Black Coffee
JF-Expert Member
- Aug 26, 2016
- 1,931
- 3,179
Ulikosea kumshika mtu shati mfe woote,weee ungetimua kuvyako
Mkuu chochote kinaweza kutokea kwenye taharuki
Ulikosea kumshika mtu shati mfe woote,weee ungetimua kuvyako
Nmecheka sana....pole lkn
Dah hatariNshapoa mkuu .. mambo ya kushtukizana maporini Uko
umesoma ruhuwiko?Hata Mimi nawaza hivyo ! iLa jamaa mwenye ile Pete ni kichwa kweli darasani ndio alikua anategemewa, jamaa alikua fundi wa kupiga kinanda ile mbaya, na alikua kiongozi(mwenye kiti) wa kikundi cha (TYCS)
mi nimehisi kasoma ruhuwiko huyu jamaahii story kama naijua, ulisoma shule gani mkuu kama hutojali
Mkuu magu sehemu ganiKipindi niko form one nilizidisha usumbufu mtaani mzee akaona hili dogo halitamaliza shule hapa town akanipeleka kusoma kwa babu kijijini kwetu alipozaliwa mzee.
Nilipofika pale kijijini kulikuwa kuna mti mmoja mkubwa nilikuwa nasikia story huwa kuna mauzauza.Siku moja nimeenda kucheki game ya UEFA ya Arsenal na FC Portal kwenye Banda la video pale kijijini.Nikawa nimekaa siti ya nyuma kabisa peke yangu kumbe nikapitiwa na usingizi nikaja kushituka game imeisha halafu niko peke angu.kuangalia saa ilikuwa saa nane usiku asee niliogopa sana.
kulikuwa na njia mbili moja ya barabara nyingine ya mkato.Ile ya mkato ndo inapita kwenye ule mti.niliona uvivu kunyoosha barabara nikasema nipite tu ya mkato.Ile nafika kwenye ule mti pembeni ya barabara nikakuta mwanamke amevaa nguo nyeusi amechuchumaa.Nikataka kujifanya sijaona mara Yule mwanamke akaniongelesha kwa kisukuma "Wewe, unatoka wapi" sikujibu.Akaniuliza tena "unaenda kwa nani" mimi kimya.Akaongea kwa ukali "mtoto mdogo usiku huu unatafuta nini hebu potea hapa haraka" niliondoka pale sikimbii ila nilipoenda mbele kidogo nilitimuka nadhani nilivunja ata record ya Bolt.
Nilipotokeza barabarani nilipishana na gari ambayo nilikua nasikia tu mlio tu ila gari yenyewe siioni.Nilikuja kuumwa balaa mpaka baba akaniombea uhamisho.
Ni issue serious iliyonitokea kijiji flani kipindi hicho ilikuwa wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza ila kwa sasa nadhani ni mkoa wa simiyu.
Angekuwa koboko wote mngeteketea,bahati yenu mlikutana na mchovu chatuNakumbuka nikiwa na miaka kama 9 hivi, nilikuwa na wenzangu 4 tulitoroka shule ile saa nne asubuhi (muda wa chai) tukaenda kuwinda ndege na kuchimba sungura huko Tabora (Kijiji cha Kigwa). Tuliingia porini tena pori zito kabisa lililoshona mpaka tukapotea bila kujuwa tuliingilia wapi, hivyo tukawa tunatembea tu na kutungua ndege huku tukitafuta sehemu nzuri ya kutokea lile eneo maana tulikuwa katikati ya pori na tulikuwa hatujuwi wapi tulipo kwa hiyo tukawa tunafuata mwanga wa jua tu. Kidogo mbele yetu tukaona kitu kama tawi hivi linataka kuanguka mbele yetu, mwenzetu mmoja akawa jasiri kwenda kulikata ili tuchimbe sungura vizuri kumbe alikuwa nyoka anashuka kuja kutukimbiza. Mwenzetu alipofika tu akagongwa mkononi na usoni then yule nyoka alishuka na kuanza kujipanga kutufuata sie...nasi kuona vile kila mmoja wetu akakimbia kivyake maana tulikuwa hatujuwi wapi tulipo. Mbeleni huko kukawa na uwazi fulani hivi, tukasimama na kujikuta tuko wawili tu wenzetu wengine hatukujuwa walikimbilia wapi. Tukawa tunawaita bila kujibiwa, kurudi kijijini tukawatafuta hatukuwaona. Usiku ule wazazi wao na polisi wakawa wanawatafuta na wakaja mpaka pale kwenye ofisi ya CCM kuulizia watoto wengine kama waliwaona wenzetu hao. Usiku wa manane wakaja mapolisi na wazazi wa wale wenzetu na kuhamsha wazazi wangu wakitaka kuongea nami kwani kuna mtu aliwaambia mara ya mwisho wale wenzetu walikuwa na mimi. Nikawaambia ukweli kuwa tulitoroka shule na kwenda kuwinda maporini ndipo tukakimbizwa na nyoka. Kwa kuwa ilikuwa usiku, wakaniacha nilale na asubuhi wakaja kutaka niwapeleke eneo la tukio. Kufika kule tukakuta mwenzetu aliyegongwa na nyoka kafa pale pale. Mbele kidogo tukalikuta chatu limeshiba karibu na pango fulani hivi na shati la shule likiwa ndani ya lile pango just next na huyo chatu. Yule chatu akauliwa na kuchunwa ndipo akakutwa mwenzetu mwingine. Hili tukio lilitokea mwaka 1979, na sitolisahau maishani mwangu kamwe. Nilipigwa sana na Mama yangu ile siku na mama alikuwa ananipiga huku akilia kwa hasira mpaka akashikwa na watu asiniue. Utoto ni janga baya sana kwani watoto wanadanganyana mno.
Mchawi Hana jeuri ya kukudhuru kama hujamkosea au kama hafahamu chimbuko lako.Hawezi kabisaDuh wachawi sio watu
Usiwe na akili za kuazima, koboko ni mkali ila ukumbuke koboko anavamia watu tu akiona kazingirwa.