyewe huna uwezo wa kumshughulikia, unayategemea mapepo, mapepo nayo yanakujibu hayana uwezo wa kuifanya hiyo kazi yako! ni wakati wa kurejesha heshima hakuna sehemu yo yote ambayo YESU amewaamuru wanaomwamini kuyatoa mapepo kutoka kwa mtu huyu na kuyaingiza kwa mtu mwingine, bali yeye alichotaka ni kuyatoa tu
Marko 16:17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
Kitendo cha Mtumishi wa MUNGU kusingiziwa! siyo cha ajabu, na hauwezi kuwakomesha wanaokusingizia kwa kuyaamuru kumwingia mtu fulani mapepo ambayo yanakwambia kuwa hayana uwezo wa kumwingia, tiba ya kukomesha masingizio ni hii
1 Petro 3:13 Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?
14 Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu.
15 Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.
16 Nanyi mwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.
17 Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya.
Ukisingiziwa jambo lolote unachotakiwa wewe ni kuonyesha dhamiri njema, ili uwaabishe wanaokusingizia, kitendo cha kuyaamuru mapepo kumwingia mtu yule ni dhamiri mbaya yenye kumtukanisha Kristo aliyetuamuru akisema
Marko 11:25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
26 Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]
Kitendo chako cha kutokumsamehe kinamfanya Kristo aonekane hakuwa na mafundisho sahihi, hivyo anahitajika kurudi afanye mabadiliko, aruhusu kulipa kisasi kwa adui zetu, kitu ambacho yeye hakukitaka
Mathayo 5:38 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;
39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.
40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.
Kristo hakututaka sisi kushindana na mtu muovu, mtu akikutuhumu, wewe ni SHOGA, jambazi, Kahaba Mvuta Madawa, Mwasherati, wakati wewe haupo hivyo ni dhahiri kuwa nia yake ni OVU! wewe hutakiwi kushindana nae, kwa kuyaamuru Mapepo kumwingia mtu huyo bali kumuombea baraka.
Luka 6: 27 Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi,
28 wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.
29 Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang'anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.
30 Mpe kila akuombaye, na akunyang'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie.
Yesu alituambia tufurahi na kushangilia kila tunaposhutiwa kwa ajili yake, kwa sababu, Thawabu yetu ni kubwa sana MBINGUNI.
Mathayo 5:11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
Unapomuona mtumishi anaposingiziwa neno, na kunenewa mabaya, halafu yeye anaanza VITA ya kutupiana mapepo ambayo hayana uwezo, inanishangaza najiuliza mtu huyo anajifunza kwa nani? Kama ni kwa Kristo tunaambiwa
1 Petro 2:20 Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.
21 Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.
22 Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.
23 Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.
Kristo alikuwa na uwezo wa kuogofya, lakini hakufanya hivyo, yeye alipotukanwa hakurudisha matukano, ameitwa CHIZI MWEHU, KICHAA, MWENDAWAZIMU (yaani mtu aliyerukwa na akili)
Marko 3: 21 Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili.
Lakini yeye hakurudisha wala kuyaamuru mapepo kuwaingia Watusi na watesi wake. Hebu fikiria, Yesu angeamua kulipiza kisasi, Waliomfanyia mabaya wangekuwa wapi wakati huo? Mapepo yalipomuona yalianguka na kulia, yakamuomba ayaruhusu yawaingie nguruwe, Je! Angeshindwa kuyazuia yasiwangie NGURUWE, na badala yake yakamwingie, Mfalme Herode?
NIMEYASEMA HAYA MTANDAONI KWA SABABU VIDEO YAKE AMEISAMBAZA MTANDAONI! NIMEYAANDIKA HAYA ILI WATU WANAODHANI KUFANYA HIVYO NI MAFUNDISHO YA KIKRISTO, WAJUE KUWA SIYO SISI TUNATAKIWA KUWA TOFAUTI NA WATU WA IMANI NYINGINE, SISI NI HIVI
Warumi 12:17 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
18 Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
20 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
By ABEL SULEIMAN SHILIWA
email abelshiriwa@gmail.com