Value Renention Fees ni wizi wa dhahiri wa Bodi ya Mikopo

Habarini wana jamvi wa Jamii Forum…

Bodi ya Mikopo imekuwa ikijinasibu kuwa inatoa mikopo isiyo na interest kwa ajili ya kusomesha watoto wa maskini. Lakini kwa utafiti mdogo nilioufanya, nimegundua kuwa mikopo inayotolewa na bodi ya mikopo ina riba iliyofichwa kwenye jina la value retention fees (6% annually). Kiasi hiki sio penalty ya waliochelewa kulipa, bali ni rate inayodhaniwa kuwa ni inflation ya Tanzania. Vilevile, kiasi hiko huchajiwa kuanzia wakati bado mwanafunzi yuko chuoni akiwa anaendelea na masomo yake

Kwa mfano:

· Kwa mwanafunzi anayesoma miaka minne (let say; 2001, 2002, 2003 na 2004)

· Ambaye kila mwaka anakopeshwa Shs. 2,500,000 (ada, malazi na kula). Miaka minne atapewa 10M.

Deni atakalodaiwa mara baada ya kumaliza chuo (i.e. mwaka 2005) ni Shs. 11,500,000. Ambapo Shs. 1,500,000 ni value retention fee, sawa na ongezeko la asilimia 15 (15%) ya mkopo aliokopeshwa.

a) Je, bodi ya mikopo hawajinasibu kuwa mikopo wanayotoa inarudishwa kama ilivyo?

b) Je retention fees ina tofauti yoyote na interest inayochajiwa na taasisi za fedha ambao wao wamezika humo ‘effect of inflation’?

c) Je ni sahihi kuanza kumtoza value retention fees kijana ambaye bado anaendelea na masomo? - Mkopo ulitakiwa kuanza kuwa deni baada ya kumaliza masomo, ama wakati bado masomo yanaendelea?

Kwa mfano tulioutaja hapo juu, ikiwa huyo mwanafunzi atachelewa kuajiriwa kwa kipindi cha miaka miwili tu; retention fee ya mkopo wake wa mwaka wa kwanza peke yake itafikia Shs. 900,000 (sawa na 36% ya 2,500,000).

Jumla ya pesa yote atayokuwa anadaiwa ni Shs. 12,700,000 ambapo retention fee ni Shs. 2,700,000 ongezeko sawa na asilimia 27 (27%).

SWALI:

Je, wakopeshwaji waliwekwa wazi kwenye mikataba kuhusu mfumo huo wa kupanda kwa madeni yao hata kabla hawajamaliza masomo na kupata ajira?

o Waliokopeshwa waje humu kutujuza undani wa mikataba yao.

o Wataalamu wa sheria, fedha, huduma za jamii na siasa waweke michango yao pia.

HITIMISHO:

Wanaodaiwa walipe pesa walizokopeshwa; vile vile Serikali nayo (kupitia Bodi) wahakikishe wanakuwa fair, ili mfumo uliowekwa kwa ajili ya kuinua maskini usije ukawa unawakandamiza. Tunaamini, bodi ya mikopo haipo pale kibiashara, ipo kihuduma zaidi ili kusaidia kupunguza gepu kati ya maskini na matajiri. Mikataba wanayopewa wanafunzi ijieleze kinagaubaga.

Nawasilisha!
hiyo huwezi ifananisha na riba ya benki, riba ni inflation + opportunity cost ya kukukopesha hela yake+ unyonyaji mwingine ..ina range kuanzia 25% hadi 60% kwa mwaka
hiyo 6% ni reasonable na justifiable kwa kuwa fedha ya tz inashuka thamani kwa kiwango hicho kwa mwaka na hakuna faida wanayopata hapo.
na wasingeweka hiyo 6% ingekuwa ni unfair kwao na kwa wadaiwa wengine, maana mtu amemaliza 1995 na hajalipa hadi leo halafu akija kulipa alipe ile ile aliyokopeshwa 95 ?
na aliyemaliza 2014 alipe aliyekopeshwa watalipa viwango tofauti kabisa
 
hiyo huwezi ifananisha na riba ya benki, riba ni inflation + opportunity cost ya kukukopesha hela yake+ unyonyaji mwingine ..ina range kuanzia 25% hadi 60% kwa mwaka
hiyo 6% ni reasonable na justifiable kwa kuwa fedha ya tz inashuka thamani kwa kiwango hicho kwa mwaka na hakuna faida wanayopata hapo.
na wasingeweka hiyo 6% ingekuwa ni unfair kwao na kwa wadaiwa wengine, maana mtu amemaliza 1995 na hajalipa hadi leo halafu akija kulipa alipe ile ile aliyokopeshwa 95 ?
na aliyemaliza 2014 alipe aliyekopeshwa watalipa viwango tofauti kabisa
Asante kwa mchango mzuri. Ila bado nimebaki na maswali kadhaa:

Iko sawa kuanza kuichaji hata kabla mwanafunzi hajamaliza masomo yake?

Kwa nini wasingetoa grace period ya kutafuta kazi, then mkopo unapokuwa deni ndo waweke assumption ya value retention?

Vipi kuhusu kuweka hilo swala wazi kwenye mikataba ya wanafunzi kipindi wanakopeshwa?

Nafikiri ikipatikana mikataba ya vipindi tofauti tofauti iliyotumika kukopesha wanafunzi inaweza kutusaidia sana.
 
Heslb pamoja na matatizo mengine ni utunzaji mbovu wa kumbukumbu. Kuna watu wamepachikwa madeni japo walishamaliza marejesho ya mkopo. Aidha wapo pia wasio wanufaika ila Heslb inawaita wanadaiwa.
 
Kuhusu hiyo VRF bodi haiko wazi ni wanufaika wepi wanapaswa kuilipa licha ya kuwa ilipitishwa 2012. Je, inawahusu wote kuanzia 1994 licha ya kuwa walisharejesha mkopo?
 
Habari wana JF,
Ukiachilia mbali mkopo uliochukua loan board pia kuna nyongeza juu yake ambayo wao wanaiita "Value Retention Fee" ambayo ni 6% ya Mkopo mzima kila mwaka,Pia wana penati ya 10% ya mkopo mzima.

Leo nataka tuzungumzie wizi wa Value Retention Fee ambayo anabebeshwa mnufaika wa mkopo,haiwezekani uniongezee mzigo huu kwa kigezo kwamba thamani ya pesa uliyonipa mwaka jana ni tofauti nitakayorudisha Leo,Mbona nikiweka fedha zangu NSSF/PPF kwa miaka hata 10 nikija kuchukua wananipa Faida ya kama laki 1 kwenye makusanyo ya milioni 10? Iweje hizo Value for Money serikali na taasisi zake wanaona wakiwa wanadai madeni yao ila wakidaiwa inakuwa Haipo?

Wabunge mbali ya kufatilia mzigo wa 15% tunaomba mfatilie mizigo wa Value Retention Fee na Penati ya Mokopo wa 10% hata kama umelipa kwa wakati.

BR,
Amalinze The Cat.
 
Habari ya asubuhi wadau,

Kwa wale walionufaika na mikopo ya elimu ya juu, kuna wito umetolewa wa wanufaika kujitokeza ili kuanza kulipa mikopo yako. Kuna suala la Value retention fee ya 6% kwa mwaka tangu mwaka mkopo ulipotolewa hadi sasa na kuendelea hadi marejesho yatakapokamilika.

Naomba tujulishane kwa wanaojua chimbuko la hii retention fee na sheria gani inayozungumzia hii kitu maana wakati tunaomba mikopo hapakuwa na taarifa ya suala hili.

Naomba kuwasilisha.
Kwa kweli retention fee inatuangamiza sana,ni gharama ambayo huijui wakati hujamaliza masomo,ukimaliza masomo ndo unakutana na mchanganuo wake wa 6% kila mwaka kuongezeka.
Mpaka umalize deni lako miaka 10 mbele unakuwa umekatwa pesa nyingi sana.
Yaani kiujumla mhitimu wa chuo kikuu uliyepata mkopo,tambua kamshahara kako halisi ni kadogo sana,kanaathiriwa mnoo na makato ya aina mbalimbali.
Mikopo tunapata lakini tunanyanyasika sana kutokana na mikopo hiyo.
Kwakweli kama unauwezo,usimwingize mtoto wako kwenye mikopo,ni MZIGO.
 
Kwa wale ambao wameanza kurejesha mikopo yao nadhani wamekutana na hiki kitu kinachoitwa Loan Retention Fee. Kuna tozo ijulikanayo kama “Loan Retention Fee” ambayo ni 6% kwa mwaka (6% per annum) ya kiwango cha fedha ulichokopa na inakatwa hadi pale utakapoanza kurejesha mkopo wako.

Pengine bodi ilikuwa/ ina dhamira nzuri tu ya tozo hii ili kulinda thamani ya fedha. Ila kinachonitatiza ni tozo hii kutozwa kwa wanufaika ambao nadhani kwa uelewa wangu hawakustahili hii tozo. Wanufaika hawa ni akina nani? Nasema haya kwa sababu gani? Wanufaika hawa ni wale walomaliza masomo yao kwa mwaka wa masomo wa 2012/13 kurudi nyuma.

Nasema hivyo kwasababu kwa mujibu wa miongozo ya kuombea mikopo “HESLB Guidelines and Criteria for Issuance of Student Loans and Grants” ya kuanzia mwaka wa masomo wa 2012/13 kurudi nyuma haina kipengele hicho cha “Loan Retention Fee”.

Muongozo wa kuombea mikopo wa kuanzia mwaka wa masoma wa 2013/14 ndio ulianza kuwa na hicho kipengele ukijulikana kama “Interest of Loan Issue” (ukurasa wa 9, kipengele cha 4.1) kabla ya kubadilishwa jina na kuitwa “ Loan Value Retention Fee” katika muongozo wa kuomba mkopo wa mwaka wa masomo 2014/15 (ukurasa wa 10 kipengele cha 4.1).

Na katika mwongozo wa mwaka wa masomo wa 2016/17 pamoja na “Loan value retention fee” wameongeza vipengele viwili yaani; “1% Loan Administration fee” na “10% penalty” (ukrasa wa 13, kipengele cha 4.2 hadi 4.4). Miongozo hiyo inapatikana kupitia link ifuatayo;

Guidelines

Maswali yangu ni kuwa;
1. Je kuna uhalali wa wanufaika wa mikopo walomaliza kuanzia mwaka wa masomo wa 2012/13 kurudi nyuma kulipa tozo hizo “6% Loan Value Retention Fee” & “1% Loan Administration fee”? 2. Je ukokotoaji wa hii tozo uko sahihi, ikumbukwe kuwa asilimia sita (6% per annum) inaanza kukatwa toka mwaka ule ulionza kusoma mwaka wako wa kwanza wa masomo chuoni , hadi pale utapoanza kurejesha mkopo, na sio mwaka ule uliomaliza chuo ukawa na uwezo wa kurejesha mkopo?
3. Je sheria inazungumziaje juu ya miongozo na utekelezaji?

Naomba mchango wenu wana JF.
Kwa mujibu wa sheria zao wenyewe, ambayo inasema
''4.0 OTHER CONDITIONS ON ISSUANCE OF LOANS

4.1 Loan Value Retention fee

For the purpose of retaining the value of loans issued as well as making the loan scheme sustainable, all loans issued beginning 2011/2012 shall bear Loan Value retention fee equal to 6% (six) percent, per annum.''

Unaoendelea sasa hivi ni wizi ambao serikali umeubariki kwa baadhi ya watu tu. Mbona wao ambao sasa ni viongozi mbona hizi sheria haziwagusi?
 
Hivi inakuaje sheria kutumika bila kuanishwa kwenye mikataba? mikataba na board ya elimu haikuwai kuanisha namna ya ulipaji wala kiasi cha mkopo zaidi ya kuonesha taarifa za mwombaji na mdhamini. Hii kisheria ikoje wenye kujua watusaidie.
Hapo ndipo wizi wenyewe unapoanzaga
 
Hiyo value retention fee iko kabisa kwenye makubaliano ya mkopo ambayo ulisaini kisha kuyatuma loan board via EMS kwaajili ya kujadili maombi yako. Mie nilitoa copy ya mkataba wenyewe nkabaki nao sikuona hicho kipengele lakini siku niliposikia hilo jambo niliamua kuurejea mkataba kwa kusoma all its content nkakuta hicho kipengele. That is a contract in a standard form you can either reject it or take it. Haukupi nafasi ya kunegotiate. Nadhani mtoa mada hukuupitia mkataba wakati wa kuutuma kama mie, thats why you seem to be surprised.
Hadi wale wa mwaka 1994?
 
Huu uzi nimeuridisha kwa faida ya wadogo zetu wanaorekebisha taarifa zao ZA mkopo ..
My take : kama kipato nyumbani kipo basi s lazma ujibebeshe zigo la mkopo

Na mlioajiriwa kuweni waadirifu mulipe mikopo wengne wasome

*Sheria ichukue mkondo wake*
 
Huu uzi nimeuridisha kwa faida ya wadogo zetu wanaorekebisha taarifa zao ZA mkopo ..
My take : kama kipato nyumbani kipo basi s lazma ujibebeshe zigo la mkopo

Na mlioajiriwa kuweni waadirifu mulipe mikopo wengne wasome

*Sheria ichukue mkondo wake*
Siku za marekebisho nadhani zimeisha mkuu
 
Hv, kwa mwanafunzi aliyepata mkopo akiripoti chuo kwa Mara ya kwanza ni taarifa zipi zinahitajika kutoka kwake kwenda bodi ya mikopo(Yaan kuna usajiri mwingine chuoni unaohusu mambo ya mikopo au ni taarifa zilezile ulizojaza wakati wa kuomba ndo wanabakiwa Nazi na kuwa eendelevu..?)
 
Jamani tunawategemea mlipe hayo maden yenu kama mlivosaini ili na sisi tukasome, hamsomi vigezo na mashart afu mnakuja hapa kulia lia
 
Back
Top Bottom