Bailly5
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 16,418
- 35,121
Mambo ya kilimo cha lazimaChezea Anko Magu tutapandikiza hadi nyanya madirishani
Mambo ya kilimo cha lazimaChezea Anko Magu tutapandikiza hadi nyanya madirishani
Si mchezo...uswahilini kiboko. Ndo sehemu yakujifunzia kila kits
Kubwa zima linaogeshwaImefanyaje.....
Hatare sana mkuu!Uswahilini dagaaa...lazima mwili unyooke km rula
Ha ha haa kama kawa..Na stress zetu za kula vishombo...
Hahahaha wewe bitoooooz tu
Nimetoka gym...naelekea Masaki kutembeza mkong'oto kwa watoto wa kishua....mwili sio nguvu
Wasije kukutoa nduki tuNaenda kutishia nyau Ishuani c kumejaa mabwege
Hahahaha kama ngapi hivi?Nna bisibisi za kutosha
Ukweli mtupu...Vipi makamanda laifu linasonga wanangu ? Last week nilipita uzunguni pande za Masaki na Oysterbay kupiga mishemishe kule...Basi nikanusanusa na kugundua vijimambo vyao ambavyo pia vipi sehemu za wenye vijisenti km kule Mikocheni n.k....
1/Vitoto vibwegebwege
Watoto wengi wa ushuani vimezidiwa maarifa na hata nguvu na watoto wa Uswaz...kwenye mihezo wanajua kucheza game tu na siku ukiweka mechi kati ya watoto wa kishua v wa Uswaz nahisi watapigwa bao za kutosha tu na kuibiwa vikorokoro vyao vyote .....Everything mabwegwbwege!!!
2/Toto kubwa linaogeshwa
Ukiingia kwenye mahekalu ya wenye nazo usishangae kumkuta beki tatu analiogesha na kulivalisha toto analolizidi miaka 5 tu...Toto linasoma standard faivu lakini halijui hata kuoga....full mdekezo !!!
3/Hawajui malavidavi
Mabinti na wavulana wa uzunguni hawajui sana mapenzi kulinganisha na watoto wa Uswahilini nahisi sababu wanafungiwa sana ndani hivyo. wanachelewa kujua mambo wakati uswahilini vitoto vidogo vinacheki"pilau" vibandani...wakikutana ni full mnyoosho !!
4/Mihogo Coco Beach
Pamoja na nyodo zao nimegundua Wateja wakubwa wa kutafuna mihogo ufukwe wa coco beach ni wakazi wa ushuani sisi watoto wa Uswahilini tunaenda beach wakati wa sikukuu ,wao hushinda kila siku...Hongereni !!!
5/Vinara wa vitambi na mandombolo
Wakazi wa uzunguni wanaongoza kwa matumbo makubwa na mawowowo wake kwa waume...sijui sababu kula kula sana au kutofanya mazoezi hadi kutofautisha demu na dume ni shughuli...full minyamanyama !!!
**** Jiachie...It's week end***
Sharobaro wa Uswaz
The Bitoz