ngebo
JF-Expert Member
- Sep 8, 2017
- 1,684
- 2,127
- Thread starter
- #21
Dah pole sana hukupata tena maruwe ya namna hiyo baada ya kufukuzwa? Na pete uliirudisha?Shukurani kwa mtoa uzi
Siku ambayo sitakuja kuisahau kamwe Maishani mwangu ni kipindi nasoma shule flani kule mkoani ruvuma nikiwa kidato cha sita, nikiwa naishi bweni , ni wiki kadhaa toka nijiapize moyoni mwangu kua ulokole siutaki tena,
Tukiwa tupo bwenini purukushani za viongozi a.k.a vilanja zikiwa zinaendelea za kututaka tuondoke bwenini, nikiwa naharaka ya kubeba material yangu niende darasan Mara niliona Pete( ndio pete unayoijua wewe ya kuvaa kidoleni) iliwa kwenye kitanda flani bila ya kujiuliza na kutafakari niliichua na kuondoka nayo adi darasani, nikiwa naendelea kusoma nikakumbuka juu ya ile Pete akiri yangu ikanituma nivae, nami bila kusita nikaivaa nikaendelea kusoam , Muda wa prepo ulipo isha nilirudi bwenini! Tukiwa tunaendelea na story Mara nikasikia mtu anasema kwa sauti ya chini na akiwa anauliza majirani wake kua kuna mtu amechukua Pete yake! Nilimsikia lakini nilimpuuza na nikapanga nimpe kesho yake, kwa hiyo nililala Nayo! MUNGU wangu nikiwa nimelala sikumbuki ilikua saa ngapi ! ilikuja ndoto ya ghafla nikaona Mtu akiwa amevaa nguo Nyeusi toka juu adi chini na USO wake akiwa ameufunika mkononi akiwa ameshika fimbo flani akaja adi pembeni ya kitanda changu na kuniangalia kwa sekunde kadhaa halafu akaninyooshea fimbo yake kisha akapotea nilistuka na nliogopa sana, nilipo tazama wenzangu nlisikia sauti za kukoroma tu hakna aliejua nini kilinitokea, nililala tena ghafla niliota namuona jirani yangu anapaa juu kitandani kwake akiwa amelala vile vile hiyo ndoto ikakata,------- lakini ghafla tulishitishwa na kelele za juu sanaa kama mtu analia kwa sauti kubwa ,wote tuliamka nakuanza kumuhoji , jamaa akasema nimeona mtu ananipaisha juu ndo nmeanguka! Kumbukumbu zangu zilirejea kwenye ndoto yangu! Lakini sikumwambia mtu yeyote , amini usiamini kesho nilipata msala msala wa ajabu ambao ulisababisha nikafukuzwa shule siku hiyo hiyo, Sitokuja kusahau hii kitu