Vanessa Mdee na Rotimi waonesha sura za watoto wao

Nifah

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
33,448
76,246
Kama tunavyofahamu, Vanessa na mchumba wake Rotimi wamefanikiwa kupata watoto wawili, wa kiume Seven na wa kike Imani.

Kwa kitambo, Vanessa na mwenzi wake hawakuwahi kuwaonesha watoto wao katika mitandao kama ambavyo mastaa wengine wakubwa nchini na ulimwenguni kote hufanya.

Usiri ulikuwa mkubwa ambao ulitupa wakati mgumu ‘wambea’ na hata wenye mapenzi mema juu yao waliopenda kuyaona matunda hayo ya mapenzi yao.

Usiku wa kuamkia leo hii, hatimaye kitendawili kimeteguliwa na wapenzi hao kwa kuweka hadharani picha za familia yao hiyo yenye kuvutia machoni na kuleta tabasamu kwa tunaoamini ktk mapenzi ya ukweli na familia bora.

Mwana JF, kipi kimekuvutia zaidi? Ladies, na sisi Mungu atuwekee mkono aliomuwekea Vanessa?

Maoni yangu: Vanessa ni mfano hai wa 'bongo bahati mbaya'. Kila kitu chake ni levels. Fashion wise, anavyoishi bongo hii tulikuwa tunamuonea tu.

Keep on smiling my girl, keep shining the World needs your light. I'm happy for you Vee.

IMG_4080.jpeg
 
Attachments

  • RPReplay_Final1700804129.mp4
    62.2 MB
Kilichonivutia ni namna dada yetu alivyonawiri sana,kweli penzi la kweli tamu ukilipata unatakata tu pasipo hata kupaka lotions. VANESSA ni wakumshinda hips Ruby kweli?Kila lakheri kwao Mungu awasaidie wafunge hiyo ndoa yao mwakani kama walivyosema.
P'se girls epukeni kudate na mwanaume anayeitwa Juma watakunyonyoa ukose nuru kama kuku kishingo hahaha,
 
Cuzoo naomba nikazie, girls yakimbieni mahusiano yaliyokufa.

Acheni kuwang'ang'ania hao wanaume wanaowatenda kwa kutoijua thamani yenu. Kuna mwanaume bora anakusubiri mahali ni wewe tu na uking'ang'anizi wako unajichelewesha.
 
Kabsa,usimpe mtu moyo wako,asiyeona thamani yako.Japokua ni ngumu kuanza upya lakini ni bora utoke kwa maumivu makali ila kesho yako ni njema kuliko toxic relationships.Kudos kwa homegirl saivi anajilia mema ya nchi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom