Uzi maalumu kuelekea mtihani wa kidato cha nne, Maswali na majibu pamoja na Solving karibu tujiandae pamoja

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
24,908
66,310
Wakuu habari , thread hii nimeanzisha makusudi kwa lengo la kusaidia walimu na wanafunzi wa kidato cha nne ambao wanajiandaa na mtihani wa TAIFA (NECTA).

Here we go!.

Mimi nitatoa hints au vidokezo katika masomo yafuatayo.

Civics
History
English
Kiswahili

Karibu Sana , tuwasaidie vijana watimize ndoto zao.
 
Leo nitazungumzia somo la history upande wa ramani.

Swali la ramani katika mtihani wa kidato cha nne huwa lina marks 11

Hivyo ni swali muhimu kulijua na kuelewa mbinu mbali mbali.

Tunaanza .

Ramani Ambazo unabidi kuzifahamu hasa hasa zipo tano

- unabidi kujua ramani ya Africa
-unabidi kujua ramani ya Tanganyika
-unabidi kujua ramani ya East Africa
-unabidi kujua ramani ya reli ambayo wakoloni waliiweka kipindi cha uchumi wa kikoloni.
-unabidi kujua ramani ya historical site .

Hizo ramani ili kujibu maswali yake ni rahisi Sana

Tutaanza na ramani ya Africa .

Ukiambiwa chora ramani ya Africa na uoneshe nchi kadhaa basi utabidi kufanya yafutayo kwanza katika usomaji wako.

Utaanza kuangalia nchi ambazo zina matukio ya kihistoria.

Tunaanza

South Africa - hapa utaangalia matukio ya kihistoria yote yaliyowahi kutokea south Africa

Kama

-Mfecane war
- Boer Trek
-Kufungwa kwa Mandela miaka 27
-kupata Uhuru wa watu wachache minority rule 1910
-kupata Uhuru wa watu wengi 1994
-Soweto

Baada ya hapo ukishajua hizo historical events za south Africa

Utakapoulizwa swali katika Map of Africa kuwa chora ramani na utuoneshe nchi ambayo ilitokea mfecane war utakuwa ushajua ni south Africa

Huu ni utangulizi

Insh ALLAH nitakuwa naleta madini kila nikipata muda
-
 
Kazi nzuri sana mkuu, endelea kushusha nondo ziwasaidie vijana wetu wanao soma shule za Kayumba
 
Nipo hapa kwa ajiri ya kujibu maswali yote ya historia. Niligonga A safi ya somo hili na nikawa mwanafunzi pekee tangu kuanzishwa kwa shule hiyo kupata A kwa masomo yote,na tangu 2019 mpaka sasa rekodi hii bado haijafikiwa.
 
1. Statistics
2. Matrix and transformation
3. Linear programming
4. Functions
5. Accounts
6. Three dimensional figures
7. Variations
8. Coordinate geometry
9. Sets
10.Numbers

Mwanafunzi akiweza kumudu hizo topics 10 nyepesi kueleweka, tayari ana C au B ya Basic Mathematics.

Mtu akifeli Hisabati O-level ni mzembe au hajui kusoma kwa malengo
 
ukiwa na D ya maths ni umefeli?
 
History njoeni hapa nataka kukumbushia mchungu waliyoyapata wazee wetu enzi hizo kama ilivyo katika avatar yangu cc K11
 
History njoeni hapa nataka kukumbushia mchungu waliyoyapata wazee wetu enzi hizo kama ilivyo katika avatar yangu cc K11
Tutaanza na Ku solve past paper kuanzia 2005.

Past paper hizi zinapatikana katika maktaba tetea google.

Welcome

Tutasolve essays questions and Map

Ur most welcome
 
Wakuu habari , thread hii nimeanzisha makusudi kwa lengo la kusaidia walimu na wanafunzi wa kidato cha nne ambao wanajiandaa na mtihani wa TAIFA (NECTA).

Here we go!.

Mimi nitatoa hints au vidokezo katika masomo yafuatayo.

Civics
History
English
Kiswahili

Karibu Sana , tuwasaidie vijana watimize ndoto zao.
Safi sana, niko na wewe kwenye hayo masomo ya arts. Anza na format za hiyo mitihani ili mwanafunzi ajue picha ya paper
 
History njoeni hapa nataka kukumbushia mchungu waliyoyapata wazee wetu enzi hizo kama ilivyo katika avatar yangu cc K11
Sawa hongera sana, na mimi nipo hapa kuhakikisha ninatoa mchango wezeshi wa ushauri upande wa Mathematics ili kumuenzi binadamu ninayemhusudu sana duniani kuwahi tokea aliyepo kwenye avatar yangu ( Cauchy).
 
Back
Top Bottom